Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Jamani hii haikai sawa hasa kwa huyu mjamaa (EL) ambaye anadaiwa kuutaka urais kwa udi na uvumba, na anayeripotiwa yuko katika mkakakti kabambe wa kupanga safu yake katika chama chake kujihakikishia uteuzi wa kugombea kwenda Ikulu mwaka 2015.
Rushwa katika chaguzi zinazoendelea katika CCM si suala la siri tena -- liko nje nje kabisa. Takriban vyombo vyote vya habari hususan magazeti vimekuwa vikiripoti rushwa ikitembea katika chaguzui hizo, tena mara nyingine waziwazi.
Isitoshe hata mwenyekiti wa chama hicho (JK) amelizungumzia suala hilo kwa masikitiko makubwa.
Lakini kwa nini huyu mgombea mtarajiwa (EL) hata siku moja hatujamsikia akizungumzia rushwa kama ni kitu kinachomkera? kulikoni?
Naomba majibu jamani, na msianze kuzungusha zungusha (spinning) katika swali hili ambalo ni simpo kabisa,
Nawasilisha.