Uko kwenye ndoa zaidi ya miaka 5?naomba ushauri.

Sijuhi na uko nje anatumia condom au anadhani mwenye possibility ya kumuua kwa ukimwi ni wife tu?

Huyu mkeo atakuwa ameamua kusali lakini akagundua aisaidiii wewe unaendelea na kimada wako.
Akaamua kuchukua hatua nyingine ya kutafuta na yeye mpango wa kando.

Kama ungeachana na huyo kimada nina hakika wife wala asingefikiria revenge; tatizo umezaa na mkeo kajua afu unaendelea. Kaona isiwe tabu wanaume wako wengi tit for tat
 
Asanteni ndugu zangu wana JF!
Nilikuja hapa kuomba ushauri nikijua ni mkosefu.
Lakini mwanume anayeniita mimi mjinga,sina akili, sina dini-namuombea asije kabisa akapatwa na mwanamke wa design hii iliyoniangukia, na sijui kwanini wanaume wengi hujidai wao ni wataalamu wa kukwepa wanawake wakati kiukweli wengi wao si kweli.
Katika kushauriana,NIMEKUBALI KUTUBU KWA MANENO NA VITENDO i.e kumueleza bibie kuwa naumomba msamaha

Lakini cha kushangaza wanaume wengi wanarudia kutoa lawama as if nimekataa kuomba msamaha,jamani NAJUA MIMI NDIE MWENYE MAKOSA,lakini sitaki kuingia kifo ninachokitabiri kwa sababu nimekosa.
Nimemuomba bibie tukapime,nimuache bibie wa nje,nimweleze mbele yake na yeye amuache ndugu yangu amweleze mbele yangu,lakini bibie amesema bora afe kuliko kumtaja mpenzie(mdogo wangu).
Kilichofuatia nimempa vitu vyote vya familia kimaandishi na mimi nitajua nitakakoelekea,maana ukimwi niliisha uona, Hapa kwenye JF nawashukuru ambao hawakunitukana,mungu awazidishie hekima.
Nawashukuru kina dada ambao wamenishauri kuwa huwa hawapendi kuona watoto wa mwanamke mwingine sikulijua hilo.
Siku njema!
 
Jaribu kumwambia tena ulivyomwambia afu hiyo sentensi kwenye red isomeke "nimemwacha" na si "nimuache"
Usikate tamaa kuijenga ndoa yako upya. Kwani unakotaka kuelekea; kwenye divorce life, huwezi jua kama pia ni maisha ya starehe na safe (hakuna HIV). Fikiri na watoto mlio nao watakuwa na malezi gani? Ya baba au mama wa kambo??? Tafuta watu mnaowaamini wawasaidie kuangalia tatizo lenu kwa jicho la tatu.

Na kama ni kweli mkeo anatembea na ndugu yako mbona easy; kwa nini usihusishe ndugu zako kumkanya huyo nduguyo? Kingine una ushaidi gani kama mkeo ana mpenzi leave aside mpenzi huyo ni ndugu yako.. Unaweza kuwa unamlazimisha akubali kosa ambalo hajatenda. Kuna wanawake wana act kama wana wapenzi ili kuwakomoa waume zao; pengine hana mtu yeyote wa nje.


 

usikate tamaa na ndoa yako,jipe nafasi ya pili cha msingi rekebisha makosa yako,inawezekana mkeo hana uhusiano na ndugu yako as you think labda anapretend ili kukurusha roho,ongea nae mjipange upya kuendeleza ndoa yenu..
 
Ndoa ikishafikia hatua hiyo ya kurevenge sio hatua njema. Ni bora hiyo ndoa ivunjwe ili kila mtu awe huru wa kufanya mambo yake awezavyo kuliko kufanya mambo ya aibu kama hayo.
 
kama bado una mapenzi nae jitahidi kutafuta sln maana sln haina cku husiku ipo cku mambo yatakaa sawa pia jiweke karibu na mungu
 
Ukimwi unaweza letwa na mkeo ila wewe huwezi uleta kupitia nyumba ndogo yako! UNAMAPEPO WEWE MWOMBE MUNGU AKUSAMEHE
 
Umechelewa sana kuomba ushauri na kulishuhuria hilo swala kwa uzito uliotakiwa, kwa hali mliofikia haina tiba tena kwani hata mkifanikiwa kurudiana hilo kovu ni kubwa sana halitaweza kufutika katika mioyo yenu.
Ushauri wangu huyo bi mkubwa hafai tena, mpe talaka yake akagange mbele.
 
