1. Mitajenga hospitali kijijini kwetu na kufanya matibabu yawe bure au rahisi
2. Nitajenga shule ambazo kila mwanafunzi ataweza kuhudhuria
2. Nitaaanzisha miradi ya kutoa ajira kwa walionizunguka
Mantiki ni kuwa utajiri wangu hauna maana yeyote, kama ninaoishi nao ni maskini! Vitu ni vya msimu tu, inafika wakati vogue yako utaiona ya zamani na utaichoka, jumba lako la fahari utalala chumba kimoja tu, ila furaha ya kweli ni ile inayodumu nayo ni kusaidia binadamu wenzako.
- Kuna wakati nilifikiria nikipata music system maisha yangu yatakuwa mazuri. Nikaweza kununua. Nikaizoea nikaona ya kawaida.
- Nikasema nikinunua TV kubwa kabisa nitafurahi. Nikanunua, vipindi vyake vikaanza kuniboa.
- Nikasema nikinunua gari (used) nitakuwa nimemaliza. Baada ya muda nikaliona limepitwa na wakati.
- Nikaamua ninunue jipya kabisa, baada ya miaka mitatu nikalichoka
- Nikajenga nyumba nzuri ya kuishi....bado nataka kujenga zingine...ila
- ...nikasaidia watu wengi wakabadilishamaisha yao kuwa bora...NIMERIDHIKA NA MOYO WANGU U SAFI KABISA!