Ukiumwa nenda Hospital acha kujifanya Daktari Mwanafunzi

Bueno

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2022
Posts
34,610
Reaction score
59,577
Wakuu, juzi kati hapa nilipatwa na kahoma nikawa sielewi elewi mwili wangu huu vipi. Basi mimi na JF Doctaz Jukwaa la Afya ni sehemu yangu ya kupokea maarifa mawili mawili matatu kuhusu magonjwa mbalimbali na Afya zetu, nikajikusanya nikaingia JF nikaanza kuandika dalili kwenye search box pale juu zikawa zinakuja content na maelezo ya Wadau. Nikaandika dawa zangu tayari nikaelekea Pharmacy.

Kabla sijaendelea naomba niseme kitu kimoja, awali ya yote mimi siendi hospital isipokua nikiwa na Ugonjwa serious tu, mfano nikipata Jeraha kubwa ambalo natakiwa kushonwa, nikiumwa sijiwezi nusu kufa nusu kuishi, nikiugua ugonjwa siuelewi elewi yaan hata nikitumia home remedy unadunda hapo lazima nikimbilie hospital.

Tuendelee.. basi mimi huyo nikaenda zangu Pharmacy nikamkuta mwenye ile Pharmacy ambae pembeni ya hio Pharmacy ana Maabara yake Ndogo kwa hio ukienda na ugonjwa fulani akawa hakuelewi elewi anakuingiza maabara anakukagua ndio anakupa dawa.

Basi yule Mfamasia ambae mimi nimemuona km Daktari nilipompa kikaratasi changu za dawa nilizojumua JF nakuziandika km Daktari, kwanza akashtuka hizi dawa anaenda kutumia nani? Nikajibu mimi.. akasema wewe ndio unaugua haya magonjwa yote? Duh hapo ikabidi nishtuke.. aisee kumbe bwana humu JF watu wanajiropokea tu madawa yoyote tumia hii tumia ilee utapona yaan mtu anaandikiwa Dawa ya Bakteria, Dawa ya Fungus, Dawa ya Virus kwenye uzi mmoja ila hawajui ni madawa ya ugonjwa gani.

Akaniuliza unajisikiaje maana mimi nakuona upo sawa tu mboni km ninavyokuona hauumwi wewe? Nikamwambia bro mimi naumwa km unabisha nikuonyeshe naumwa nini.. akasema basi tuingie maabara unionyeshe unachoumwa, mimi huyo tukaingia maabara nikabidi nimuonyeshee ni tuvipele tu niliona tunaniota mwilini ikabidi nimwonyeshee akasema yaan hutu tuvipele ndio unataka ununue ile midawa mikubwa vile ya ma-Virus kwa ki-ugonjwa hiki, kwanza unajua yale madawa ni yanatibu ugonjwa gani na ugonjwa gani?

Ikabidi niishiwe pozi ndio akanifafanulia akanipa darasa la muda mfupi kuhusu dawa zote nilizoziandika, hii inatibu kitu fulani na hii inatibu kitu fulani na akanielewesha kwamba sio vizuri kukupa dawa tu bila kukupima na kujua unaumwa nini, lakini kwa hapa nimeshakuangalia nimejua unaumwa nini na unatakiwa utumie dawa gani? Akanitajia...

Akauliza swali la mwisho.. aliekuandikia hizi dawa huyu ni Mwanafunzi wa Udaktari?

Mimi nikaona isiwe kesi kubwaa sana nikamjibu tu ndio... akaulize yeye yupo wapi nikampa location akasema kwa hio ameekupimaje nikasema nilimtumia picha.. akasema basi amekuangalia vibaya wewe hauumwi haya magonjwa ya hizi dawa.

Twendeni Hospital wakuu japokua Mimi zile foleni tu ndio zinanifanyaga napona haraka sana.
 
Kati ya mambo yanayo sababisha watanzania wengi kuuwa Figo zao Ni kunywa dawa hovyo.
Za kienyeji pia hatari sana.
Baadhi ya clinical officers wa zahanati ndogo nao wanawapa dawa hovyo dozi kali kali wagonjwa wao.
Take care.
 
Mtaani na JF kuna tabia ya watu kujipa udaktari.
"Mimi niliumwa ugonjwa kama huo nikapewa dawa hii. Ninazo zimebaki chukua unywe."
 
