Ukivuta sigara hadharani Zanzibar kukiona

Ukivuta sigara hadharani Zanzibar kukiona

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,698
Reaction score
2,262
Na Mwashungi Tahir – Maelezo

Wizara ya Afya imezindua kanuni ya udhibiti wa matumizi ya Tumbaku ikiwa ni mkakati wa kupambana na ongezeko la Matumizi ya Tumbaku kwa jamii ya Zanzibar.

Hafla ya uzinduzi huo imefanywa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Harusi Saidi Suleiman huko Wizara ya Afya mnazi mmoja.

Akizungumza katika hafla hiyo Naibu huyo amesema jamii ya kizanzibari inakabiliwa na changamoto kubwa ya matumizi ya tumbaku ikiwemo uvutaji wa sigara.

Amesema Sigara ni bidhaa halali inayoingizia Serikali mapato kupitia kodi, hata hivyo mbali na mapato yanayopatikana , matumizi yake yamethibitika kuwa ni athari kubwa mno kwa mtumiaji pamoja na wanaomzunguka .

“Ifahamike kuwa tumbaku ina aina nyingi ya sumu ikiwemo NIKOTIN ambayo inasababisha uraibu na husafirishwa kwa njia ya mzunguko wa damu na kuathiri sehemu mbali mbali za mwilini” alisema Naibu huyo.

Alisema tafiti zilizofanywa ulimwenguni zinafahamisha kuwa matumizi ya tumbaku ikiwemo uvutaji wa sigara hupelekea kupata maradhi yasiyoambukiza ikiwemo Saratani za mapafu, kinywa, shingo ya kizazi , ugonjwa wa shinikizo la damu na kisukari .

Aliongeza kuwa matumizi yake huathiri pia mfumo mzima wa mishipa ya damu, maradhi sugu ya kuziba njia ya hewa kusababisha maradhi ya kiharusi.

Akielezea kuhusu Utafiti uliofanyika Zanzibar mwaka 2011 Naibu huyo alisema asilimia 7.3 ya watu katika jamii ni watumiaji wa Sigara na bidhaa zitokanazo na tumbaku, na kwa upande wa wanafunzi tafiti ndogo zilizofanyika imebainika skuli zaidi ya nane zilizomo wilaya ya mjini asilimia 9.5 ya wanafunzi wanatumia bidhaa zitokanazo na tumbaku ikiwemo sigara.

Akizitaja changamoto katika jamii alisema ni matumizi holela ya tumbaku hususan uvutaji wa sigara katika maeneo ya uwazi kama vile majengo yanayotoa huduma za kijamii, maeneo ya burudani, sokoni, viwanja vya mpira.

Naibu huyo alieleza kuwa Zanzibar inashuhudia watoto chini ya umri wa miaka 18 wakishirikishwa kwa njia moja au nyengine katika matumizi hayo na kwamba ipo haja wazazi na walezi kuwa na hadhari kwa watoto wao.

Ameviomba vyombo vya habari na vyombo vya sheria kuzipitia na kuzisimamia kanuni hizo ili kuweza kukabiliana na changamoto za matumizi hayo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mtu atakayeuza bidhaa ya tumbaku ikiwemo sigara lazima bidhaa hiyo iambatane na onyo la afya liililochapishwa kwa wino mwekundu na inayosomeka vizuri.

Kanuni hizo pia zinakataza mtu yeyote chini ya umri wa miaka 18 kutoruhusiwa kujishughulisha na kuuza sigara au kushiriki katika bidhaa ya tumbaku na kanuni inakataza kudhamini na kuhamasisha bidhaa hii ikiwa nchini au nje ya nchi kupitia vyombo vya habari na matangazo yanayohamasisha matumizi ya tumbaku.

Nae Mwakilishi wa Shirika la Afya duniani (WHO) Dr. Matthieu Kamwa amesema tumbaku ni miongoni mwa bidhaa zinazoongoza kusababisha vifo kwa watumiaji wake ambapo zaidi ya watu million saba hufariki duniani kote kutokana na matumizi yake.

Mwakilishi huyo amesema Tumbaku ni janga kubwa ambalo linagharimu uchumi wa dunia ambapo takriban dola za Marekani Tirion 1.2 hutumika kwa ajili ya matibabu ya watumiaji wa tumbaku.

Ameongeza kuwa Shirika la afya ulimwenguni litaendelea na mashirikiano yake na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kutengeneza kanuni zake dhidi yamatumizi ya tumbaku .

“Malengo endelevu ya dunia ni kuona dunia iko salama dhidi ya matumizi ya tumbaku ifikapo 2030 na ni jambo linalohitaji mashirikiano ya kila mdau katika kuhakikisha wanaepukana na matumizi hayo” alisema Kamwa.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa wizara ya Afya Asha Ali Abdullah akizungumza katika uzinduzi huo alisema tumbaku ni miongoni mwa Madawa ya kulevya hivyo ameomba elimu itolewe ili watumiaji waelewe athari zake hasa kwa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa la kesho.

Zenji.jpg

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Bi. Harusi Said Suleiman akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha kanuni ya kuzibiti matumizi ya tumbaku Zanzibar (kushoto alieshika kitabu) ni Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani Dr. Matthieu Kamwa
 
Zanzibar wamejenga chuki na nguruwe bila sababu yoyote, kumbe tumbaku inawaumiza siku zote...
Masikini usilolijua!
 
Hii sheria wailete hadi bara..
Maana inakera mtu anavutia sigara hadharani mbele ya watoto.
Mwisho wa siku moshi wake unaathiri hadi watu wasio na hatia..

Sigara zipigwe marufuku kuvutiwa hadharani..kama mtu anataka kujiua kwa kuvuta basi na afe peke yake sio kuua na watu wasio na hatia kwa kuvuti hadharani

Sent from my SHV-E330L using JamiiForums mobile app
 
Wakafee mbele huko na
Uislam wao tukivuta kwan
Inaingia kwenye mapavu yao
Stupid![emoji15] [emoji15]

[Color= yellow]Triple A[/color]
 
Haya ni mawazo ya ma ccm

Yani hili li sesrikali bhana, kila mda kukurupuka
 
Huwajui wazenji wewe nini sigara bangi inavutwa hadharani beach

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya ni mawazo ya ma ccm

Yani hili li sesrikali bhana, kila mda kukurupuka
Mkuu mimi siko kwenye siasa....niko kwenye medical field ..
Na nineandika baada ya kuona magonjwa mengi kama hypertension ambayo zamani yalikuwa yanatokea sana kwa wazee sasa hivi hadi watoto wanapata..

Moja ya sababu ni uvutaji wa sigara na moshi wake unaathiri hata watoto wadiovuta..

Sasa wewe na upuuzi wako au sijui ni kushindwa kutafsiri mambo kwa jicho tofauti na la kisiasa unapinga kila kitu bila hata kufanya research kidogo kuhusu madhara ya sigara kwa watu ambao hawavuti lakini wanakuwa exposed kwenye moshi..

Acha ujinga

Mawazo mgand kama haya yataondoka nchini siku li CCM likitoka madarakani.

Tatizo lq vijana wa uvccm ndio hilo. Haya umeniambia mi ni mpuuzi, kachukue buku saba yako
 
Mawazo mgand kama haya yataondoka nchini siku li CCM likitoka madarakani.

Tatizo lq vijana wa uvccm ndio hilo. Haya umeniambia mi ni mpuuzi, kachukue buku saba yako
Hii nchi kwa upuuzi kama wako haiwezi kuendelea...
Mimi nimekujibu kwa fact.
Na wewe basi niprove wrong kama matumizi ya sigara hadharani hayana madhara ili tuelewane...
Tatizo lako ni kuwa kila mtu anayekubaliana na tamko la serikali ni uvccm..mimi naagalia faida ya tamko na hasara sio kama wewe huna fact lakini unachokijua ni kubisha vitu ambavyo hata huvijui.

Sent from my SHV-E330L using JamiiForums mobile app
 
kwanini wasifunge kiwanda na kuzuia uingizwaji wa hiyo bidhaa hapa nchini
 
acha chuki za kidini wewe.

The Difference Between Stupidity and Genius Is That Genius Has Its Limits
Tulia ww hayo mashsrt yenu
Yasiyo na mashiko peleken
Huko saudia co tz

[Color= yellow]Triple A[/color]
 
Wakafee mbele huko na
Uislam wao tukivuta kwan
Inaingia kwenye mapavu yao
Stupid![emoji15] [emoji15]

[Color= yellow]Triple A[/color]
Kwahivyo nchi za ulaya ambazo zimepiga marufuku ya uvutaji sigara hadharani nao wakafe mbele na uislamu wao?

Acha ujinga, na uzwazwa!
 
Back
Top Bottom