Tizedi Tizo
Member
- Feb 15, 2017
- 20
- 24
Katika hotuba yake ya juzi na waandishi wa habari nimepata vitu ishirini ambavyo hutavisika kwenye vyombo vya habari.
1. Amezungumzia hili jambo zima la yeye kuhusishwa na urusi ni njama zinazofanywa na wapinzani kumtoa madarakani. Hasa watu wa Hillary Clinton.
2. Akasema vyombo vya habari vya siasa havina uaminifu. Vinathubutu hata kutunga stori inayomuhusu yeye bila hata ya kuzungumza naye. Hii ikiwa ni pamoja na kutangaza hadharani kuwa serikali yake sasa iko katika machafuko wakati ukweli ni kuwa mambo ni shwari kabisa.
3. Suala la email za chama cha democrat kuhakiwa alisema ni uzembe wa Democrat wa kushindwa kulinda servers zao. Ila alishangazwa na upendeleo wa vyombo vya habari kuacha kuzungumzia vitu vilivyogundulika katika server hizo.
4. Uvujaji wa habari za serikali yake unafanywa na watu wa CIA na FBI ambao bado wana mawasiliano na wapinzani wake. Amesema tatizo hilo analitatua kwa kuweka viongozi wake katika ngazi za juu. Akawataja Pompeo na Comey kuwa watasaidia kuzuia uvujaji wa habari.
(Sikujua kuwa Comey ni mtu wake. Wabaya wake wameandika siku ya pili yake kuwa Trump kamfokea Pompei- Inawahusu nin?)
5. Akaendelea kusema uvujishaji wa siri za serikali (classified information) ni kosa la jinai. Na waliovujisha hasa lile zogo lake na kiongozi wa Australia watachukuliwa hatua za kisheria.
6. Michael Flynn alimwachisha kazi kwa kuwa hakuripoti vizuri habari kwa makamu wa rais. Na baadae akasema hakumbuki. Na pia vyombo vya habari vilichangia kuvujisha habari za Flynn
7. Kuhusu ukuta akitangaza kuwa hatua za awali za ujenzi wa ukuta huo zimeanza.
8. Aliulizwa swali kuhusu kusaidia miji ya watu weusi ambayo iko katika hali mbaya kiuchumi na kiusalama. Akajibu ameanza kulifanyia kazi hilo jambo. Ila tatizo ni baadhi ya viongozi wa watu kukataa kukutana nae kwa kuogopa kuonekana wasaliti wa watu weusi. Alimuomba muulizaji swali hilo ambaye alikuwa ni mwanamke mmarekani mweusi aandae mkutano wa kuzungumzia suala hilo.
9. Alichukizwa na swali la kujibu kuwa yenye ni mbaguzi wa rangi. Akachukulia swali hilo kuwa ni tusi.
10. Alitangaza wamo katika hatua za kutangaza mpango wa bima ya afya utakaochukua nafasi ya Obama Care.
11. Akataja makampuni yakiwemo Ford na Intel ambayo yamekubali kubaki Marekani na kuongeza kazi za viwandani kwa Marekani hasa viwanda vya magari.
12. Akaongezea kuwa serikali ipo katika mjadala na bunge juu ya kupata tax nafuu na vivutio vingine kwa kampuni zitakazofanya uzalisha ndani ya Marekani
13. Alizumgumzia mradi utakaoiwezesha Marekani kutumia madini ya chuma (steel) yaliyopo ndani ya Marekani.
14. Alitoa taarifa kuwa wiki ijayo atatoa oda mpya ya kuzuia watu wasiingie Marekani. Oda hii imetengenezwa na wanasheria ikizingatia ile oda ya mwanzo iliyopingwa na mahakama. Isitoshe bado anafuatilia kupitia mahakama kuu ile oda ambayo imekwamishwa mahakamani.
15. Aliwalaumu chama cha Democrat kwa kuchelewesha kupitisha wateule wake wa baraza lake la mawaziri. Kwa makusudi tu ili kazi zake zizorote.
16. Alikubaliana na waandishi wa habari kuwa inachofanya Urusi kupitisha ndege za jeshi karibu na meli za vita ya Marekani si jambo zuri. Ila alisema huenda rais Putin wa Urusi anafanya hivyo kwa kuona watu wamemkalia vibaya Trump haitawezekana kisiasa kwa Trump kufanya dili na Urusi.
17. Alielezea umuhimu wa Marekani kuna na uhusiano mzuri na Urusi. Ameonyeshwa nguvu za nyuklia zilizopo Marekani na walizo nazo warusi. Ni hatari kwa mataifa hayo kutooelewana. Na si Urusi tu hata China na Japan ni muhimu kuwa na mahusiano nao mazuri.
18. Alitangaza kuwa ameshachukua hatua za kulijenga upya jeshi la Marekani liwe na nguvu kuliko nchi yeyote duniani. Ingawaje alisema anatarajia kutolimitumia hilo jeshi.
19. Kutotumia jeshi hilo kunatokana na uwezo wake na baraza lake la mawaziri hasa secretary of state katika kukata madili na masulihisho ya amani.
20. Alirudia kauli yake ya kwenye kampeni kuwa hatatangaza hadharani tarehe na mipango yake ya kivita iwapo atawajibika kuchukua hatua za kijeshi.