Ukistaajabu ya Musa

Ukistaajabu ya Musa

Ngwananzengo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2012
Posts
1,911
Reaction score
1,320
Wahenga hawakukosea waliposema kua uyaone. Rafiki yangu mmoja ambae tupo wote katika shughuli za kusaka tonge, alikuwa na tabia yenye kutia ukakasi. Kwa umri ana miaka 30 na kidogo na bado hajaoa. Katika mahusiano amekuwa akitoka na wake za watu. Tabia hii kwa kiasi imenifanya niwe nikimsisitiza kwa nini wake za watu? Yeye amekuwa akijibu mosi amekuwa na bahati na wake za watu kwani kila akitupa ndoano mambo huenda sawia.Pili anatafuta uzoefu kwa nini wake za watu wanaasi kiapo chao. Mimi ni nani nimhukumu jamaa yangu huyu. Kama ni uovu imesemwa siku ya kiama "kila mmoja ataubeba msalaba wake."Katika utafutaji kuna "sometimes Yes , sometimes No". Mwaka jana jamaa alianza kupata matatizo. Kila pesa ikiingia matatizo ndiyo yanaongezeka. Mwisho wa siku akasema Hapana lazima kuna kitu. Akajifikiria aende kwake yeye yule jana leo na hata milele akapige magoti. Katika kutafuta ushauri akaamua aende kwa "fundi". Alipofika akaambiwa ni kweli ana Tatizo la pesa kutokutulia na akapewa "dawa" za kutibu. Sharti alilopewa ni marufuku kutembea na wake za watu. Kwa kuwa alikuwa na nia ya kuondokana na Tatizo lake aliamua kufyeka michepuko yake na kurudi kuwa mwongofu. Tatizo limeisha na kile anachokipata walau kinatulia. Ama kweli sayansi zingine ni ngumu kuzielewa. Na kumbe laana zipo za Aina nyingi. Waliosema na wanaoamini mke wa mtu Sumu hawakukosea. Tukumbushane ule msemo wa wahenga waliposema, "Cha mtu m.a.v.I" na "mwenye chake muungwana".
 
wake za watu wataendelea kugegedwa mpaka akili ziwakae sawa
 
Busara ya kawaida kabisa hyo. Haiwezekani mtu ushupalie wake za wenzio kila siku afu hujaoa kwamba anagalau na wenzio watakuja kurevenge kwako. Mungu kaamua kuwa fair .
 
Kwani yeye alishindwa kujiongeza, angewezaji kuwa vizuri kiuchumi wakati anawasaidia wanaume wenzake kutunza wake????? hapo hamna laana wal nini, ni akili ya kawaida kabisa ametumia mganga kumuweka sawa huyo mjinga, kuhonga si mchezo kama unavihela vya mboga lazima utabaki mweupe.
 
Kwani yeye alishindwa kujiongeza, angewezaji kuwa vizuri kiuchumi wakati anawasaidia wanaume wenzake kutunza wake????? hapo hamna laana wal nini, ni akili ya kawaida kabisa ametumia mganga kumuweka sawa huyo mjinga, kuhonga si mchezo kama unavihela vya mboga lazima utabaki mweupe.
Wengine wanaamini wake za watu ndio mteremko. Ataanzaje kukuambia kodi ya nyumba imeisha? Au ....
 
Wengine wanaamini wake za watu ndio mteremko. Ataanzaje kukuambia kodi ya nyumba imeisha? Au ....


Hakuna mke wa mtu anayegawa bure, wengi wanaotoka ni wale wanaokosa huduma muhimu ndio maana wanatoka, hivo kumgharamia kuko pale pale hakuna nafuu kwa mwanamke wa sasa.
 
Hajapewa dawa wala nini Mganga kacheza na Saikolojia yake tu akajua jamaa mtu wa kujirusha na kutumia. Kwa mfano kama un matumizi yafuatayo kwa vipato vya bongo jua utakua maskini. Haya tuanze;

1: Matumizi ya Bar # 50,000
2: Bajaj/Boda/Taxi # 20,00 (kwenda nakurudi)
3: Hotel ya faster room# 50,000
4: Wewe mwenyewe na washkaji na vocha # 50,000
3: Mengineyo kama mafuta ya gari yako, nakadhalika # 50,000

Kwa kadirio la chini kwa week kama itaenda vizuri utatumia sio chini ya laki mbili hadi mbili na nusu. Kwa mwezi ukigegeda mara mbili na mitoko hio hio unapata sio chini ya laki tano hadi sita.

Kazi nyingi na milioni kwa mwezi pamoja na dili za wizi unafikisha milioni mbili na kidogo. Ukitoa laki sita za matanuzi unabaki na kama milioni na nusu. Haya ipigie mahesabu ifike mwisho wa mwezi na unataka kujenga, kuwatumia nyumbani, kuwalipia ada wadogo zako. Hahahahaaaa halafu useme mganga kakupa dawa!

Badilisha tabia na mienendo yako tu. Hio salary hapo juu ukumbuke ni kadirio la juu.
 
Back
Top Bottom