Ukitaka kujua hii nchi bado iko kwenye lindi la umaskini angalia aina vyakula vinavyopikwa/kuuzwa mitaani!

Lavit

JF-Expert Member
May 16, 2011
13,344
27,746
Kwa hapa Dar es Salaam mtu kama hupiki kwako ukitegemea kula migahawani basi utateseka sana, huku mitaani kukuta mahali wanapika vyakula vya kueleweka basi utazunguka sana.

Wengi wanapika vyakula ilimradi na hii ni dsm ambalo tunaona ni jiji na pengine watu wake wanatarajiwa kuwa na kipato kizuri.

Mwanzo nilikuwa najiuliza sana shida ni nini, mwisho nikagundua watu wengi wana kipato duni na ndo wateja wao wakuu,wengi ambao huwa wanajaribu kuboresha biashara huwa wanaishia kufunga.Inafika mahali ukitaka kula chakula cha kueleweka basi inakubidi usafiri maili kadhaa!

NB; Kwa uzoefu wangu kuanzia ubungo mpaka mbezi mwisho, sehemu zenye chakula kizuri haziwez fika hata 5!
 
Hoja yako ni IPI hasa?

Kuhusu Tanzania kuwa nchi masikini hiyo inajulikana na umasikini mkubwa huchangiwa na UJINGA wa viongozi pamoja na wananchi.

Ila kuhusu chakula , Tanzania hamna umasikini wa chakula.

Kuhusu chakula unahitaji kula cha kula kizuri kwa bei ya 2000 ?

Ukienda katika mgahawa ambao chakula kinauzwa 10K lazima upate chakula kizuri.

Nchi ina umasikini wa AKILI na sio chakula.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom