Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
UKIUKWAJI WA HAKI UNAOHUJUMIWA NA WABUNGE WA CCM BUNGENI HAUKWEPEKI KAMWE KUNG'OLEWA NA IBARA ZA 21 NA 71(f) ZA KATIBA YETU.
Ibara ya 21(1-2) imeamuru kuwa kila raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi ( yaani Rais, wabunge, madiwani na wenye viti wa mitaa)
Pia ibara ya 71(f) imeamuru kuwa mbunge atakoma kuwa mbunge na ataacha kii chake katika bunge iwapo mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa mbunge.
Ibara ya 21(1-2) inaweza kutumiwa na raia walioungana wa majimbo yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwasilisha kiutaratibu wa kisheria miswada au hoja kwa wabunge wote ndani ya kipindi kimoja walichokubaliana kwa lengo la kuwalazimisha wabunge wote wapitishe miswada hiyo au hoja hizo bungeni bila kukwepa.
Na iwapo mbunge atabainika kutowasilisha mswada huo au hoja hiyo bungeni, raia wana haki ya kumshtaki mbunge mahakamani kwa kosa la kuvunja katiba. Ibara hii ya 21 inathibitisha kuwa ukiukwaji wa haki wa wabunge wa CCM unasababishwa na kutojitambua kisheria kwa raia wa Tanzania.
Ikiwa watanzania tumeumizwa na kuondolewa hoja bungeni ya mheshimiwa Zitto Kabwe ya kuunda kamati ya uchunguzi ya matukio ya utekaji pamoja na hoja ya wabunge wote wa upinzani ya kurejesha bunge la katiba basi tunapaswa kuwasilisha hoja hizo kwa wabunge wote nchini zitakazowasilishwa kwao kwa taratibu za kisheria ambazo hazikwepeki kukanwa mahakamani. Kwa utaratibu huu wa kisheria utawakamata wabunge wanaopinga hadharani kwa kupigia kura za wazi kwenye miswada na hoja zilizo mbele yao.
Na kama mbunge atakataa kupokea mswada au hoja kutoka kwa raia wa kata zote za jimboni kwake basi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake kwa kufuata misingi ya sheria ya katiba yetu.
Pia kwenye jimbo ambalo wana CCM wameweka utaifa mbele kuliko itikadi yao ya kisiasa wana fursa ya kikatiba ya kichama kumfukuza uanachama mbunge asiye wakilisha haki zao bungeni ili aachishwe ubunge wake. Yapo majimbo mengi tu ya CCM ambayo yana wabunge wasiokubalika na wanachama wao wa chama chao na wakatumia fursa ya sheria hii ya kumfukuza uanachama ili afukuzwe ubunge.
Wakati umewadia wa sisi raia kuazisha vita dhidi ya ukiukwaji wa haki bungeni kwa kuwasilisha kisheria miswada na hoja zetu kwa wabunge itakayo walazimisha kuipitisha bungeni bila kupingwa
Kwa hiyo vyama vya upinzani vinapaswa kujipanga kwa pamoja kuteuwa muda wa kuwasilisha miswada na hoja kwa wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwatumia mwanachama wao kama raia wa majimbo yote ya Tanzania.
Ibara ya 21 inawapa haki raia kuwasilisha hoja zao kwa mbunge bila kujali itikadi zao za kisiasa kwa hoja kuwa mbunge alichaguliwa na raia bila kujali itikadi zao.
Kwa kufuata utaratibu huu wa kisheria hakuna hoja itakayopingwa bungeni kwa sababu hata spika na naibu wakiwa kama wabunge watalazimika kupitisha miswada na hoja ambazo zitafanana kisheria na wabunge wote.
Kwa kuheshimu utaratibu huu wa kisheria bunge litaweza kuilazimisha serikali kurejesha bunge la katiba litakalounda katiba mpya, tume huru ya haki ya uchaguzi, ofisi huru ya haki ya msajili wa vyama vya kisiasa na taasisi huru ya haki ya mahakama.
Hayo ndiyo matokeo ya kushindwa juhudi zangu za mwanzo nilizowashauri wabunge wa upinzani ambazo wiki hii zilionekana zikiuwawa kwa kuhujumiwa na uongozi wa spika na kuthibitika unyonge wa sisi wapinzani ndani ya bunge.
Nina imani mfumo wa sheria nilioushauri utatupa uhuru wa kidemokrasia bungeni na nje ya bunge.