Nawashukuru sana jamani mmenitia moyo hadi machozi yamenitoka. Mungu ananipigania ila naanza kukata tamaa, niliupata 2008 na sijaanza kutumia dawa; bado Mungu ananiongoza.
Tatizo maisha yamekuwa magumu sana kwa sasa kiasi hadi nashindwa kula, yote ni woga wa kuwashirikisha marafiki na familia ila naamin Mungu atajibu maombi yangu
pole sana mpendwa wangu.
Kimsingi HIV imegusa karibu kila familia hapa tanzania. hivyo naomba nikutie moyo kwamba usiogope wala usisononeke kwaajili ya hili mpendwa wangu.
kama ni toka mwaka 2008 uligundulika na bado hujaanza kuumia dawa nina weka assumption kwamba bado CD4 zilikuwa juu, na hata viral load haikuwa kubwa.
nakuomba kama utathubutu naomba unipm CD4 level yako kwa sasa, na nakuomba sana kama unaweza hata viral load status pia pima uniambie. kisha nitakuomba uwe na ujasiri nikuweke kwenye utaratibu wa dawa ila hizi ni za majaribio so nitakuombea uingie kwenye huo utaratibu na tutakuwa tunakumonitor. Dawa hizi za majaribio sio ARV's lakini zimeonyesha kufanya vyema zaid kwenye kupunguza viral load, kuongeza cd4 na hazina contraindications kama zilivyo arv's
Tupo pamoja rafiki.Kibarua hauna? AshaDii pls, kama unaweza fanya kama ya yule kijana ili tumsaidie mtaji ili aweze kujikwamua
Nina amini mashosti na mabro kama FP snowhite, Smile, Mentor, KIKUNGU, gfsonwin, Riwa, mwaJ, cacico, MwanajamiiOne, King'asti na wengine wengi wanaweza kusaidia mdada akaweza simama kwa miguu yake.
sasa hapo cha kufanya wewe tumia hii mitandao ya kijamiii kujiuza piga picha za kutamanisha kisha aanza kusanbaza hapo itakua fresh mpaka dawa ipatikane 2015 utaishi nao fureshi
Nawashukuru sana jamani mmenitia moyo hadi machozi yamenitoka. Mungu ananipigania ila naanza kukata tamaa, niliupata 2008 na sijaanza kutumia dawa; bado Mungu ananiongoza.
Tatizo maisha yamekuwa magumu sana kwa sasa kiasi hadi nashindwa kula, yote ni woga wa kuwashirikisha marafiki na familia ila naamin Mungu atajibu maombi yangu
Nimemaliza ba ya sociology and social work nashukuru kwa ushauri wenu coz watu wengi ni fake umu ndani kuna kipindi nilitafuta mwenza mwenye vvu watu tulikuwa tunawailiana siku moja shida yao wanione then basi kumbe hawana ugonjwa
Siwezi kuwa tapeli maana sijaomba hela ya mtu.
Nimeongea hivi ili nishauriwe sababu sijawahi mshirikisha mtu, najua hapa sijulikani ndo maana nikaongea hivi wala sihitaji mia ya mtu, napenda kushauriwa tu
asante nimekuelewa izo dawa umesema ni za majaribio na utaratibu wake wa kunywa ni ule wa kila siku au inakuwaje nieleweshe kwanza