Asanteni ndugu zangu wana JF!
Nilikuja hapa kuomba ushauri nikijua ni mkosefu.
Lakini mwanume anayeniita mimi mjinga,sina akili, sina dini-namuombea asije kabisa akapatwa na mwanamke wa design hii iliyoniangukia, na sijui kwanini wanaume wengi hujidai wao ni wataalamu wa kukwepa wanawake wakati kiukweli wengi wao si kweli.
Katika kushauriana,NIMEKUBALI KUTUBU KWA MANENO NA VITENDO i.e kumueleza bibie kuwa naumomba msamaha

Lakini cha kushangaza wanaume wengi wanarudia kutoa lawama as if nimekataa kuomba msamaha,jamani NAJUA MIMI NDIE MWENYE MAKOSA,lakini sitaki kuingia kifo ninachokitabiri kwa sababu nimekosa.
Nimemuomba bibie tukapime,nimuache bibie wa nje,nimweleze mbele yake na yeye amuache ndugu yangu amweleze mbele yangu,lakini bibie amesema bora afe kuliko kumtaja mpenzie(mdogo wangu).
Kilichofuatia nimempa vitu vyote vya familia kimaandishi na mimi nitajua nitakakoelekea,maana ukimwi niliisha uona, Hapa kwenye JF nawashukuru ambao hawakunitukana,mungu awazidishie hekima.
Nawashukuru kina dada ambao wamenishauri kuwa huwa hawapendi kuona watoto wa mwanamke mwingine sikulijua hilo.
Siku njema!

As a woman, I can see kwa nini mama anakuwa mgumu kusamehe. Wanawake wengi tuna mapenzi na wanaume wetu lakini pale moyo ukisha umia ni vigumu sana ku forgive and forget. You have to understand when a woman decides to walk out, anakua amevumilia vya kutosha...by the time unakuja omba msamaha the damage is already done, there might be nothing you can do (When a woman's fed up - by R. Kelly)
Nakusifu sana kwa kukubali makosa and willingness to work it out. Unfortunately mama amegoma...bembeleza tena but make sure you mean it (no more nyumba ndogo) kama akikataa basi. Cha muhimu jisamehe wewe nafsi yako for everything you did to her but also forgive her then MOVE ON.
May God protect and help us all.
 

Ila wewe ndugu una vituko sana. Unataka mkapime kwa kuwa mkeo kakurusha roho. Mbona hukumwambia mkapime kabla na baada ya kuzaa nje?

Ki ukweli maelezo yako yanakera sana. Mie ni mwanamume, mwenye familia na uzoefu wa kutosha wa maisha ya ndoa. Kwa ufupi nakueleza kuwa umeniudhi sana tena sana!

Babu DC!!
 
Ndg zangu wana JF,
Hivi mtu akiomba msaada wa ushauri ni busara kumtukana kwa kosa alilolifanya au unampa ushauri -uwe mzuri au mbaya?
Mimi nilichouliza wengi wamenijibu lakini nasikitika na pretenders!
I had a friend ambae mke wake alitaka kumkata shingo-kwa kisu kwa sababu ya ulevi na kurudi usiku, siku ya kumkata shingo bahati mbaya kumbe siku hiyo jamaa hakuwa amelewa sawa sawa, akamkata kidogo,lakini mume alipotoka hospitalini baada ya siku kama 14 za kulazwa akawaita ndg na marafiki wengi wa karibu na kuwaambia kinyume na wengi mnachotegemea nimewaita ili nimsamehe mke wangu-hivi ndio alivyojisikia na ilikuwa ni kinyume na ushauri wa wengi waliompa.
Sasa mimi katika njia yangu ya kuogopa kufa kwa ukimwi au kupunguza chances za kuogopa kufa kwa ukimwi,nimeamua kupunguza njia moja,sasa mtu ukiniuliza kwanini ulimfuata huyo mama wa 2, wakati ni jambo nimeishaliombea msamaha na nimekubali makosa unakuwa unataka niseme nini cha kukufurahisha.
Kama alivyosema mwana JF mmoja hapo juu, tuombeane,sio wote waliopata HIV kuwa walikuwa wajinga saaana!
Hii HIV does not depend on your brain only!mke wako anaweza kubakwa na mtu mwenye HIV asikwambie na ukakuta wote mmeambukizwa,wote tuna ndgu na watoto-si lazima jambo kama hili likukute wewe tu,sijui kama kuna mwanaume mwenye control kwa mke wake au vice versa,
Nawapenda nyote.
Tuombeane!
 

