Uko kwenye ndoa zaidi ya miaka 5?naomba ushauri.

Mkuu Herald si umuelimishe hapa hapa na sisi wengine tuelewe/Au kuna shida ukiwaeleza na wengine tusije kuangukia huko?Does it matter ukimueleza yeye kwa email au kutuandikia sote tukasoma?wengine tumenyamaza lakini tunasoma,si unaona wangapi tumetia macho mkuu?tuelimishe sote kama haina gharama.Asante pia kwa dada Ashadii.
 
Ndg zangu wana JF,
Hivi mtu akiomba msaada wa ushauri ni busara kumtukana kwa kosa alilolifanya au unampa ushauri -uwe mzuri au mbaya?
Mimi nilichouliza wengi wamenijibu lakini nasikitika na pretenders!
I had a friend ambae mke wake alitaka kumkata shingo-kwa kisu kwa sababu ya ulevi na kurudi usiku, siku ya kumkata shingo bahati mbaya kumbe siku hiyo jamaa hakuwa amelewa sawa sawa, akamkata kidogo,lakini mume alipotoka hospitalini baada ya siku kama 14 za kulazwa akawaita ndg na marafiki wengi wa karibu na kuwaambia kinyume na wengi mnachotegemea nimewaita ili nimsamehe mke wangu-hivi ndio alivyojisikia na ilikuwa ni kinyume na ushauri wa wengi waliompa.
Sasa mimi katika njia yangu ya kuogopa kufa kwa ukimwi au kupunguza chances za kuogopa kufa kwa ukimwi,nimeamua kupunguza njia moja,sasa mtu ukiniuliza kwanini ulimfuata huyo mama wa 2, wakati ni jambo nimeishaliombea msamaha na nimekubali makosa unakuwa unataka niseme nini cha kukufurahisha.
Kama alivyosema mwana JF mmoja hapo juu, tuombeane,sio wote waliopata HIV kuwa walikuwa wajinga saaana!
Hii HIV does not depend on your brain only!mke wako anaweza kubakwa na mtu mwenye HIV asikwambie na ukakuta wote mmeambukizwa,wote tuna ndgu na watoto-si lazima jambo kama hili likukute wewe tu,sijui kama kuna mwanaume mwenye control kwa mke wake au vice versa,
Nawapenda nyote.
Tuombeane!


TMK hapa kuna members wa kila aina, mawazo ya kila aina na hoja za kila aina, hao hao members nao wana maisha yao ambayo pia yahusisha Mapenzi, na waelewa kua Mapenzi yanauma (for naamini hapa upo kuumia); hio inapelekea wengine kuguswa na post yako ya ushauri (ukute yamewakuta kama hayo uliomfanyia mkeo) na kuna wengine ambao tu anakukejeli/kemea/tukana kwa sababu mbali mbali.

Hata hivo kubali ukatae umeonekana a Hypocrate... as much as kweli tatizo lako ni kubwa; kitendo cha kuogopa UKIMWI sababu mkeo katoka nje na hukuogopa hali uko na hio nyumba ndogo ndicho hasa kimeboa wengi... Hebu liangalia upya hata wewe utaona hapo umechemka....

Kingine sio kila mabaya/negative lisemwalo ni baya... Mengine yanajenga. Naamini kua katika hoja ambazo hujazipenda humu kwenye thread nyingine nyingi ni za kukujenga. Wewe tuliza tu akili na chukua kila uliloambiwa na uchanganye na zako.
 
mwisho wa dhambi ni mauti,anaogopaje ukimwi wakati yy ndo alie anza??ko angeuleta yy je?wanawake huwa wanatuvumilia sana katika uzinzi wetu ila hapo pa kufikia mpaka kuzaa inamana haikua tamaa ulimpenda kabisa.ntarudi kwa ushauri
 