Baadhi ya Medical officers wa zahanati ndogo nao wanawapa dawa hovyo dozi kali kali wagonjwa wao.
Take care.
Ni hatari sana mkuu yaan acha kabisa
 
Mtaani na JF kuna tabia ya watu kujipa udaktari.
"Mimi niliumwa ugonjwa kama huo nikapewa dawa hii. Ninazo zimebaki chukua unywe."
Humu mkuu watu wanatisha watu mtu anaanzisha uzi labda anaumwa tu fungus kwenye maeneo nyeti anaomba ushauri afanyaje unakuta anaandikiwa dawa ya Kaswende eti akaitumie na weengine sio wafutiliaji anaandika dawa hio huyo anawahi famasi kuulizia dawa bila kujua ile dawa aliyoandikiwa na mdau ni ya Kaswende na yeye sio mgonjwa wa Kaswende
 
Kati ya mambo yanayo sababisha watanzania wengi kuuwa Figo zao Ni kunywa dawa hovyo.
Za kienyeji pia hatari sana.
Baadhi ya Medical officers wa zahanati ndogo nao wanawapa dawa hovyo dozi kali kali wagonjwa wao.
Take care.
Zahanati hakuna Medical Officer. Kuna Clinical Officers
 
Kati ya mambo yanayo sababisha watanzania wengi kuuwa Figo zao Ni kunywa dawa hovyo.
Za kienyeji pia hatari sana.
Baadhi ya clinical officers wa zahanati ndogo nao wanawapa dawa hovyo dozi kali kali wagonjwa wao.
Take care.
Mbona madokta wa hospitali pia wanaumwa figo mkuu
 
Wakuu, juzi kati hapa nilipatwa na kahoma nikawa sielewi elewi mwili wangu huu vipi. Basi mimi na JF Doctaz Jukwaa la Afya ni sehemu yangu ya kupokea maarifa mawili mawili matatu kuhusu magonjwa mbalimbali na Afya zetu, nikajikusanya nikaingia JF nikaanza kuandika dalili kwenye search box pale juu zikawa zinakuja content na maelezo ya Wadau. Nikaandika dawa zangu tayari nikaelekea Pharmacy.

Kabla sijaendelea naomba niseme kitu kimoja, awali ya yote mimi siendi hospital isipokua nikiwa na Ugonjwa serious tu, mfano nikipata Jeraha kubwa ambalo natakiwa kushonwa, nikiumwa sijiwezi nusu kufa nusu kuishi, nikiugua ugonjwa siuelewi elewi yaan hata nikitumia home remedy unadunda hapo lazima nikimbilie hospital.

Tuendelee.. basi mimi huyo nikaenda zangu Pharmacy nikamkuta mwenye ile Pharmacy ambae pembeni ya hio Pharmacy ana Maabara yake Ndogo kwa hio ukienda na ugonjwa fulani akawa hakuelewi elewi anakuingiza maabara anakukagua ndio anakupa dawa.

Basi yule Mfamasia ambae mimi nimemuona km Daktari nilipompa kikaratasi changu za dawa nilizojumua JF nakuziandika km Daktari, kwanza akashtuka hizi dawa anaenda kutumia nani? Nikajibu mimi.. akasema wewe ndio unaugua haya magonjwa yote? Duh hapo ikabidi nishtuke.. aisee kumbe bwana humu JF watu wanajiropokea tu madawa yoyote tumia hii tumia ilee utapona yaan mtu anaandikiwa Dawa ya Bakteria, Dawa ya Fungus, Dawa ya Virus kwenye uzi mmoja ila hawajui ni madawa ya ugonjwa gani.

Akaniuliza unajisikiaje maana mimi nakuona upo sawa tu mboni km ninavyokuona hauumwi wewe? Nikamwambia bro mimi naumwa km unabisha nikuonyeshe naumwa nini.. akasema basi tuingie maabara unionyeshe unachoumwa, mimi huyo tukaingia maabara nikabidi nimuonyeshee ni tuvipele tu niliona tunaniota mwilini ikabidi nimwonyeshee akasema yaan hutu tuvipele ndio unataka ununue ile midawa mikubwa vile ya ma-Virus kwa ki-ugonjwa hiki, kwanza unajua yale madawa ni yanatibu ugonjwa gani na ugonjwa gani?

Ikabidi niishiwe pozi ndio akanifafanulia akanipa darasa la muda mfupi kuhusu dawa zote nilizoziandika, hii inatibu kitu fulani na hii inatibu kitu fulani na akanielewesha kwamba sio vizuri kukupa dawa tu bila kukupima na kujua unaumwa nini, lakini kwa hapa nimeshakuangalia nimejua unaumwa nini na unatakiwa utumie dawa gani? Akanitajia...

Akauliza swali la mwisho.. aliekuandikia hizi dawa huyu ni Mwanafunzi wa Udaktari?

Mimi nikaona isiwe kesi kubwaa sana nikamjibu tu ndio... akaulize yeye yupo wapi nikampa location akasema kwa hio ameekupimaje nikasema nilimtumia picha.. akasema basi amekuangalia vibaya wewe hauumwi haya magonjwa ya hizi dawa.

Twendeni Hospital wakuu japokua Mimi zile foleni tu ndio zinanifanyaga napona haraka sana.

Rudi kwenye uzi wako huo uyaandike haya, ili kusaidia wengine.

Bila hivyo ni yale yale tu....
 
Back
Top Bottom