Ukimfumania Mumeo na Kondomu Mpongeze' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukimfumania Mumeo na Kondomu Mpongeze'

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Apr 20, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Mkufunzi mmoja ambaye ni nguli wa kuwafunda akina dada wakati wa Kitchen Party amewataka akina dada ambao wanakwenda kuolewa kufahamu vizuri jinsi ya kuutumia mwiko wa kupikia kwenye chungu ili kuzidumisha ndoa zao na pia wasiwe na ghadhabu wanapokuta kondomu kwenye mifuko ya suruali ya waume zao. Nguli huyo maarufu jijini Dar es Salaa kwa masuala ya Kitchen Party [Jina Kapuni] alikuwa akitoa mafunzo katika sherehe mojawapo iliyofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, hivi karibuni.

  "Katika ndoa kuna mengi yanayojitokeza mbali na kufanya kazi za nyumbani, unaweza kukuta katika suruali ya mume wako ndani ya mfuko amesahau Kondomu ukiona hivyo mpongeze mume wako maana anakujali pia usichukie wewe iweke vizuri na ikiwezekana pindi anaposafiri nenda dukani kamwongezee boksi nyingine ,mfungie kwenye begi lake", alisema kungwi huyo.

  Kungwi huyo alimwambia pia bibi harusi kuwa ukiona mwanamke mwenzako jirani yako amekuja kwako kukwambia kwamba mume wako ana uhusiano na mwanamke mwingine basi mchukulie mwanamke huyo kuwa anataka kuharibu ndoa yako.

  Mambo yako ya ndani usimwambie mtu mwingine zaidi ya mume wako maana ukisema mume wako anakojoa kitandani atakayechekwa ni wewe mwenyewe", alimalizia kusema mama huyo.

  Alisema pia kuwa wengi wa wasichana wanapoolewa huwa hawajui maana ya huu mwiko ambao alikuwa ameushikilia akimwelezea bibi harusi mtarajiwa jina tunalihifadhi.

  Alisema utakuta akina mama watu wazima ambao tayari wameolewa wanakuwa wanachanganya mwiko katika vyungu mbalimbali jambo ambalo halitakiwi mwiko unatakiwa kuingia katika chungu kimoja tu ni cha mme wako ambaye amekuoa na si vinginevyo.

  "Mwiko ukitumika katika vyungu vingi hupoteza ladha" alisema nguli huyo.

  Alifafanua kuwa wengi wa akina mama walioolewa wamekuwa wakithubutu kwenda nje ya ndoa zoa na hivyo miili yao kuingiliwa na miiko zaidi ya mmoja ambapo hasara yake ni kuambukizwa magonjwa.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4344750&&Cat=1
   
 2. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  "Mwiko ukitumika katika vyungu vingi hupoteza ladha"

  anayefundwa sasa hapa ni nani?mwanamke au mwanaume?

  BTT:nikikute na condom afu nikupongeze????thubutuuuuu... :rolleyez:
   
 3. RR

  RR JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Yes, nipongeze halafu uniongezee boksi zima.
   
 4. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #4
  Apr 21, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Duuuuuuuuuuuuuuu.
   
 5. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Saaaaaaafiiii!!!! Good knowledge on war against HIV/AIDS
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  kuna point zingine nimezikubali ..ila hilo la Condoms hapana
   
 7. Mhache

  Mhache JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2010
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kuongea hapa ni rahisi, lakini kutrenda ni ngumu sana. fikiria kama ni wewe umekuta kndomu moja mfukoni mwa suruali ya mumeo kwenye kiboks chake, wakati unajua katika boksi hukaa kondomu tatu, utajisikiaje? Uatakua na moyo wa kumuongezea nyingine? Ni vigumu kumuongezea kondomu. Inaonyesha mke hamridhishi mmewe, au mume hawezi kuvumilia.
   
 8. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Full of contradictions and double standard... huyu kungwi hafai kumpa mtu advice...
  anamwambia am support mme wake kwenda nje halafu anamkataza yeye ku cheat...

  Naona hapo mwanamke amedhalilishwa...
   
 9. ngonzi zomukama

  ngonzi zomukama Senior Member

  #9
  Apr 21, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhh!! itakuwa ngumu iseee!!! nimkute na Condom nimpongeze duh!!
   
 10. T

  Tall JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  umpongeze ili aendeleze ufuska? Na siku ikipasuka au a missuse? Naona baada ya kumpongeza,tembelea maeneo ya muhimbili kafanye windowshopping ya jeneza lako.
   
 11. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Hata mimi naona kama imegeuzwa vile!
   
 12. Sydney

  Sydney Senior Member

  #12
  Apr 22, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi na wivu woote huu nilionao, kumpongeza hata siwezi jamani, kutakuwa hakulaliki humo ndani! Kwakweli atanieleza alikozitoa na alizitumia na nani!
   
 13. m

  masho Member

  #13
  Apr 24, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  haaaa huyo kungwi kweli akili yake inamtosha mwenyewe, yaani ata kushauri ajui, yaani nimkute na koncom moja then nikanunue box nimwongezee it means akazini kwa amani sio, hiyo nguvu sitokuwa nayo
   
Loading...