Fredinho
JF-Expert Member
- May 18, 2016
- 971
- 1,160
Kurwa na Doto ni wasichana mapacha wafananao sura ,umbile na sauti,hawafichani jambo,la kuvutia zaidi ni kuwa wote wanapenda vitu vya aina mmoja,tena hupenda kuvaa nguo za kufanana kila watokapo.Mizunguko yako kimaisha yakukutanisha na Kurwa kidume wewe warusha chambo,chambo yako yaunasa moyo wa Kurwa.Kwa furaha Kurwa anakutambulisha kwa Doto moyo wa Doto unapasuka paaah! hisia kali za mapenzi zachanua moyoni mwake anapata uthubutu,anakueleza mubashara kinachomsibu,utata ni kuwa huwezi kuwatofautisha kirahisi sura umbile na sauti vyote vyafanana,Kurwa anasema anavyokupenda ukimuacha anajiua,Doto anasema ukimkatalia anajiua,kila mmoja anadai siku akikuta na mwanamke mwingine anajiua daaaaaaaah! unafanyaje?