Ukitumiwa hela toa shukrani, kujikausha kunakera

Natafuta pesa

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2022
Posts
287
Reaction score
396
Kwema?

Unakuta una mpenzi, rafiki au ndugu wa familia, amekwama, mfano vocha, gas imekata, na mikwamo mingine inayofanana na hiyo,

Kiroho safi unaingia mfukoni, unaenda kwa wakala unamtumia, baada ya kumtumia hata kusema nimeiona au ahsante hakuna, hii kitu huwa Ina kata sana,

Ni kweli unapotenda lililojema yakupasa usisubiri shukrani lakini ukirudi kwenye uhalisia wa kibinadamu kuna faraja mtu anaipata unaposhukuru,

Hata siku nyingine ukikwama tena mtu anakuwa na moyo mkunjufu kukuwezesha.

Kwaheri.
 
kawaida hii, kuna dogo huwa namcheki mwisho wa mwezi nimtumie pocket money ila nikishamtumia anajikausha, mi huwa napaniki nadhani labda pesa haijafika inabidi nianze kumwambia wakala anaioneshe mesej maana nadhani haijafika, nikicheki huyo dogo yeye anachukulia poa tu anasema ilifika mda.

ila kuna siku kwa maksudi sitamtumia nami ntamwambia nilidhani imefika
 
T
Kwema?

Unakuta una mpenzi, rafiki au ndugu wa familia, amekwama, mfano vocha, gas imekata, na mikwamo mingine inayofanana na hiyo,

Kiroho safi unaingia mfukoni, unaenda kwa wakala unamtumia, baada ya kumtumia hata kusema nimeiona au ahsante hakuna, hii kitu huwa Ina kata sana,

Ni kweli unapotenda lililojema yakupasa usisubiri shukrani lakini ukirudi kwenye uhalisia wa kibinadamu kuna faraja mtu anaipata unaposhukuru,

Hata siku nyingine ukikwama tena mtu anakuwa na moyo mkunjufu kukuwezesha.

Kwaheri.
TAbia ya pisi
 
Back
Top Bottom