Ukitaka kujua tabia ya ndugu subiri aoe

Ukitaka kujua tabia ya ndugu subiri aoe

Kuna mambo watu hawayatambui, kumsaidia mzazi, jamaa zako ni fadhila tu na wala si wajibu iko hivyo, wajibu wako uko kwa familia yako(wife and your children). Na wewe pia mtoto wako si wajibu wako kukusaidia wewe ila ni fadhila tu.
 
"Mtegemea cha nduguye hufa masikini" pigana na hali yako na wewe uwe mshua kama bro.

Sasa mtu ameoa ulitaka aoe wangapi? Siku nyingine tafuta cable ya aibu uiunganishe kichwani kabla hujatuma post za aina hii.
 
Hunyu,umeongea kweli kabisa.
Ambao hamjaoa hebu jaribuni kuwasoma na kuwajua vizuri tabia za wachumba na wazazi wa wachumba zenu.
Bahati mbaya vijana bado hatulitambui hili, mtu anakutana na demu mzuri anakurupuka tu bila hata kujua background yake vyema. Hakika masikitiko na malalamiko hayataisha
 
Ndugu achana na mawazo ya kimasikini, sasa ulitaka bro mshua akulee?.

Umasikini ni kitu kibaya sana, naona dalili za kuanza mchukia bro mshua kisa anapanga familia yake.
 
Kuna jamaa mmoja Mangi anaishi Dar mitaa ya Mikocheni namkubali sana,kwanza ni family man balaa.Ana kiwanda cha steel jamaa amejengea wadogo zake wote wa kike + wa kiume nyumba kawanunulia magari na mitaji ya biashara juu inshort amefanya ukoo wake unaonekana kama wa kitajiri hivi,kipindi flani mke wake alitaka kuleta mdomo jamaa akamwambia wadogo zako wangapi nimewapa maisha?

Msimamo wa jamaa ni kwamba yeye ametoka mbali na kaka/dada/wazazi zake na hakuna wa kumtenganisha na nduguze na hua anafurahisha anaposema anapotaka kusaidia ndg zake wala hahitaji kuomba ruhusa kwa mke wake.
 
Mkuu JIFUNZE KUJITEGEMEA

Lawana hazikusaidii wala hazikujengi
 
Back
Top Bottom