Mie jamani huyu shoga yangu wala simwelewi. Mwanzoni mwa mwezi ulopita, alikuja kunazima vidani vyangu vya dhahabu ili kuhudhuria pamvu ya dada yake. Siku kadhaa baadae akaja kunambia kwamba, vidani vyangu vimepotea, lakini akaahidi kunilipa. Sasa naona karibu mwezi wesha, mwenzangu kimya! Juzi nimemkumbusha, imekuwa nongwa. Anapita kila mtaa kuntangaza ubaya.
Jamani wenzangu hebu nambieni, ubaya wangu uwapi? Yaani kudai changu ndiyo niwe mbaya! Vidani vyangu, mwenyewe nimepewa na bibi yangu Al Marhum Bi Kijakazi, leo hii huyu hayawani asiye na haya anletea za kuleta! Mwenyewe nilikuwa na mtoko weekend hii na nilitaka nikaoshee huko kwenye mtoko, lakini huyu majununi ananipa majibu ya kifedhuli. Ama kweli, wafadhilaka wapundaka, heri kumfadhili mbuzi, kuliko binadamu mwenye maudhi!
Eti wana JF wenzangu, nimfanye nini huyu baradhuli?
Zinduna, hilo liwe ni fundisho tosha kwako, usimuazime mtu kitu chako chochote "personal" iwe dhahabu, fedha, shaba, nguo, plastiki, mume. Kwa kifupi chochote kile. Ukitaka uwe na furaha ya maisha kama unaweza mpe kuliko kumuazima.
Na wala wewe usiazime cha mtu chochote kile, kama huna kaa utulie utafute chako.

Huh?? Mume?? Nae aazimishwa.... Umenshangaza Twin... kwa misingi ipi?? aaise, the imagination yenyewe imenitia hasira.....
@Zinduna.... Pole Dear, twajifunza tokana na Makosa....
Da, AshaDii, ahsante mwaya, wajua vidani vyenyewe vya urithi ndo maana roho yaniuma mwenzio
Da Zinduna nina uhakika hapa watu wengi hawataelewa uliposema "leso" =Khanga lakini "ndweo" hata mimi umeniacha na kukaa kwangu kote Unguja miaka 3
Ile Avatar yako yenye uso wa upole maridhawa iwapi? Irejeshe kaka, wajua ilikuwa yatuvutia kweli.