Ukikutana na Lowassa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukikutana na Lowassa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Calnde, Aug 18, 2011.

 1. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2011
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Edward Ngoyai Lowassa! Nina Mengi ya kumweleza. Nikikutana naye sitamwambia kuwa yeye ni fisadi, wala kwamba yeye ni GAMBA.

  Ila nitamwalika kwa chakula cha jioni. Nitamwambia yeye ni mchapakazi hodari ila kuna mambo anatuficha. Nitamwambia atuambie wakati wanapitisha mkataba wa Richmond JK alikuwa wapi. Nitamwambia aniambie kwanini alikubali kumwachia JK urais ili hali alikuwa na nguvu na ushawishi zaidi yake.

  Atuambie hii mambo ya rafikiye Rostam imekaaje. Atuambie mpango wake wa 2015. Atuambie kama kweli anaipenda CCM.

  Atugusie kidogo ugomvi wake na Sitta. Labda atumegee kaumbea kidogo, kama ile mambo yake na buriani ni ya kweli!

  Atumegee kidogo na 'kauwekezaji' ka kijana wa rais. Atupe yale ambayo Mwakyembe alisema 'hatujayasema'. Pengine na ya Chenge, Shimbo labda na Luhanjo! Halafu kama wafanyavyo wengine, atutajie kautajiri kake kwa faida yetu.

  Hii inaweza isiwe na maana yeyote ile, ila moja tuu! Kushuhudia maziko ya kinachoitwa chama tawala na kuibuka kwa chama tawala kipya!

  We mwenzangu ukikutana naye utamwambia nini? Na ukikutana na JK je?
   
Loading...