Ukiona hii unakumbuka nini

Ukiona hii unakumbuka nini

Nimecheka sana leo! sikujua kama kuna wa long kiasi hiki ndani ya jf!! Hinzi enzi zingerudi nchi ingetengamaa sana
 
Alaf si unajua kutofautisha timu, lazima tim moja wavue mashati? nilikua mwembaba kiasi kwamba ikitokea timu yetu wanatakiwa kuvua shati inabidi nitoke au nihame timu dah.

Ukiwa na viatu unaambiwa uvue kwa sababu wenzako wote hawana viatu, inabidi mcheze pekupeku....

Na mwenye kimo kikubwa pia alikuwa anakataliwa. Kulikuwa na neno khs kukataza kuvaa viatu lkn limenitoka.
 
Mr & Mrs daudi namkumbuka mwalimu wangu Mwaisenya pale shule ya Msingi Wailes temeke, alikuwa na usemi wake "mi nafundisha we unachezesha vijiti,nikikuita hapa mbele uje usome alphabet unaanza kujamba puuh puum,puuh puum,wanafunzi wote mbavu hawana...
 
Sie tulisoma vya mkoloni "mudhungu" Namkumbuka mwalimu wangu wa hesabu akivaa kaptura na kalamu akiichomeka kwenye stockings. Mpira tulicheza wa ngozi, ukishajaza upepo ile bladder unaifungia ndani ya gozi kwa kufungia Kamba za viatu.

Hawa walimu sikuwakuta, lkn huu mpira niliucheza. Ukiloa, kasheshe; ulikuwa unaongezeka uzito. Kilimi cha bladder kikijitokeza, mchezo unasimama kwa muda ili kirudishwe ndani.
 
Hawa walimu sikuwakuta, lkn huu mpira niliucheza. Ukiloa, kasheshe; ulikuwa unaongezeka uzito. Kilimi cha bladder kikijitokeza, mchezo unasimama kwa muda ili kirudishwe ndani.

Nyie mnabahati mpira wenu ilikua inajazwa upepo, wa kwetu ni mifuko ya rambo inafungwa kwa ustadi tu lakini ndimu ilikua inakamuliwa balaa.

Nimecheka sana leo! sikujua kama kuna wa long kiasi hiki ndani ya jf!! Hinzi enzi zingerudi nchi ingetengamaa sana

Kwa kweli hii ni burudani

Ukiona hicho kitabu na hako ka mpira unakumbuka enzi zipi?? Nini kilikua cha maana sana kwako wakati huo???

Yaani kwa kweli Kitabu cha Mr and Mrs Daudi kinanikumbusha viboko nilivyochapwa na baba enzi za uhai wake akiwa mwalimu wa kiingereza.

Shule niliyokuwa nasoma ilikua ni kijijini sana kiasi kwamba suala la uniform au sare ya shule sio ishu wewe ilimradi uje na kaptula tu na juu kama utapiga tshirt, flana shati ni uwezo wako tu. Mwenye kandambili yaani hizo akirudi nyumbani anaziosha anaziweka hadi kesho shule au zitavaliwa kwenye mtoko maalum.

Enzi hizo watu wakivuna mahindi, tulikua tunapita kuokoteza baada ya wenye shamba kuvuna kisha tunaenda kuuza.
Nikawa nimepata vijisent vyangu nikaenda mnadani nikanunua pensi, shati na mkanda. Kwa bahati mimi nilikua na sare za shule (baba alikua mwal. mkuu). Ila siku hiyo si unajua nilitaka nikawaonyeshee wenzangu pamba zangu mpya? Nikaulamba pekupeku nguo zangu mpya.

Huku nikiwa nimechelewa darasani, nilikuta baba (mwalimu wa kiingereza) anafundisha, aliponiona tu na mavazi yangu na nimechelewa, alinishushia kipigo cha mbwa mwizi, kisha akaniambia nisome aya kwenye kitabu cha Mr and Mrs Daudi. Kwa kuwa nilikua na hasira huku bado nalia na nnatakiwa kusoma kwa sauti ili darasa lote wasikie nilikua najikuta naanza kulia tena na kila nikilia naongezewa dozi ya viboko.

Umenifurahisha sana mkuu.
 
Nyie mnabahati mpira wenu ilikua inajazwa upepo, wa kwetu ni mifuko ya rambo inafungwa kwa ustadi tu lakini ndimu ilikua inakamuliwa balaa.

Sisi tulichezea yote. Huo wa bladder wkt mwingine ulikuwa unapata pancha, basi tulikuwa hatuna jinsi; ilibidi tuchezee ya mifuko iliyoshonwa na nyuzi za manilla. kulikuwa na jamaa walikuwa ni hodari sana wa kufunga -- tulikuwa tunaita kushona. Sisi tulikuwa tunatumia mifuko ya mbolea, ya Rambo ilikuwa haijaanza kuingia.
 
Back
Top Bottom