Ukimfahamu Makonda hutaacha kumpenda, hata wapinzani wake mkimpata mtampenda sana

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,318
Huyu Ndugu Makonda. Ni vile wengi hawamfaham. Kama akiwa rafiki yako, akiwa chini yako hutaacha kumpenda. Ni mtu ambaye unapompa maelekezo anasikiliza. Anafanya kwa namna ambayo unataka iwe.

Bwana makonda ni mtu ambaye kama amelala ukamwamsha kuwa tukachote maji ndoo mbili mbili atakuuliza kwa nini tusichote nne? Au ukichota mbili ukapumzika yeye ataendelea kuchota zaidi. Kwa nini usimpende. Ni aina ya mtu ambaye when you tell him. Jump! He will ask "how high? Kwa unyenyekevu kabisa. Ukimwambia akimbie mita 100 atakimbia 1000.

Ungemuuliza Marehem Sitah angekwambia. Ungemuuliza Riziwan angekwambia kuwa This man ni mtiifu sana. Ni msikivu unapompa maelekezo hufuata bila kusita, bila kuuliza uliza. Ni kwa nini usimpende?

Akiwa rafiki yako. Ikatokea ukamfahamisha kwa baba yako. Atamheshimu baba yako, atampenda na kumjali.wakat wewe hupigi simu mpaka uwe na shida. Yeye atapiga simu na kumuuliza " mzee habari za asubuh?umeaamkaje hajambo na mama? Haya mi nlikuwa nawasilimia tu. Mungu awabariki" kwa nini mzee wako asimpende? Asitaman awe mtoto wake?

Jamaa anachapa kazi. Akipewa kazi anafanya hasa. Ni aina ya watu ambao husemwa "amesifiwa kukimbia kapitiliza hadi kwao" anafanya kazi kwa kujituma sana.

Alipoambiwa adui mkubwa wa CCM ni Ed Lowasa alipambana na Lowasa mchana na usiku. Alimtukana na kumkebehi.aliambiwa yeye adeal na lowasa akafanya kaz kwa mapenz makubwa sana wakamwona anafaa.

Akaambiwa sasa ahamishie nguvu zote kwenye katiba mpya. Aipinge mchana na usiku. Alifanikiwa sana na tunajua nini kilitokea kwa mzee warioba kwenye mkutano wake wa mwisho pale udsm.

Sasa mtu wa hivi kwa nini asipendwe?kwa nini asiaminiwe?ni mwaminifu na mtiifu. Haulizi maswali. Anasema hewala baba ntafanya. Vijana wengine wanahoji. Wanasema hili haliwezekani. Wakati yeye haamini kama kuna jambo ataambiwa haliwezekani.kwa nini asipendwe?

Kila chama ili kisimame kinahitaji akina yeye. Hawa ni watu wa muhimu sana katika ujenz wa chama na hata serikalini. Hutumika na watawala sehemu yoyote il duniani wanakuwepo. Hawa hutenda kwa uaminifu yale watawala wanayotaka yatokee.ni waaminifu sana. Adolf hitler alikuwa nao, idd amini alikuwa nao, bokassa alikuwa nao, djamen alikuwa nao, nyerere alikuwa nao, mandela alikuwa nao. Kila kiongozi anakuwa nao. Ni watu muhimu sana kushikilia itikadi.

Ni vile hamjamfaham makonda mkimfaham hata ninyi mtampenda. Mtatamani kumsajili awe kwenu. Trust me kama ingekuwa kunafanyika usajili basi angekuwa anagombaniwa kwa dau kubwa sana.
 
Kama ni MSIKIVU...anakwenda mita 1000 badala ya mita 100, ALETE VYETI vyake vya Fomu Foo..
Hahaha hio single ya vyeti Inaelekea mwishoni Kwa hiyo tafuteni kitu kingine cha kudai... Hahaha mlikuwa mnafurahisha Sana kipindi mnadai Cheti kila siku Cheti Cheti.. Sasa hivi Kimyaa.. Hii awamu bado hamjaielewa nadhani Subirini tufike 2018 kwenda mbele uone jinsi watu watakavokuwa wanampokea mfalme Wao magufuli na Prince wetu makonda
Hapa kazi tu.. SISI tunataka viongozi wawajibikaji na Walio wazi. Basi.. Hizo kelele nyingine mtaishia humu humu mtandaoni.
 
Kamwambie yeye na huyo anamweka mjini tunaham nao
Hahaha tena uzuri wa Sasa hatuwezi kuandamana kama zamani.. Vijana wenu wa kinondoni na arusha wako na arosto.. Kelele zenu hiz mtaishia humu humu mtandaoni.. Hakuna pesa ya kuratibu hata hizo operesheni uchwara zenu
 
Aoneshe utii katika kutolea ufafanuzi yale aliyotuhumiwa. Vinginevyo asubiri hukumu ya sheria ya asili (nature) Ambayo yeye na wakili wake wote "malikanyanga" sijui hapo"" nimempatia hayati Nyerere?

Na washawasha!
 
Hahaha tena uzuri wa Sasa hatuwezi kuandamana kama zamani.. Vijana wenu wa kinondoni na arusha wako na arosto.. Kelele zenu hiz mtaishia humu humu mtandaoni.. Hakuna pesa ya kuratibu hata hizo operesheni uchwara zenu

Mkuu tena bora hata hayo maandamano, huu ukweli unaomwaga huku mitandaoni ni shida. Na sasa hivi watu wote wanaojitambua wanasoma mitandao ya jamii. Hata house girl humuongopei tena.
 
Makonda ni robot, unachotakiwa ni kushika remote tu na kubonyeza.
 
Back
Top Bottom