Ukimya wa Lowassa kuzungumzia rushwa katika chaguzi za CCM -- kulikoni?

Hawezi kwa sababu inamsaidia sana kisiasa

Yaani harakati zake zote kumbe -- huwezeshwa na rushwa?

Nilidhani yeye anaweza kuuzika bila pesa! Halafu hiyo kampeni yake itafanyikaje?
 
Halafu nina hakika as the next sunrise kwamba akiteuliwa kugombea 2015, katika kampeni naye atafuata nyayo za huyo mwenzake - JK -- kukataa mdahalo wa kujieleza akiwa na wagombea wa vyama vingine. Ataogopa kuibuliwa masuala ya ufisadi.
 
Hivi hakuna katika wapambe wake wa kumwambia kwamba "kule saiti wanasema unapaswa kuonyesha kwamba nawe unakerwa na rushwa katika chaguzi za chama na ulizungumzie suala hilo, kama vile alivyofanya Sumaye na swahiba wako JK."
 
Tatizo la wana JF wengi ni kuandika mambo mengi kwa kuongozwa na hisia, chuki binafsi na unafiki badala ya kufanya utafiti na kuwa na ushahidi hasa linapokuja suala linalomhusu Lowassa. Hivi kama mna ushahidi na tuhuma za Lowassa kuwa ni fisadi na mtoa rushwa mkubwa je ni kipi hasa kilichosababisha msiupeleke huo ushahidi wenu mahakamani?. Je hakuna vyombo vya kupambana na rushwa na ufisadi nchini vya kumkamata na kumhoji?. Kama hayo yote hayawezekani basi Lowassa ni "mtakatifu" na anastahili kuingia ikulu 2015. No research no right to speak.
 
rushwa ni adui wa haki kila sehemu ipo na ndiyo maana ikawekewa sheria, lowassa unataka aseme kama nani wakati hayupo serikalini.

watanzania lowasa akiingia madarakani hela yake yote mtailipa aliotumia kuwapa misaada na michango yake kwenye harambee. Hakuna hata siku moja akiwa jukwaani akazungumzia rushwa .
Iko siku mtaikumbuka hii statement .
 
JK kaongelea rushwa tena kwa kulalamika wakati ana machinery za kuitokomeza na hafanyi hivyo

Lowassa hana mdomo mwingi yeye ni mtendaji na angelikuwa LOWASSA ndiye Rais ungekuta leo nusu ya UVCCM wapo selo manake lazima TAKUKURU wangefanya kazi

Lowassa anaogopwa na watendaji na hii ni sifa kubwa inamfanya awe mgobea bora ndani ya ccm

viva LOWASSA, hata MALAWI wasingeleta ujinga mbele ya Lowassa
 
Chezea lowassa wewe, kwanza yeye haamini katika rushwa(huyu mzee yeye hupenyeza rupia kwenye uzia,ulizeni vizuri watu wanaomfahamu vizuri kule monduli)
 
shime shime EL, huna sababu ya kusema chochote juu ya hilo linalozungumzwa la rushwa. Mungu amekujalia busara ya kukaa kimya ktk hoja za kijinga zinazoletwa mbele yako. mwl Nyerere aliwahi kutuhumiwa kuwa amejilimbikizia fedha kwenye mabank ya ulaya yy pamoja na kawawa na jamal, jibu lake alisema yeye huwa ajibu hoja za kipumbavu lkin kwa kuwa swala hili wamehusishwa jamal na Rashid basi ataliongelea kwa ajili yao. ndipo alipotumia neno kuwatuhumu hao basi neno UAMINIFU litakuwa halina maana.EL kuna viongozi wengi walioliongelea hilo la Rushwa ktk chaguzi utadhani kuwa ndiyo tatizo pekee la rushwa ktk nchi hii, tuna mengi saana mpeni nchi yote anayajua mfaidi matunda ya nchi hii.
 
Tatizo la wana JF wengi ni kuandika mambo mengi kwa kuongozwa na hisia, chuki binafsi na unafiki badala ya kufanya utafiti na kuwa na ushahidi hasa linapokuja suala linalomhusu Lowassa. Hivi kama mna ushahidi na tuhuma za Lowassa kuwa ni fisadi na mtoa rushwa mkubwa je ni kipi hasa kilichosababisha msiupeleke huo ushahidi wenu mahakamani?. Je hakuna vyombo vya kupambana na rushwa na ufisadi nchini vya kumkamata na kumhoji?. Kama hayo yote hayawezekani basi Lowassa ni "mtakatifu" na anastahili kuingia ikulu 2015. No research no right to speak.

