Ukiona Jaji mkuu anafanya press conference ujue hakuna muhimili wa mahakama, ushawekwa mfukoni na mtu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Kwa mara ya kwanza tangu mhimili wa mahakama uanzishwe duniani, leo Jaji Mkuu wa TZ kafanya Press Conference kujibu mijadala inayoendelea katika jamii. Mahakama imeacha kazi yake ya kusimamia sheria imeanza kujibizana na watu. Haijawahi kutokea popote duniani. Na sababu ni kwamba mahakama kwa "nature" yake haina jambo lolote la kuargue na umma. HALIPO.!

Mahakama kama mhimili wa dola unaojitegemea haubishani, haujawahi kubishana na hautakaa ubishane na umma kwa jambo lolote lile. Ndio maana hata mahakama ikituhumiwa huwezi kuona inafanya press conference kujibu. Duniani popote mahakama haijibizani na watu.

Katika kitabu Practitioner’s Guide to the Federal Circuit, kilichoandikwa na Melissa M.Devine anasema "Ukiona nchi yoyote ambayo mahakama imeanza kujibizana na umma (public), basi elewa kwamba nchi hiyo haina tena mhimili uitwao mahakama".

Kwa maelezo ya Mellisa inaonekana Tanzania tunakaribia kufikia stage hiyo (ya kukosa mhimili uitwao mahakama). So sad.!!

Malisa GJ
 
Hata mimi nilishangaa kidogo ila sio sana maana hata mkuu wa kule ujedani na yeye alifanya almost similar thing siku chache nyuma. Yaani politic tupu. Hawa wote ni wanachama watiifu wa chama twawala na probably wameshaona ombwe la akina PoleSlow
 
Kuna tatizo kubwa la vijana wa Chadema nadhani tokea wamekosa kiongozi. Sina shida na Patrobas ila nadhani Heche aliweza zaidi kuwasimamia vijana wenzake. Huu uropokaji uropokaji usio na lazima unaifanya taasisi nzima kuonekana kama kituko. Sasa baada ya facts kuhusu mkutano mkubwa wa taasis za mahakama kufanyika hapa nchini na jaji mkuu akiwa mwenyeji sasa huu ujinga wanauweka wapi?
 
Kawaida tu, tumeshaona CDF anafanya press conference kuwajibu wanasiasa wa upinzan na kuzungumzia masuala ya Kibiti kana kwamba Usalama wa raia ni jukumu lake na sio IGP. Kwa sasa kutaka kila mhimili ujipambanue ni sawa na kutegemea kuona ngano na alizeti kwenye andazi. Tuelewe tu kwamba mihimili 3 imejumlishwa na kuwa mmoja(andazi).
 
Mkuu Pascal Mayalla samahani kwa usumbufu..
Hivi huyu Jaji Mkuu ulieshangilia wakati ule kwa kusema sasa Tanzania imepata Jaji Mkuu ndie huyu??

Wapi umewahi kusikia Hakimu sembuse Jaji tena Jaji Mkuu akizungumzia aina ya wapelelezi wa kuchunguza kesi wawe wa namna fulani?! ( kesi ya Lissu lazima itachunguzwa na wapelelezi wa ndani kwasababu ndio wenye uwezo wa kukusanya ushahidi..!!)

Anachokitaka Jaji kwa kesi yoyote iliyo mbele yake ni kitu kimoja tu.. USHAHIDI MADHUBUTI, basi.

Lakini Jaji Mkuu wetu anataka mpaka na aina fulani ya wapelelezi wa kukusanya ushahidi.

Honestly kama Nchi tumepata HASARA kubwa kwa Mhimili wa Mahakama ambao kuna kila dalili sasa unawekwa mfukoni na watawala!

Aibu kubwa kwa Mahakama ya Tanzania.
 
Kawaida tu, tumeshaona CDF anafanya press conference kuwajibu wanasiasa wa upinzan na kuzungumzia masuala ya Kibiti kana kwamba Usalama wa raia ni jukumu lake na sio IGP. Kwa sasa kutaka kila mhimili ujipambanue ni sawa na kutegemea kuona ngano na alizeti kwenye andazi. Tuelewe tu kwamba mihimili 3 imejumlishwa na kuwa mmoja(andazi).
Safari hii tutaona vituko haswa kutoka CCM.
 
Mahakama inapojibizana na public mja kwa moja inajionsoa katika imani na some members wa public, hata kama iko sahihi. Mahakama inajibizana na watu wakati wa kesi tu, au kutoa ufafanuzi wa matukio yaliyotokea mahakamani.
 
Back
Top Bottom