Ukimya ni maandamano

Ukimya ni maandamano

NEWSINKP

Member
Joined
Sep 26, 2016
Posts
77
Reaction score
94
Wasalaam.

Watanzania wenzangu tumechagua viongozi/ kuchaguliwa viongozi bado sisi ndio tunaowafundisha namna ya kutuongoza. Hili ni kosa kubwa mno na ndio maana haya ya tozo, kukamatwa watu huko mwanza n.k yanatokea. Kama ni mtu mwerevu umeshaelewa namna na sifa za watu tulio nao kwenye madaraka mbalimbali.

Je, umeshawahi kujiuliza hivi hii nchi itaelekea wapi kama wananchi wote tukikaa kimya na kuwaangalia tuu wafanye wanayoona ni sawa?

Imagine
  • Mbowe awe kimya,
  • Kidogo awe kimya,
  • Mwamakula awe kimya,
  • Malisa awe kimya,
  • Yerico awe kimya
  • Lema awe kimya
  • Heche awe kimya
  • Msigwa awe kimya
  • Sugu awe kimya
  • Twaha awe kimya
  • Sarungi awe kimya
  • Fatma awe kimya
  • ZZK awe kimya
  • Assad awe kimya
  • Warioba awe kimya
  • Lwaitama awe kimya
  • Ulimwengu awe kimya
  • Prof Shivji awe kimya
  • Mdude awe kimya
  • Bagonza awe kimya

Members wa jamii forum wasijadili suala lolote la kisiasa. Pamoja na asasi zote za kiraia na kidini. Ni nakuhakikishia hakuna mtu ataweza kuongoza hili taifa hapo niliowataja hapo watatafutwa Kwa nguvu waongee either kwa uteuzi.

Nimefuatilia sana nikagundua viongozi wote wanaoingia madarakani hua wanayafanyia kazi mengi ya yale yaliyokua yanapigiwa kelele na walio nje ya uongozi. Fuatilia mtanzania mwenzangu utaniambia, we jiulize kama sio hilo vuguvugu la katiba Leo wale polisi wangemkamata nani.
 
Mbeya miaka Fulani walikuwa wanamwita sugu Rais,na yalitokea maandamano makubwa ambayo ililazimika Sugu aombwe bungeni kwenda mbeya kuwasikiliza. Lugha aliyotumia ninyepesi sana watu wakarudi kwenye shughuli zao.

Watanzania ni wavumilivu. Ila wana ukimya wenye madhara ukiendekeza wawe wakimya kwenye haki yao ya msingi.
 
Back
Top Bottom