Ukitaka kujua Rushwa ni adui wa kila kitu tembelea Kenya

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,542
7,450
Habari zenu wadau

Leo nataka tujadili jambo hili la athari za rushwa katika jamii,
Mwl nyerere aliwahi kusema mara nyingi tu kuwa rushwa ni adui wa haki, rushwa ni kansa,
Maneno haya hutajua maana yake mpaka utapoishi kwenye Taifa lenye kutukuza rushwa

Tanzania ipo rushwa ipo kwa kiwango chake, lakini ukitaka kuona athari kubwa za rushwa basi fanya kutembelea jirani zetu pale Kenya,
Utashangaa awamu ya 3 na 4 kwetu zilisifika kwa rushwa lakini kwa kile kiwango naomba niwahakikishie ukifananisha na Kenya ya sasa bado rushwa kwetu ilikuwa ndogo sana,
Kenya rushwa sio siri, rushwa iko wazi kabisa, hakuna huduma yyte utapata bila kutanguliza rushwa nchi ya Kenya,
Rushwa imeathiri mfumo mzima wa maisha ya watu wote,
Yaani mwenye pesa Kenya ndio mwenye haki ya kila kitu, na hakuna taasisi inaongoza kwa rushwa Kenya kuzidi polisi,

Ndugu zangu tupige vita rushwa kwa nguvu zote rushwa ni adui wa haki na kansa mbaya
 
Juzijuzi tu nilikuwa natoka namanga kwenda sun city nilikuwa na clock 120kph hadi 140kph hakuna cha tochi wala askari juu ya mwembe halafu hawana visheria vya kingese ngese..rushwa zao ni ni kuanzia mabilioni ka ma zambia.
 
mtoa post rusha ipo kila sehem ila sio kama bongo, tanzania ndio nchi inaongoza kunyanyasa wageni kwa visa vya rushwa, madereva watalii nk kutoka nchi zingine huonewa sana bongo
 
Nadhani hujaishi Kenya labda unaingia na kutoka, rushwa imeathiri sana maisha ya watu wa chini zaidi ya hao matajiri
 
mtoa post rusha ipo kila sehem ila sio kama bongo, tanzania ndio nchi inaongoza kunyanyasa wageni kwa visa vya rushwa, madereva watalii nk kutoka nchi zingine huonewa sana bongo
Hata kwetu hapa nimesema rushwa ipo, ila kiwango cha rushwa Kenya ni hatari sana
 
Back
Top Bottom