Ukijitambua utafika mbali sana

Ukijitambua utafika mbali sana

Encryption

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
999
Reaction score
1,356
UKIJITAMBUA UTAFIKA MBALI SANA
………….. Maisha yako, yamo mikononi mwako KABISA.
LAKINI, katika ulimwengu huu, ni rahisi sana kuyapaki pembeni,
Ukaanza kuishi maisha ya watu wengine.
………….
Fikiria mtu ambaye kutwa kucha:
Anavaa kama staa fulani,
Ananyoa kama staa fulani,
Anahangaika kwenda na fasheni fulani za mavazi,
Yuko bize kushabikia chama fulani, nk, nk.
………….
Maana yake ni hii:
Unakuwa umeacha kuishi maisha yako lakini unaendeleza maisha ya mwingine.
…………
Kwenye maisha yako umepewa mitaji mingi. Baadhi yake ni:
- Muda
- Afya
- Nguvu
- Akili.
………….
Sisemi kushabikia mambo ni vibaya;
Lakini unapotumia muda kila siku kwa ajili ya kushabikia wengine;
Huku hufanyi cha maana kwa maisha yako, liko tatizo.
…………
Muda haumngoji mtu; wala haujali.
Ukitumia saa moja au mbili KILA siku kwa mambo yasiyokuzalishia chochote,
Maana yake UNAFYONZA MITAJI YAKO hiyo na kuwapa wengine.
…………..
Mfano:
Kila siku unanunua bando lakini unachofanya ni:
- kutukana tu watu mtandaoni
- kuangalia ngono
- kusikiliza muziki
- kuangalia mpira
- kushabikia siasa, nk
…………
Kupitia tabia kama hizo, wapo wanaofaidika na MUDA, AFYA, NGUVU na AKILI yako.
Lakini wewe je?
Unapoteza, na kupoteza, na kupoteza.
………..
Mambo MENGI ya hasara kama hayo, ukifanya sasa,
Wala hutaona madhara yake,
Lakini ukijumuisha ya leo, kesho, mwezi ujao, mwaka ujao,
Mkusanyiko wake NI HASARA KUBWA MAISHANI MWAKO ambayo
Atakayeilipa ni wewe mwenyewe.
…………..
Utailipaje basi?
Utailipa kwa kuendelea kuishi kwenye umaskini, huku
Wengine wakinufaika kwa nguvu zako, fedha zako, akili yako na muda wako.
………….
SASA KUJITAMBUA NI NINI?
Kujitambua ni kuelewa kuwa dereva wa maisha yangu ni MIMI MWENYEWE.
Niache kufanya mambo kwa kufuata mkumbo.
Kama ambavyo kufanya mambo HASI KIDOGOKIDOGO, mwishowe hasara ndogondogo yanayonipa ITARUNDIKANA na kuwa kubwa;
Vivyohivyo, nikitumia muda, afya, akili na nguvu zangu kufanya mambo CHANYA KIDOGOKIDOGO, faida kidogokidogo yanayonipa, ITARUNDIKANA na kuwa dhahiri baada ya muda fulani.
………….
Maisha YAKO FAIR.
Kamwe hayampendelei mtu, wala hayamwonei mtu.
Ukifanya vibaya, yatakulipa hasara.
Ukifanya vema, yatakulipa mafanikio.
 
Kila mtu aishi atakavyo ili mradi asiharibu maisha ya wengine.

Zingatia "asiharibu maisha ya wengine"
 
Ata kusoma na kuchangia mada hii ni kupaki gari pembeni..
 
Kweli kabisa mkuu,mtu anafanya kazi masaa 5tu kati ya 24 ina maana kwa mwaka atafanya masaa mangapi? akiishi miaka let say 50? Halafu analalamika maisha magumu,Anataka kula nguvu za wenzake yeye abaki kwenda na fasheni tuu.
 
Asante sana mkuu kwa ujumbe mzuri wenye ukumbusho.....
Ubarikiwe sana.....

Bila shaka vijana watajifunza mengi kupitia hili andiko lako.....
 
Mkuu maisha Ni Tofauti sana na ulivyoandika. Wengi wangependa yawr kama hiyo positive side uliyoiandika lakini kuna "Clock of Life".
 
Ni bandiko nzuri sana
Angalizo:makosa yako au uzembe wako ni faida kwa wengine
 
Umejitahidi kunena kweli yenye mantiki, mafanikio au kushindwa ni zao la matokeo ya maandalizi na mipango binafsi. Ifahamike kuwa neno KUSHINDWA limetumika kama uzoefu wa kujaribu mambo kwa njia tofauti tofauti Wagunduzi wa Vitu vingi tunavyo tumia leo walipitia KUSHINDWA kuliko tunavyo fikiri kwahiyo KUSHINDWA sio MTAJI wa kukata Tamaa na kuanza kulalamika.
 
Back
Top Bottom