Ukiwa huna kitu hakuna mtu atayejishughulisha na wewe ila ukipata tegemea yafuatayo

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Kama kichwa cha habari kinavyojielezea hapo mtu ukiwa huna kitu hakuna binadamu atayejishughulisha nawe ila ukipata tegemea yafuatayo:

1. Ndugu au marafiki kukushawishi uingie kwenye biashara fulani hivi ambao wao wanaona zinalipa.

2. Ndugu na marafiki kukupa taarifa za kibiashara kuhusu viwanja, nyumba, wapi vinauzwa

3. Ndugu na marafiki kukushirikisha katika mipango yao ya kuoa au kuolewa.

4. Ndugu na marafiki kukuona wewe ndio kama msaada katika maisha yao na chochote ufanyacho juu yao hukwambia Mungu akubariki

5. Kila siku tegemea kupokea simu zaidi ya kumi ya ndugu jamaa na marafiki kukujulia hali na kukusalimia.

Haya endeleeaaaaaaaa
 
Kupewa nafasi ya kuwa msemaji mkuu ktk familia,hata kama ndugu yako ni mkubwa kwko na ana mawazo mazuri kuliko wewe ataambiwa atulie kukupisha wewe mwenye fweza hata kama unaongea rubbish utaskilizwa hivyo hivyo mpaka kikao kinakwisha vilevile japo kaongea pumba ndugu watampigia makofi vigele gele na kumpongeza kwa ushauri mzuri ndani ya familia yetu kama kuna jambo hata kama ni la kijinga nyie wengine mnaombwa mpishe wanataka kuteta hata kama nyie ni wakubwa.

Wabongo buana ni wanafiki sana yaani mwenye fweza hata akijamba ndani ya kikao watamtengenezea sentensi nzuri kwamba huyu anatatizo la kuumwa tumbo toka jana kwa hiyo tumvumilie wanafamilia watajibu ''haina sheeda tuendele na mambo mengine hilo tuliache mbona kawaida tu''

wanaogopa hata kuziba pua japo kishuzi kinanuka mno wanahisi wataonekana wamemdharau jamaa..sasa jamba wewe maskini utasemwa wewe mpaka utatamani uchukue kitanzi ukajinyonge.hayo ni kawaida hapa kwe2 africa.
 
Umaskini mbaya sana
Kwenye ukoo wetu mimi na vikao nashiriki lwa lazima la sivyo ntaenda kuosha masufuria staki kusikiliza upuuzi wanaoongea watu wenye hela na vile wanavyowasapoti. Sijawahi kutia neno maana ndio sie tunaoleta vurugu
Ha ha ha
 
Kama kichwa cha habari kinavyojielezea hapo mtu ukiwa huna kitu hakuna binadamu atayejishughulisha nawe ila ukipata tegemea yafuatayo:

1. Ndugu au marafiki kukushawishi uingie kwenye biashara fulani hivi ambao wao wanaona zinalipa.

2. Ndugu na marafiki kukupa taarifa za kibiashara kuhusu viwanja, nyumba, wapi vinauzwa

3. Ndugu na marafiki kukushirikisha katika mipango yao ya kuoa au kuolewa.

4. Ndugu na marafiki kukuona wewe ndio kama msaada katika maisha yao na chochote ufanyacho juu yao hukwambia Mungu akubariki

5. Kila siku tegemea kupokea simu zaidi ya kumi ya ndugu jamaa na marafiki kukujulia hali na kukusalimia.

Haya endeleeaaaaaaaa
Mkuu hyo namba 5 ndy fact kabisa.... Pia tegemea ndugu kuja kutembea nyumbani kwako na hujuwi wataondoka lini
 
Back
Top Bottom