Ashadii hapo pekundu nadhani panategemea na moyo wa mtu ulivyo katika kubeba mtihani mpya.Labda ndo mana mtoa mada akahitaji walioko ndoano kwa miaka mitano na zaidi,maana mim kwa kweli sijui nitawezaje kudumisha amani pale nitakapojua mwenzangu ana mpenzi mwingine huko nje.Nisingetembea na ndugu zake lakini pia nisingereact vizuri,kwa hiyo amani ingepotea.Kwanza mim kujua tu amenisaliti amani itatoweka moyoni mwangu.Kwa kweli ni vizuri kutumia busara ktk mambo kama haya lkn huwezi kujua huyu mama alichanganyikiwa kwa maumivu kiasi gani hadi akafikia kufanya hayo aliyoyafanya.Mim naona baba ndio chanzo cha kuvunjika kwa hii ndoa,kama itavunjika.

In Blue; When young in most cases kila mwanamke hufikiri in those lines... Hasa kama hujaolewa ama umeolowa na your marriage bado ni young, tuombe uzima.... Huo msimamo huenda ukabadilika with time tokana na forces mbali mbali.... Mungu akujaalie uje Uolewe na kama umeolewa basi ndoa yako iwe ni ya kudumu. When this happens (sisemi lazima i happen) then; that is when utaelewa nilikua na maana gani.... Of coz Amani na trust vinabomoka na kuvunjika kabisaa... BUT what you both do baada ya hapo is what counts... kua huo mbomoko mtau treat vipi?

In beige; Queenkami sometimes we are funny creatures.... sie wanadamu. Kitu kama hiki hamna ambae hujua atafanya nini hadi itokee... WHY? Kusikia ama kujua kwa usaliti the way wewe uta react yategemeana na mengi. Kumbuka kua sio ndoa zote zinakua defined in the same way... Lets say bahati mbaya ulishawahi tereza na uli cheat kwa mumeo siku ukisikia kakucheat reaction yako na kuumia ni tofauti kabisaa na ukifananisha na kama ungekua hujawahi cheat. Lets say humo ndani mwaisha yenu ni vulu vulu, mume ni mlevi/un reliable/Mvivu/hana focus na maisha/hakujali wala nini yaani yupo yupo tu kama picha such a Man ukisikia kakucheat Imani yangu ni kua hutaona ajabu na kukuuma ni tofauti na kama hizo traits angekua opposite. Ok Lets say ni sensitive kwako/anakupenda wewe na wanao ipasavo/ ni good dad na hubby/ yupo responsible na reliable na a lot of other qualities thou hawezi kosa madhaifu... katereza ka cheat... Queenkami utaumia mno... BUT will you leave him?

Haya mambo sio black and white thou majority twapenda chukulia hivo... Ni magumu muno na kila case (hata zikiwa 50) hata kama wote tatizo ni moja la Cheating... kila moja ya hiio case ni unique...
 
Muombe msamaa mke wako na mfungue ukurasa mpya kabisa utashangaa mnaweza kuwa na ndoa nzuri ajabu.Hii ilishatokea kwa dadangu nae aliamua kuokoka kutokana na mumewe kuwa na nyumba ndogo yenye watoto.lakini hakubadilika,dada wa watu akaamua kutafuta wake na alikuwa adai talaka na waoane na mwanaume mwingine.Mumewe alipogundua kwamba mkewe anataka aolewe tena aliumia sana na ugomvi ulikuwa mkubwa,ndugu walishindwa kusuluisha,walipotengana kwa miezi mitatu wakagundua hamna anayeweza kuishi bila mwenzake kwani mwanaume alipatwa na maradhi ya ajabu na mwanamke maisha ya kulea watoto mwenyewe yalikuwa magumu kwake hatimaye wenyewe wakarudiana na wanaelewana na kuheshimiana kuliko hapo awali.
Hivyo angalieni na muanze upya kwani mwenzako nae ni binadamu na ana mahitaji hasa kupendwa na kuthaminiwa,utakapompenda na kumthamini hata uwe na nyumba ndogo mbili haitamsumbua.Watoto acha wawe wakubwa watakuja fahamiana.
 
Back
Top Bottom