mzee wa kijiwe
JF-Expert Member
- Jun 25, 2012
- 947
- 685
Sio kawaida kwa rais wetu kukaa kimya namna hiI! Mzee wetu huwa hakubali kulala na donge lazima atapike na watu wajue msimamo wake.
Katika hili nimeshangaa Kumwona Rais wetu akikaa kimya bila hata kuitetea serikali yake, na kwa hulka ya awamu hii ya tano Rais ndiye mtetezi mkuu wa serikali wengine husema baada ya yeye kusema, wanaogopa wakisema kabla watakosea na watatumbuliwa, labda ni kwa sababu hatabiriki.
Serikali imepigwa madonge makubwa kuliko wakati mwingine wowote, watu wamejilipua, uoga wameweka pembeni wanasema kwa vinywa vipana bila kupepesa macho, nafikiri kuanzia serikali hii iingie madarakani hii ni Mara ya kwanza!
Je, Rais amemsikiliza Gwajima?? Labda ningekuwa na namba ya simu ningemtumia kwenye WhatsApp.
Je, Rais amewasikiliza majaji wa mahakama ya juu nchini wale watatu kule Arusha? Ameonyeshwa jibu la usoni, asipolitumbua tuseme nini?
Je, Rais amemsikia Nyerere mchekeshaji? Mbona kimya?
Je, Rais anaanza kuchoka? Je kutumbua majibu ndio basi?
Angalia vizuri majipu yatakuumbua Rais wangu! Hii kazi uliiomba mwenyewe japo kikatiba sii kazi yako kln ulisema wewe utakuwa mtumbua majipu sasa wengine wanakuonyesha majipu yalipo, utafikiri wamekuajiri, usichoke mapema tumbua, tumbua baba!!