Dumelang
JF-Expert Member
- Aug 11, 2011
- 3,267
- 5,854
Hawa “Watoto” wanaoisumbua CCM na Serikali yake, CCM waliwaandaa wenyewe. Kama vile Mkoloni alivoandaa waafrika kwa nafasi duni za ukarani, mesenja nk akiamini wakiwa na elimu kubwa watamwangusha akawapa Elimu duni ya Masingi tu lakini ajabu haohao bado wakatumika kumtoa, “mkoloni hakuamini.”
historia ina tabia, inajirudia.
wakati huu miaka mingi baadae sio wakoloni toka ulaya ni wakoloni wa ndani walioandaa kundi la watu wenye akili duni kufikiri kwakuwapa elimu duni, elimu za shule za kata. Watu waliosoma shule zikiwa hoehae.
Shule ambazo zilianza kama mabanda ya kufugia kuku. Shule zilizokosa miundombinu ya Elimu na Elimu stahiki, Shule zisizokuwa na hata debate (midahalo)ya kusisimua ubongo kufikiri kwa hoja, zikaandaa watu ambao hawawezi shindana kwa hoja.
Leo zinawapa matokeo sawia na walicho kiandaa.
Jenga hoja watakujibu kwa tusi. Sio hoja kwa hoja. Hawa waliandaliwa na CCM yenyewe na Watu wake (viongozi) wenye kiburi kumliko Ibilisi.
Mwana falsafa mmoja aliandika “Insults are the weapons of those who have no argument.” Yani “ matusi ndio silaha ya wasio na hoja”. 🤔
CCM ni sikio la kufa iliambiwa miaka mingi Jengeni nchi ya watu werevu, Wakabeba fikira za Wakoloni wa kizungu.
Marehemu Lowassa akijua hilo alisisitiza nikiingia madarakani kipaumbele cha kwanza ni ELIMU cha pili ELIMU na cha tatu ni ELIMU, alijua vema aina ya elimu wanayowapa watoto wa Masikini, na yeye (LOWASA) akiwa Mmoja wa waasisi wa Elimu hiyo.
Leo miaka 20 baadae CCM na Serikali yake wanapambana na Matokeo ya walichopanda. CCM walidhani wakizalisha watu wenye elimu bora watawatoa madarakani, ni kweli wangewatoa Madarakani lakini watu walioelimika wangewatoeni kwa Hoja na Ushindani, maana akili ya mtu aliesoma na kuelimika vema upima matokeo hasi na Chanya ya kila hatua yake. Kwa maneno mengine msomi ana uoni wa mbali.
CCM na Serikali zake Wakaandaa elimu iliyozaoisha panya road wengi hawa wanakutoa Madarakani, ila wanakutoa madarakani hata kama hawana hoja.
Socrate, Mwanafalsafa; Aliandika
“Smart people learn from everything and everyone, average people from their experiences, stupid people already have all the answers.“
kwa tafsiri isiyo Rasmi
“ watu waerevu hujifunza kutoka katika kila kitu na kila mtu, watu wa kawaida ujifunza kupitia uzoefu wao binafsi, watu wajinga tayari wana majibu ya kila kitu”
Huo msemo wa Socrates unakupa picha gani? Vijana wengi wa Tanzania wapo katika eneo hilo la mwisho. Wana majibu ya kila kilichopo Tanzania, serikalini, kilichopita, kilichopo na wanachotarajia. Wangekuwa hata watu wa kawaida wangejifunza kwa uzoefu wa Jana🙂↕️
Leo, ya Jana hayajawafundisha, hawataki hata neno “Maridhiano”
Nimeandika mahala Hapa jamii forum “Maridhiano ni Tunu ya Utu na Ubinaadam”
CCM inakufa ila hatari yake ni wakati CCM inakufa inakufa pamoja na Nchi yetu tunayoipenda.
Lazima CCM waone sasa kuwa tunahtaji nchi hii zaidi kuliko uroho wao wa madaraka na utawala wa kikundi kidogo kinachokula mema ya nchi.
Wakubali kujirekebisha wawape nafasi watanzania wengine pia kutoa mchango katika maendelo ya nchi, walichofanya wamefanya hatubezi wameileta nchi ilipo, wakubali (kijasusi) kujenga vyama vikuu viwili imara vitakavyo ilea Tanzania ikiwapa vijana Smart nafasi huru kuweka mawazo chanya katika nchi.
Waruhusu nchi ijenge Taasisi Imara nje ya CCM. Isije kufa ikafa pamoja na nchi hii ambayo ni nyumbani kwetu, wajukuu na watoto wa wajukuu zetu. Hawa wajinga wengi mliotengeneza hawajui hili na hawahtaji kujua kwakuwa wao wana majibu ya kila kitu. Wataichoma nyumba yetu na kesho tutakuwa wapangaji. Kufeni peke yenu kama mmekuwa sikio la kufa.
Mwenyezi Mungu aibariki Tanzania