Hapo kwenye red nazidi kuona jinsi mwanaume anavyo LEGALIZE makosa yake, na kuyafanya yale ya mwanamke ndo makosa tena yanayonuka. Hivi, mwanaume alipoanza kutembea nje ya ndoa hadi kuzaa hakumweka mkewe wa ndoa katika hatari ya kupata ukimwi? Iweje baada ya mwanamke kutembea nje mwanaume awe na hofu ya kutembea na mkewe wa ndoa akiogopa ukimwi? Rejea msemo usemao KUNYA ANYE KUKU, AKINYA BATA KAHARISHA! looh!

Anyway, sitetei alichofanya mwanamke ina ninamlaumu mwanaume kuwa ndio chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yake. Sishauri divorce wala separation ila wanandoa hao wasameheane tu na waishi kama zamani.
 
ironically!?..................YES!......I bet it was meant to read.."sacred".
 
wakati mwanamume anatembea nje hadi kutoa mimba hakujua kama kuna ukimwi, ila mwanamke aliporenge ndo anajua, sasa huyo mwanaume atajiju. na ole wako hao watoto haramu niwakute wakijichanganya na wa nyumba kubwa.
 

segere umeanzisha mwenyewe kucheza unakimbia, utakomaje?? (wanawake oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee)
 

Bora umetukumbusha ndoa ni nini dear....good analysis IMO
 

TMK.....unaokelekea sio kuzuri

Kumbuka hapa JF kuna watu wa aina mbali mbali na wana mawazo tofauti...wengine hawawezi kukupa mawazo ambayo ungependa kuyasikia tu

Kimsingi nakuelewa and I feel a pity kwa mkeo ambaye ameshindwa kukuelewa pia na kukusamehe...

Cha msingi, nenda kampime kama bado, ukijihakikishia uko safi, then maadam umeshamwandikisha 'kila kitu' mkeo, basi tengana naye nenda kwa nyumba ndogo yako pamoja na watoto muanze upya maisha.

Mwache aendelee na mdogo wako...mwisho wake utajulikana tu.
 

Ashadii hapo pekundu nadhani panategemea na moyo wa mtu ulivyo katika kubeba mtihani mpya.Labda ndo mana mtoa mada akahitaji walioko ndoano kwa miaka mitano na zaidi,maana mim kwa kweli sijui nitawezaje kudumisha amani pale nitakapojua mwenzangu ana mpenzi mwingine huko nje.Nisingetembea na ndugu zake lakini pia nisingereact vizuri,kwa hiyo amani ingepotea.Kwanza mim kujua tu amenisaliti amani itatoweka moyoni mwangu.Kwa kweli ni vizuri kutumia busara ktk mambo kama haya lkn huwezi kujua huyu mama alichanganyikiwa kwa maumivu kiasi gani hadi akafikia kufanya hayo aliyoyafanya.Mim naona baba ndio chanzo cha kuvunjika kwa hii ndoa,kama itavunjika.
 
Huu ni ushahidi usiopingika kwamba wanaume ni very weak linapokua suala la ngono!!!

Yeye katembea nje hadi kuzaa na kuona ni sawa; ila wife kaguswa tu ndipo anakumbuka magonjwa ya zinaa!!!

Babu DC!!

Huyo mwanaume ni mbinafsi kosa akifanya yeye sawa akifanya mkewe ndo analiona kosa! Yeye ameenda amepiga nje bila hata condom, hadi mtoto amezaliwa anachukulia poa tu, still anaendelea na huyo mwanamke eti anahalalisha ukewenza nani atakubali upuuzi huo? Unadhani kulala ndani ya nyumba ndo nini kama ukiamka asubuhi unaenda nyumba ndogo, ukitoka job unaanzia small house! Acha hiyo kitu tabia ya kucheat hadi unazaa mtoto huko no!no! Pls, tena hawa wanaume ni wa puuzi huwa wanawabembeleza hawa small house zao ziwazalie watoto! Na nyumbani watoto anao basi misifa tu unadhani kuzaa nje ya ndoa ndo ujanja? Mwache mkeo atafute pumziko la moyo wake maana ww umeshaligawa hilo penzi,
 
Ndugu yangu kama mwanaume mwenyewe ni wewe, nipigie simu nikusaidie kabla sijairusha kwa wanajamii...usiieleze katika nafsi ya tatu, Sema Jamani mtu huyo ni mimi ili tusiassume majibu....ila kwa ufupi kuna makosa na dhami ambazo wanume tumejihakikishia kuwa tumezimiliki kumbe twajidanganya.

Nipigie haraka au weka namba yako hapo mimi nitakupigia kwa gharama zozote., au tuma email katika thanda.rsa@gmail.com

Usicheze na moto hata siku moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…