Ukikutana na JAMBAZI Uwe na NIDHAMU

Ukikutana na JAMBAZI Uwe na NIDHAMU

Mchunguzi Huru yuko sahihi kabisa.

Hata siku moja usimsumbue jambazi, kuwa mkweli na usithubutu kumkimbiza jambazi.

Kuna issue moja ilitokea Tabata majambazi au niseme wauaji walikwenda kumuua kwa makusudi aliyekuwa mtumishi wa TRA. Walikuwa wamemwinda siku nyingi wakawa wanamkosa, nahisi walitumwa kufanya kazi maana hawakuiba.

Siku ya siku wakamfuatilia wakajua yuko kumbe alikuwa amesafiri. Walipofika wakamkuta mke na mtoto wao. Walipomuuliza mke hakuwa mkweli kusema kuwa mume hayupo amesafiri, pale pale wakamwambia sasa ngoja tukufanyie kitu ili ujue kuwa tuko serious. Pale pale walimpiga yule mtoto risasi na kufa pale pale na alikuwa ndiye mtoto pekee of course mdogo, then wakapanda juu ghorofani na wakatafuta hawakumpata.

Waliposhuka chini yule mama ndipo akasema ukweli kuwa mume alisafiri yuko Mbeya. Jambazi alimwambia hivi 'mama ungesema ukweli tangu awali na kuacha ubishi mtoto wako angekuwa hai, na iwe fundisho kwako". Hiki kisa nilisimuliwa na tangu siku hiyo nilisema kabisa akija jambazi nitampa hela niliyokuwa nayo, kadi ya bank na password kabisa, ofcourse ninakuwa na account za kawaida zisizo nono sana, nitampa funguo za magari yote kama anataka.

Yote hayo ni kuokoa roho yangu maana nikiwa hai magari nitanunua na pesa nitatengeneza kupitia miradi yangu. Jambazi si ndugu yako, wengine wanachonga hata kuua ndugu ili wapate pesa, sembuse wewe kanyaga twende? Mwenye silaha mpishe hata kama ni nondo ya kibaka.
 
Mkuu Wewe jambazi! Unataka tukupe hela kuwa urahisi tu! Hatuwapi!
 
Mi Mungu anisaidie mi ni jasiri kamwe siwezi kuwaruhusu wachukue bure, bora nami nibaki na kucha yake!
 
Wengine unatoa pesa na kisha wanakumaliza kuondoa ushahidi kwa kweli hawatabiriki
 
Wewe mleta mada, Mchunguzi huru, si ajabu wewe ulikuwa miongoni ya hao majambazi waliokuwa kwenye pikipiki, waliomuua huyo Sista.

Haiwezekani ucomment kuwa raia wema wanapokumbana na kadhia ya kukutana na majambazi au vibaka, wajisalimishe kirahisi na kutoa kila walichonacho, ili tu wasalimishe maisha yao.

Comments hizo pia zitawapa pia kichwa hao majambazi na vibaka kuongezeka zaidi mitaani, wakijua popote pale watakapowavamia raia wema, watasurrender kiulaini, kwa kufuata ushauri wa mchunguzi huru, kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kusalimisha maisha yao!

Kwa kuwa kitendo cha kuuawa sista ni kitendo cha kikatili na unyama wa hali ya juu, na kwa kuwa jeshi la polisi limekiri kuwa halijamtia mbaroni hata mtuhumiwa mmoja, basi ingekuwa vyema likaanza kwa kumkamata mchunguzi huru, ili aisaidie polisi katika uchunguzi wa kuwanasa 'wenzie' walioshiriki katika kuitoa roho ya huyo sista ambaye hakuwa na kosa lolote!

Matatizo ya umeme kukatika.
sijakuelewa ngoja uwake labda.
 
Kumbe ni 2 mil!,Siamini hilo. Sasa mbona kwenye vyombo vya habari wamesema kiasi kilichoibiwa hakijafahamika?
 
Siwezi kufa kizembe ubishi lazima uwepo, unaweza kuwa mpole na kuwapa kila wanachotaka na bado wakakuua.
 
  • Thanks
Reactions: y-n
10492406_884030108320025_1746256827670088025_n.png
 
unazungumzi hawa majambazi wa kova Pia.....?
 
Aah wapi siku hiyo mbona tutabakana hapo hadi mwaka mpya!! Pesa zinatafutwa kwa tabu ati.
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Mchunguzi Huru yuko sahihi kabisa. Hata siku moja usimsumbue jambazi, kuwa mkweli na usithubutu kumkimbiza jambazi. Kuna issue moja ilitokea Tabata majambazi au niseme wauaji walikwenda kumuua kwa makusudi aliyekuwa mtumishi wa TRA. Walikuwa wamemwinda siku nyingi wakawa wanamkosa, nahisi walitumwa kufanya kazi maana hawakuiba. Siku ya siku wakamfuatilia wakajua yuko kumbe alikuwa amesafiri. Walipofika wakamkuta mke na mtoto wao. Walipomuuliza mke hakuwa mkweli kusema kuwa mume hayupo amesafiri, pale pale wakamwambia sasa ngoja tukufanyie kitu ili ujue kuwa tuko serious. Pale pale walimpiga yule mtoto risasi na kufa pale pale na alikuwa ndiye mtoto pekee of course mdogo, then wakapanda juu ghorofani na wakatafuta hawakumpata. Waliposhuka chini yule mama ndipo akasema ukweli kuwa mume alisafiri yuko Mbeya. Jambazi alimwambia hivi 'mama ungesema ukweli tangu awali na kuacha ubishi mtoto wako angekuwa hai, na iwe fundisho kwako". Hiki kisa nilisimuliwa na tangu siku hiyo nilisema kabisa akija jambazi nitampa hela niliyokuwa nayo, kadi ya bank na password kabisa, ofcourse ninakuwa na account za kawaida zisizo nono sana, nitampa funguo za magari yote kama anataka. Yote hayo ni kuokoa roho yangu maana nikiwa hai magari nitanunua na pesa nitatengeneza kupitia miradi yangu. Jambazi si ndugu yako, wengine wanachonga hata kuua ndugu ili wapate pesa, sembuse wewe kanyaga twende? Mwenye silaha mpishe hata kama ni nondo ya kibaka.

unapendele mitaa gani nije nichukue vyako kuiulahisi, yaani hata kwa nondo.! Vyangu jambazi atachukua kama anabunduki yenye risasi, na ameshapiga juu kadhaa au ameshatoa mfano wa kuuwa kwa vitendo
 
  • Thanks
Reactions: y-n
unapendele mitaa gani nije nichukue vyako kuiulahisi, yaani hata kwa nondo.! Vyangu jambazi atachukua kama anabunduki yenye risasi, na ameshapiga juu kadhaa au ameshatoa mfano wa kuuwa kwa vitendo

kama alivyotoa mfano kwa huyo sista mkatoliki, lol!
 
Kwangu mimi km hakuna namna ya kujinasua ni afadhali nikawapa jamaa mgao wao. Kwa sababu mara nyingi hawa jamaa hawana muda wa kupoteza na wakiona unazingua tu wanaweza kufanya lolote usilotegemea.

Nakumbuka rafiki yangu alikutana na vibaka mtaani kwake akawazingua baada ya kuwa wametaka salio. Alikula nondo ya kichwa na jamaa walichukua walichotaka na kumtupa mtaroni wa maji machafu. Ilikuwa ni usiku mwingi jamaa alishtushwa na baridi kali la siku ya pili asubuhi.
 
Back
Top Bottom