Ukitaka kujua tabia ya rais wetu angalia tabia za wateule wake kama maDED, maRAS, maRC, maDC.

jpm anahitaji sana maombi maana hata yeye aelewi tunaenda wapi,kila siku matamko,matendo yake ni tofauti na maneno mikopo hakuna,dawa hakuna mahakama ya mafisadi hakuna jaani shida tupu
Nafikiri watu watachoka kuendelea kuomba kama hawaoni matunda ya maombi yao.
 
Kama ni kweli Gambo alipigiwa simu na JPM na kumwambia yupo pamoja nae baada ya kuvuruga hafla ya Uzinduzi wa ujenzi wa hospital ya wakina mama na watoto.

Basi kutakuwa na shida kubwa sana kwenye nafasi ya juu kabisa ya utawala wa Nchi hii.

Na kawaida ya watu type ya Gambo huwa hawaaribu mara moja. Atakuja kuharibu siku nyingine ndipo mamlaka ya uteuzi wake itakapoona ilivyo achwa utupu.
Mimi siamini kama kweli rais anaweza kupiga simu kwa mteule aliyefanya maovu lakini kama ni kweli alifanya hivyo basi ninaamini hatuna rais
 
Hatujui tunaelekea wapi, kila siku wateule wanafanya vituko vya ajabu. Mungu tusaidie
 
Nljua labda utakuwa umeandika cha maana kumbe ni upuuzi kabisa .........mahakamani hata mbowe kapelekwa kwani ajabu? kurudia shule sio ajabu acha ubwege ndugu....jenha hoja za maaana.....kama roho zinakuuma wenzio kuchaguliwa .......na wewe shika ukuta wa chadema upate kuchaguliwa....chei chei
 
sijui hivyo viwanda vitaendeshwa na wezi wa majina mitihani sijui kama tutaendelea .


swissme
 
Mimi siamini kama kweli rais anaweza kupiga simu kwa mteule aliyefanya maovu lakini kama ni kweli alifanya hivyo basi ninaamini hatuna rais
Ngoja nitafute clip yake, na kwa wasivyo na busara wanaropoka wenyewe ili kutafuta sifa.
 
HAWA NDIO VIONGOZI WANAONGOZA WATANZANIA WENYE PHD MADOCTOR PROFESSOR WENYE REALLY GOOD SCHOOL BILA KUUNGAUNGA SIJUI HIVYO VIWANDA VITAENDESHWAJE.

downloadfile-9.jpeg

downloadfile-10.jpeg

swissme
 
Namkumbuka sana kamanda mawazo.... nakumbuka ile picha amelala porini akiinua kichwa bila kuweza, roho inasema amka, mwili umeisha dhoofu kwa kipigo, nakumbuka hata haki ya kumuaga ilibidi mahakama pekee ndo iitoe la sivo do...... RIP kamanda....ahsante kwa kila ulilo fanya hapa duniani....
 
Hawa ndio wateule wa rais.

Katika hali inayoashiria ULEVI wa madaraka, Mkurugenzi wa Wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza amegiza wenyeviti 174 wa serikali za mitaa wanyanganywe mihuri. Sintofahamu hiyo imetokea katika mkutano ulioitishwa na mkuu wa wilaya hiyo kujadili maendeleo, ambapo mkurugenzi huyo aliropoka kwamba wenyeviti wote wanyanganywe mihuri, bila kujali kwamba mihuri ni vitendea kazi halali vya wenyeviti hao katika kuwahudumia wananchi wa maeneo yao.

Utata huo umezua maswali mengi na wengi wamebaki wanajiuliza: je, mkurugenzi anataka wenyeviti wanyanganywe mihuri apewe nani? Ndipo wenyeviti hao wakamkatalia katakata, huku wakitaka kumpiga na kupelekea mkutano kuvunjika.

Hii ndio aina ya wateule ambao nao wanataka kujigeuza miungu watu kama mteuzi wao alivyo. Hivi kweli jamani mkurugenzi mwenye akili zilizotimia anataka wenyeviti wanyanganywe mihuri ili iweje? Hebu tusaidiane kumshangaa mkurugenzi huyu.

CHANZO: ITV
 
Back
Top Bottom