Duh! Tayari umesha enda nje ya mada! Mtoa mada anasema kwa nini EL hazungumzii rushwa katika chaguzi hizi za CCM? haonekani kukrwa?
 
watanzania lowasa akiingia madarakani hela yake yote mtailipa aliotumia kuwapa misaada na michango yake kwenye harambee. Hakuna hata siku moja akiwa jukwaani akazungumzia rushwa .
Iko siku mtaikumbuka hii statement .

SITTA anazungumza rushwa kuwa ni ile ya Richmond tu kisa kunyimwa uwaziri mkuu

JK ana zana za kupambana na rushwa ila hazitumii

MEMBE anasaini mikataba bila kuisoma

LOWASSA ukimzingua unafukuzwa kazi on the spot....huyu anafaa kuwa rais
 
Jamani hii haikai sawa hasa kwa huyu mjamaa (EL) ambaye anadaiwa kuutaka urais kwa udi na uvumba, na anayeripotiwa yuko katika mkakakti kabambe wa kupanga safu yake katika chama chake kujihakikishia uteuzi wa kugombea kwenda Ikulu mwaka 2015.

Rushwa katika chaguzi zinazoendelea katika CCM si suala la siri tena -- liko nje nje kabisa. Takriban vyombo vyote vya habari hususan magazeti vimekuwa vikiripoti rushwa ikitembea katika chaguzui hizo, tena mara nyingine waziwazi.

Isitoshe hata mwenyekiti wa chama hicho (JK) amelizungumzia suala hilo kwa masikitiko makubwa.

Lakini kwa nini huyu mgombea mtarajiwa (EL) hata siku moja hatujamsikia akizungumzia rushwa kama ni kitu kinachomkera? kulikoni?

Naomba majibu jamani, na msianze kuzungusha zungusha (spinning) katika swali hili ambalo ni simpo kabisa,

Nawasilisha.

Kwa kawaida kinyozi hawezi kukosoa mtindo wa kunyoa alioubuni yeye mwenyewe, hukaa akiwa ametega sikio kusikiliza watu wanasemaje kuhusu mtindo huo mpya.
 
Lowassa ni mtoa rushwa, mla rushwa... hafai, na hasafishiki hata kwa dodoki
 
Tatizo la wana JF wengi ni kuandika mambo mengi kwa kuongozwa na hisia, chuki binafsi na unafiki badala ya kufanya utafiti na kuwa na ushahidi hasa linapokuja suala linalomhusu Lowassa. Hivi kama mna ushahidi na tuhuma za Lowassa kuwa ni fisadi na mtoa rushwa mkubwa je ni kipi hasa kilichosababisha msiupeleke huo ushahidi wenu mahakamani?. Je hakuna vyombo vya kupambana na rushwa na ufisadi nchini vya kumkamata na kumhoji?. Kama hayo yote hayawezekani basi Lowassa ni "mtakatifu" na anastahili kuingia ikulu 2015. No research no right to speak.
Anaiona Rushwa kama ni tatizo nchi hii? Mbona anazungumzia AJIRA kwa vijana, anazungumzia mpaka wa Malawi na Tanzania, kwa nini hasemi kitu juu ya rushwa ambayo anatajwa kuwa na kambi kuubwa kila kona nchi hii!
 
Alipo zungumzia kuhusu jeshi lipo makini na lipo tayari kulinda mipaka...mka mzonga, sasa hivi anaona awacheni mzungumze ninyi maana ninyi sindio mnajua zaidi, hata sokomoko la ponda na janja widi wa huko zanzibar huja msikia akisema,
hii ni ishara tosha kua anaajenda ndefu na kumshinda ni ngumu sana, labda afe kwa kuugua au ajali
wait,
 
Itaweza kuwapa rushwa hao hao wasiojitambua. Ila sidhani kama anaweza kutoa rushwa kwa Watz wote zaidi ya M40.
 
Tatizo la wana JF wengi ni kuandika mambo mengi kwa kuongozwa na hisia, chuki binafsi na unafiki badala ya kufanya utafiti na kuwa na ushahidi hasa linapokuja suala linalomhusu Lowassa. Hivi kama mna ushahidi na tuhuma za Lowassa kuwa ni fisadi na mtoa rushwa mkubwa je ni kipi hasa kilichosababisha msiupeleke huo ushahidi wenu mahakamani?. Je hakuna vyombo vya kupambana na rushwa na ufisadi nchini vya kumkamata na kumhoji?. Kama hayo yote hayawezekani basi Lowassa ni "mtakatifu" na anastahili kuingia ikulu 2015. No research no right to speak.
kweli wewe ni kilaza,yaani lowassa apelekwe mahakamani kwa serikali hii ya jk?
Hata mtoto mdogo anajua! Hivi unajua uchaguzi wa kumpata mgombea wa arumeru mashariki kupitia ccm? Nakwambia hakuna mgombea ndani ya ccm wa kupenda kutumia short cut ka lowassa! Huyu urais haumfai hata kidogo!
 
Back
Top Bottom