UZUSHI Ukila Tango na Asali unaweza kupoteza Maisha

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
1697713920028.png
Wakuu habari,

Leo katika pita pita zangu nikakutana na uvumi kuwa mtu akila Tango na Asali anaweza kufa.

Je kuna ukweli wowote juu ya hilo? Na kama kuna ukweli chanzo kitakuwa nini?
 
Tunachokijua
Ukiambiwa kutaja bidhaa moja inayoweza kutunzwa kwa miaka mingi pasipo kuharibika hauwezi kuikwepa asali.

Historia ya chakula hiki imedumu kwa karne nyingi, kuanzia enzi za mababu zetu hadi sasa ambapo hutengenezwa kwa viambata viwili vikubwa vya maji na sukari.

Kwa mujibu wa USDA, asali huwa pia na amino acids, protini, viondoa sumu, vitamini mbalimbali pamoja na madini chuma, sodium, zinc.

Baadhi ya faida zinazohusishwa na ulaji wa asali ni kuongeza kinga ya mwili, husaidia kutibu vidonda na kikohozi, huongeza nishati mwilini lakini pia husaidia kuondoa sumu mwilini.

Kwa upande mwingine, zaidi ya asilimia 95 ya tango huwa ni maji. Hubeba pia nishati, protini, wanga, nyuzilishe, viondoa sumu pamoja na sukari kidogo.

Huwa pia na madini chuma, calcium, zinc, selenium, magnesium, phosphorus, potassium, sodium pamoja na vitamini C, vitamini B6, thiamin, riboflavin na folate.

Baadhi ya faida za ulaji wa tango ni kuongeza maji mwilini, huhitajika kuboresha afya ya ngozi, kucha, moyo, na nywele pia husaidia kutoa kinga dhidi ya kisukari na aina mbalimbali za saratani.

Mchanganyiko wa asali na tango unaua?
Uvumi huu umekuwepo kwa muda mrefu. Mathalani, Oktoba 24, 2016, mdau wa JamiiForums aliwahi kuzungumzia suala hili. Mdau huyu alisema:

"Habari wakuu...

Kwa muda mrefu sana labda tokea huko tunakua, nimekuwa nikisikia ukila tango na asali pamoja unakufa. Kwa mwenye utafiti anifahamishe."


Aidha, Mei 19, 2022, mtumiaji wa Mtandao wa X (Zamani Twitter) anayefahamika kwa jina la Bakundukize aliomba ushauri juu ya uvumi huu akidai kuwa inasemekana mchanganyiko wa asali na tangu huzalisha sumu.

cucumber1.jpg

Mchanganyiko wa Asali na Tango/Google
JamiiForums imezungumza na wataalam wa lishe waliothibitisha kuwa mchanganyiko wa Tango na Asali hauna athari mbaya kwa afya, pia hauzalishi sumu.

Aidha, kwa Tanzania hakuna kumbukumbu rasmi kutoka mamlaka za afya za uwepo wa mtu aliyefariki au kupatwa na madhara kwa kutumia mchanganyiko huu.

Katika utafutaji wa kimtandao, JamiiForums imebaini kuwa baadhi ya nchi duniani hutumia mchanganyiko huu kama sehemu ya mlo wao wa kila siku.

Mathalani, Lithuania, mojawapo ya nchi zinazopatikana Barani Ulaya, ni mojawapo ya sehemu zinazotumia sana mchanganyiko wa asali na tango.

Julai 7, 2016, tovuti ya International Cuisine ilichapisha makala fupi yanayofafanua asili ya chakula hiki nchini humo, na jinsi ambavyo huvutia kwa walaji wake.

"Sikuwa nimewahi kufikiria kuchanganya matango na asali lakini kwa kweli husababisha uraibu kwa kiasi fulani. Tulifurahia kifungua kinywa hiki hasa nyakati za kiangazi zenye joto kali kama sehemu ya mlo wa Kilithuania. Leo, sahani hii ni ya kawaida katika Ulaya ya Mashariki. Furahia!" sehemu ya maneno ya tovuti hii inaandika.

Huu ni uthibitisho mwingine kuwa mchanganyiko wa asali na Tango hauna madhara na unaweza kutumika kama sehemu ya chakula.

Pia, mmojawapo wa watumiaji wa Jukwaa hili alithibitisha kuwa mara kadhaa amekula mchanganyiko huo na hajafa. Alisema;

"Simjibu Mtu. Kwa uzoefu wangu nimekula mara nyingi Tango na Asali na bado ninapumua. Hadithi za bibi. Taja watu wawili unafahamu ama uliosoma gazeti au kusikia Redioni, kwamba walifariki Kwa kula Tango na Asali!"

Madhara ya mchanganyiko huu
Watu wenye mzio (Allergy) wa Asali au Tango wanaweza kupatwa na changamoto za kawaida ambazo mara zote huhusishwa na ulaji wa vyakula hivi.

Baadhi ya athari hizo ni miwasho, wekundu na kuumuka kwa ngozi pamoja na tumbo kujaa gesi.

Tahadhari
Mchanganyiko huu haufai kutolewa kwa watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja kwa kuwa mfumo wao wa kinga, pamoja na ule wa chakula huwa haujakomaa vizuri.

Asali huwa na uwezekano mkubwa wa kubeba bakteria wabaya jamii ya Clostridium botulinum ambao kwa umri huo, mtoto huwa hawezi kuwaharibu akiwala.

Husababisha tatizo hatari lisilo onekana mara kwa mara linaloitwa Infant botulism ambalo huwa na dalili za choo kigumu, kuweweseka, kifafa, changamoto za kupumua na hatimaye kifo ikiwa msaada wa haraka hautatolewa.

isifood-in-vitro-1.jpg

Clostridium botulinum/ Google
Watoto wenye zaidi ya mwaka mmoja, watu wazima, wanawake wajawazito pamoja na wazee wanaweza kutumia mchanganyiko huu kwani miili yao huwa imekomaa vya kutosha kupambana na bakteria hawa.

Aidha, tango halina madhara yoyote kwa watoto hivyo wanaweza kupewa muda wote pasipo kuchanganywa na asali.
Mimi nilishakula Tango na Asali mbona nipo hai.... Huo ni uongo kama uongo mwingine
 
Jaribu uone cha mtema kuni. Utahisi moyo unaungua that's really bad.
Uwongo na uzandiki mimi nimtumiaji wa asali kila siku nachukua slice mbili za mkate napakaza asali plus yai jicho la ngombe plus hivo vitango nafanyaga kama sandwichi nakula safi kabisaa hayo mengine nakuachia mwenyewe ni sawa na kusema asali na ndimu ukila unakufa sio kweli .
 
Uwongo na uzandiki mimi nimtumiaji wa asali kila siku nachukua slice mbili za mkate napakaza asali plus yai jicho la ngombe plus hivo vitango nafanyaga kama sandwichi nakula safi kabisaa hayo mengine nakuachia mwenyewe ni sawa na kusema asali na ndimu ukila unakufa sio kweli .
Blaza usizungumzie haya matango ya mchongo ambayo yapo kibao mjini. Nikikupa tango lenyewe la asili huchukui raund unakufa kama panyabuku kwenye maji
 
Fanya research kwa kula tango na asali Kisha ulete mrejesho hapa jukwaani. Kama ukifariki acha ujumbe kwa mwana jukwaa atujuze ukweli wa utafiti wako.
Uongo mimi ninatumia asali na tango kwenye mkate naweka katikati mbona sijafa tena ni tamu haswa ...chukua asali tia kwenye mkate kisha weka slesi za tango kisha fun8ka na mkate kula ni tamu haswa
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom