Ukiona unamchukia mkeo au mumeo fanya yafuatayo

kethika

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
630
472
Kwa wale waliooa au kuolewa wanalielewa hili. Kuna wakati mtu anaweza kumchukia tu mke wake au mume wake bila sababu ya msingi. Na hii iko dhahiri pale mtu akikosewa tu kidogo anakasirika sana. Kama ni mke hataki hata kumsogelea mumewe kadhalika mume.

Inafika mahali mpaka wahusika wanajiuliza kwanini niliolewa na huyu au kumuoa huyu. Mume anaweza hata kutamani laiti angekuwa ameoa dada wa kazi kuliko mkewe. N.k kwa wale waliooa.

Kuna wengine wanajiuluza kuwa kwanini mambo hayo yanawatokea na wangetamani watoke hapo. Kuna wengine hayo yanawatokea na wanaona ni hali ya kawaida imetokea na ni kweli wapenzi wao wamebadilika tabia au muonekano au walidanganyika walipokubali kuoa au kuolewa.

Ukweli ni kuwa kama ulikuwa umekubali kuolewa au kumuoa uliyemuoa ni kwasababu alikuwa mzuri na tabia iliyokufurahisha. Mabadiliko ya muonekano yapo ila yakifunikwa na upendo huwezi kuyaona kiviile in fact utampenda zaidi. Si mnajua kuwa yule mtoto mwenye changamoto huwa ndiye anayependwa na kujaliwa zaidi.

Swali ni kuwa nifanyeje kama simpendi niliyekuwa nampenda mwanzoni?

Pamoja na majibu mengine ambayo wadau watayatoa hapa naomba nikupe jibu moja huku niliendelea kutafuta ukweli wa jibu langu.

Ukiona hayo yanakuotokea fanya hivi:

Usiruhusu hisia za kimapenzi za mtu mwingine nje ya mke wako au mume wako kukuingia. Hisia za kimapenzi hapa ninamaanisha kuvutia na mtu wa kike au wa kiume kwa namna yoyote ambaye sio mkeo au mumeo. Usiruhusu mawazo yenye uhusiano na maswala ya kimapenzi kwa mtu mwingine nje ya mkeo au mumeo kujikita kwenye fahamu zako.

Najua huwezi kumzuia tai kutua kwenye kichwa chako ila unaweza kumzuia asijenge kiota kwenye fahamu zako.

Ukifanikiwa katika hili utakuja hapa na majibu.

Utashangaa jinsi ambavyo kwa kadri unavyofanikiwa kuzuia tai asijenge kiota kwenye kichwa chako ndivyo upendo na hisia za mapenzi zinavyorudi kwa mkeo au mumeo.
 
darasa zuri sana hili kwa wale wote tulio na michepuko
japokuwa mkuu si kazi ndogo kuzuia hisia za mapenzi na haswa ukiwa ushatekwa na shetanij jambo hilo ni gumu kama vile kujaribu kuzuia mvua
mapenzi ya michepuko yasikie hivyo hivyo yana nguvu ni kama ulevi wa unga kuacha tabu
 
sasa unaoa mke mambo yote yanakuendea kombo ile akiba uliyokuwa unaweka inapotea maisha yanakuwa magum shughuli haziendi hapo utafikilia kuendelea kumpenda hiyo mke??
 
Mi sijaona jibu solutions uliotoa,labda sijakuelewa.unasema ukiona hisia za kimapenzi kati yenu zimepungua "usiruhusu mawazo ya kimapenzi kwa mtu mwingine" hapa ndio pananikwaza,sababu kama tayari hamna hisia za kimapenzi (wanawake wakiwa hawana hisia za ki mapenzi na wewe balaa lake sio dogo),itakuwaje tena uwe na uwe uwezo wa kuvuta hisia kwake.
Ni sawa na kusema 'sikutamani lakini nitakutamani' haya mambo hayabadiliki gafla namana hii,wakati mwingine wote mnahitaji mda na jitihada nyingi tofauti ili mkae sawa tena.
Kutamani wengine au kutotamani ni masual mengi.mkiwa n ugomvi haina maana ,kutaka mwingine
 
Michepuko mingi siku hizi inatoa kipira, huo ndo ulevi wa vijana sa hv kuacha ni kama unga ngumu sana mpka uende rehab
 
sasa unaoa mke mambo yote yanakuendea kombo ile akiba uliyokuwa unaweka inapotea maisha yanakuwa magum shughuli haziendi hapo utafikilia kuendelea kumpenda hiyo mke??
Una uhakika kuwa yeye ndio chanzo? Katika upendo hakuna kulaumiana ila kuna kusaidiana
 
Back
Top Bottom