Sijawahi kuelewa kwa nini mtu amtafute baba yake, baba ambaye hajamtafuta.
Human psychology is very complex Kiranga. Kuna mambo hata waliobobea katika fani hii hawajaelewa wakamaliza.
Na hili ni la kawaida sana. Ungependa kujua character traits zako zinatoka wapi. Inakupa raha kujitambua.... Kujitambua Kiranga; that's all.
Nadhani catch ni kumtafuta rafiki yake mama aliokuwa msichana kipindi kimoja, na sasa ni mtu mzima. Atatoa details
tu. Wasichana hawanaga siri hata kidogo wakiopoa kidume kinaaminika kuwa na hela. Lazima watakuwapo marafiki zake mamake huyu binti wanajua habari za baba huyo; na kutoka kwa huyo sasa tafuta marafiki zake babako wa kiume. Marafiki zake mama watamhurumia tu mtoto wampe details....
Haya we kabinti tafuta marafiki zake mamako wa enzi hizo... Kama mamako hajui JF atakuwa hajaona haya maelezo. Unaeza hata kumuuliza yeye mwenyewe eti marafiki zake wa enzi hizo wanakaa wapi: "anza hivi...hivi we mama mashosti zako wa enzi hizo wako wapi siku hizi"... pata wawili watatu; anzia hapo.
Haya ubarikiwe....umeishi miaka zaidi ya 20 bila yeye vipi tena leo unamhitaji zaidi. Yeye pia anawajibika kukutafuta, yawezekana kweli alikufa kwenye MV Bukoba.
Ningekuwa mie wewe, kwanza ningempongeza mama for being there. Angeweza kuwatelekeza. Lakini ameonyesha yeye ni mwanamke kweli na kukomaa na wanawe. Baba ambae hana time na mimi, hata tukikutana kwa bahati mbaya atahitaji kuwa na sababu nzuri sana sana za kwa nini hakuweza kuwa kwenye maisha yangu japo kwa barua!
Move on, like ur mom! Kafa huyo kwenye ajali ya mv maisha! Unaweza kumjua akaishia kukumess up tu! Na kukuvuruga for the rest of your days. Haumuhitaji kwa ajili ya maisha yako kuwa complete!
Umenena, anaweza kumtafuta akaja kumpata alafu baadae ikawa nongwa,......inatokea sana katika maisha mtu hajui ulikuwa unaishije, alafu unamtafuta ukimpata anajiona yeye ndo anastahili kufanyiwa kama mzazi. Anasahau yote aliyokutendea.....mambo ya binadam hayooo
Mtu ambae hajajishughulisha na shida na challenges zangu za maisha out of nowhere aanze kunihusisha na matatizo yake? Hell no, huyo angechangia mbegu yu aisee. Agu wanakuwaga very demanding manake hawana huruma wala nini!