Ukiitiwa fursa ujue wewe ni fursa

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,480
5,502
Fursa ni nini?

Katika kufanya kazi na wajasiriamali wengi nimegundua kwamba wengi huchanganya FURSA na kujikuta wanapoteza FURSA.Kama mjasiriamali na mtu mwenye kiu ya mafanikio lazima ujue kwamba KILI KITU na KILA MTU na FURSA kwa kutegemea jinsi unavyokitazama.

Kwa mfano kama mtaa ni mchafu kwa matu anayejua kutazama fursa basi ataona fursa ya kufanya usafi ili mazingira yawe bora na kwa mtu asiyekuwa na macho ya fursa atasema huu mtaa haufai kuishi atahama.Ukiangalia hapa utaona kwamba wote wameona jambo moja ila kila mmoja amelitafsiri mwenyewe na kufanya maamuzi mwenyewe.

Kuna ka msemo ka watu waliokata tamaa na wasiokuwa na maono kanakopendwa sana na LOOSERS kwamba UKIONA FURSA UNAITIWA FURSA UJUE WEWE NI FURSA.Wanasahau kwamba wahenga walishasema USIKATAE WITO KATAA ULICHOITIWA.Ukiitiwa FURSA na ukaona haikufai unao uwezo wa kuikataa ila usikatae kuifahamu FURSA kwani unaweza kujifunza kitu tofauti.

FURSA ni FURSA tu bila kujali nani anaitiwa FURSA.

Andiko hili ni FURSA kwako ila jinsi utakavolitazama unaweza usipate matokeo mazuri

Hivyo basi niwakaribishe wakati tunasubiri matokea na KUAPISHWA kwa RAIS wetu tujadili kuhusu FURSA na Namna tunaweza kuzitumia na KUTENGENEZA Fursa zaidi kwa ajili ya wengine.

Karibuni
 
Watanzania tunazidi kuwa waandisha wazuri na kuzidi kugundua maneno ya ushawishi
 
Vipi Hapo FOREVER LIVING wote mmeishanunua Range rover sports? na zile safari za Dubai, ibiza na Miami zinaendaje huko.
 
Back
Top Bottom