Haikuandikwa pahala popote, lakini Nyerere alijitahidi sana kuhakikisha kuwa mgombea urais nchini hatoki miongoni mwa makabila au kanda zenye watu wengi sana wanaofananafanana kitabia na kiutamaduni kama vile kanda za ziwa, nyanda za juu kusini, na mashariki mwa Tanzania.
Wachagga, wapare, wamasai, wambulu na waarusha kwa pamoja ni wengi na wana sifa sinazoshabihiana.
Wasukuma, wanyamwezi, waha, wahaya, wakerewe, wakuria, wajaluo na wagita ni wengi sana na wana tabia zinazosikilizana.
Mbeya, Iringa na Ruvuma ni wengi sana na wana tabia zinazorandana.
Hivyo, mgombea yeyote atakayetokana na makabila ya wasukuma, wanyakyusa na wachagga ana uwezekano mkubwa wa kuungwa mkono kwa wingi na watu wanaotoka makabila yao na makabila yaliyoko kwenye kanda zao na kusababisha makabila haya yawe kigezo cha kushinda uchaguzi Tanzania.
Hii inaweza kusababisha kila chama cha siasa kusimamisha mgombea wa kutoka makabila ya kisukuma, kichagga/kiarusha, au kinyakyusa ili kupata mtaji wa kura nyingi.
Hii itakuwa sawa na Kenya ambako kabila la Kikuyu na Kijaluo ndiyo yenye kura ya turufu ya kushinda uchaguzi wa urais. Tukifanya hivyo sisi Tanzania tutakuwa tunarudi nyuma kule tuliko toka.
Kila mtu anayo haki kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa, lakini tunajiandaaje kukabiliana na hatari ya kurejesha ukabila nchini ndio jambo la msingi linalopaswa kujadiliwa kwenye uzi huu.