Ukiona mwanaume analia ujue kaguswa pabaya

Ukiona mwanaume analia ujue kaguswa pabaya

juakal

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2015
Posts
587
Reaction score
125
Wakuu nisiwachoshe, iko hivi:

Leo wakati nko na beiby wangu nayemwamini sana na nliekuwa na malengo ya kumfanya mke wangu, gafla simu yake ikaita kucheki jina ni Abdu ( kama yupo humu atakuwa shahidi), baby akapokea huyo abdu sijui alikuwa anaomba namba ya nani, sikufatilia zaidi.

Badae kidogo abdu akapiga tena, wakaongea kidogo,, sikufatilia. Baada ya muda akapiga tena, baby hakupokea, ndo Abdu akazidi kupiga kama missed call 7 hivi.
Ikabidi nimlazimishe baby apokee, akagoma nikamwambia mimi napokea, hapo ndo ukawa ugomvi sasa. Nikachukua simu kuchek call record nikakuta amejaa Abdu tangu siku za nyuma.

Abdu alivyozidi kupiga nikapokea, akauliza wewe ni nani? Nikamwambia mimi ni Flani na mwenye simu niko nae mbona unasumbua sana?
Akasema huyo ni demu wangu niko naye kama mwaka na nusu hadi mama yake ananifahamu, akanieleza kuwa hata jana walikuwa wote akamuomba nauli anaenda kumuona babu yake ( na kweli hiyo safari alikuwa nayo hata mimi aliniomba nauli nikamtumia).
Akazidi kusisitiza kuwa hata jana jioni alikuwa naye na aliona tunachat akawa amepotezea.

Baada ya hapo mtu mzima kijasho kikachuruzika mgongoni, na huyu baby akajitetea hivi:
Akasema huyu mtu alikuwa anamfatilia mda sana akamkataa sasa huwa anasumbua sana.
Akadai kuwa alikataa kunipa niongee naye kwa sababu alijua tu atamsingizia vitu ambavyo si vya kweli.

Ikabidi nimnyanganye baby simu ili niende nayo alaf nimrudishie j3 ila badae nikaamua kumrudishia.

Hadi sasa sijachukua uamuzi wowote, ila najua penye wengi hapakosi busara. Naombeni ushauri ndugu zangu maana ghafla kichwa changu kimekuwa kidogo sana,
 
Unataka kushauriwa nini wakati ukweli wote ushaufahamu labda kama unataka kujua maisha ya kuwa mume mwenza yakoje

Kwahiyo nipige chini? Mimi nafikiria nifatilie zaidi, ila ndo sioni nitumie njia ipi
 
huyo dem ni muongo jamaa bwana wake,kama sio bwana wake namba ya sim aliipataje?
 
Pole saana kwa huyo mtarajiwa wako kukuonyesha kila dalili ya kukusalit but usimwache....
Tafuta ushahidi wakutosha na kama ni kweli, kisha mueleze na umuonye mkuu...
hayo ni mambo madogo, usihamishe malengo yako nae
 
Pole sana mkuu juakal kwa yaliyokufika. Kuna msemo wa waswali unaosema "Nyota njema huonekana asubuhi" na "mwenye macho haambiwi tazama." Nina imani misemo hii itakusaidia ktk kufanya maamuzi ya busara.
 
Last edited by a moderator:
Ngumu saana, but ningetafuta ushahidi wa kutosha kabla ya kufanya maamuzi


Somehow itasaidia but utakua umejidhatiti kukabiliana na huo ushahidi maana mengine yanauma had ukajutia why umetafta ushahidi
 
Pole saana kwa huyo mtarajiwa wako kukuonyesha kila dalili ya kukusalit but usimwache....
Tafuta ushahidi wakutosha na kama ni kweli, kisha mueleze na umuonye mkuu...
hayo ni mambo madogo, usihamishe malengo yako nae

Asante sana mkuu. Nitalishughulikia hili, inaumiza sana kwakweli hasa ukiwa umeweka malengo
 
Somehow itasaidia but utakua umejidhatiti kukabiliana na huo ushahidi maana mengine yanauma had ukajutia why umetafta ushahidi

Yes kwavile ni mtu ambae kwa namna moja au nyingine nimekuwa nae kwa muda kabla sijafanya chochote lazima nifanye critical investiagation. Kama mtu ushafikia hatua ya kuweka malengo sio vema kumwacha kirahisi....
 
Back
Top Bottom