Ukiandaa dodoso kama hili na ukapitisha vyuo vikuu, majibu utakayopata unaweza kutamani kuhama nchi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,673
149,860
Andaa dodoso yenye maswali haya na kisha uipitishe vyuo vikuu uombe wanafunzi wakujazie.Majibu utakayopata yatakusaidi kujua ni kwanini tuko hapa tulipo kama Taifa.

Maswali:

1.Taja jina la Msajili wa vyama vya siasa hapa nchini

2.Naibu Spika wa Bunge lililopita (Bunge la 10) alikuwa nani

3.Taja jina la aliekuwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba

4.Taja vyama vya siasa vinavyounda umoja wa UKAWA

5.Samweli Sitta alikuwa Spika wa Bunge la ngapi

6.Taja jina la mwanamke aliegombea uraisi katika uchaguzi mkuu uliopita

7.Taja jina la chama ambacho mwanamke huyo alitoka

8.Taja jina la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

9.Taja jina la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.

10.Taja kirefu cha chama siasa kinachojulikana kwa kifupi kama CUF.

11.Katiba ya Tanzania ni Katiba ya mwaka gani.

12.Peter Msigwa ni mbunge kutoka mkoa gani

13.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi anaitwa nani

14.Taja jina la kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni

15.Taja kirefu cha neno UKAWA

16.Maandamano ni haki ya kikatiba au uamuzi wa Jeshi la Polisi

17.Deni la Taifa kwa sasa ni kiasi gani

18.Mfumo wa vyama vingi hapa nchini ulianza rasimi mwaka gani

19.Nani kiongozi wa shughuli za serikali Bungeni

20.Bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ni kiasi gani.

21.Katibu wa Baraza la Mawaziri ni nani/huwa na cheo gani?

Ninaamini majibu ya maswali haya yatakusaidia kujua ni namna gani watanzania tunafuatilia habari za siasa na wanasiasa na hivyo itakupa picha kama wanaweza kuchagua kiongozi bora au bora kiongozi.
 
Wale majamaa ambao wako pale NASA HQ jinsi navyowaona sidhani hata kama kura huwa wanapiga# watu wana interest tofauti maana watu hao hao ukiwauliza yanayowahusu watakujibu
 
labda haina umuhimu wa kukumbuka wala kuhifadhi, utahifadhi watu ama matukio yasio na tija?
binafsi naona ni bora hichi kioja chako kuliko kukaa ukawasikiliza hao uliowataja wakiongelea chochote kuhusu nchi yetu iwe cha maendeleo ama utafunwaji wa nchi hii. i have lost their touch.
 
wengne umeshawanasa hapahapa!hahahaa.. eti field, kwahyo kufaham mfumo wa vyama vng ulianza lini tasmi Tz inahtaji uwe umesoma ps hapo chuo!?utan tu..hahahaa..
 
labda haina umuhimu wa kukumbuka wala kuhifadhi, utahifadhi watu ama matukio yasio na tija?
binafsi naona ni bora hichi kioja chako kuliko kukaa ukawasikiliza hao uliowataja wakiongelea chochote kuhusu nchi yetu iwe cha maendeleo ama utafunwaji wa nchi hii. i have lost their touch.
Ukishindwa kujibu maswali haya unaweza kuchagua kiongozi bora?
 
Andaa dodoso yenye maswali haya na kisha uipitishe vyuo vikuu uombe wanafunzi wakujazie.Majibu utakayopata yatakusaidi kujua ni kwanini tuko hapa tulipo kama Taifa.

Maswali:

1.Taja jina la Msajili wa vyama vya siasa hapa nchini
2.Naibu Spika wa Bunge lililopita (Bunge la 10) alikuwa nani
3.Taja jina la aliekuwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba
4.Taja vyama vya siasa vinavyounda umoja wa UKAWA
5.Samweli Sitta alikuwa Spika wa Bunge la ngapi
6.Taja jina la mwanamke aliegombea uraisi katika uchaguzi mkuu uliopita
7.Taja jina la chama ambacho mwanamke huyo alitoka
8.Taja jina la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
9.Taja jina la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar
9.Katiba ya Tanzania ni Katiba ya mwaka gani.
10.Peter Msigwa ni mbunge kutoka mkoa gani
11.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi anaitwa nani
12.Taja jina la kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni
13.Taja kirefu cha neno UKAWA
14.Maandamano ni haki ya kikatiba au uamuzi wa Jeshi la Polisi
15.Deni la Taifa kwa sasa ni kiasi gani
16.Mfumo wa vyama vingi hapa nchini ulianza rasimi mwaka gani
17.Nani kiongozi wa shughuli za serikali Bungeni

Wako walimu wengi tu wanaofundisha GS..hayo maswali yatawatoa nduki.....na wamepita huko University unakosema!!!!!
 
Upeo wao wa mambo wanafunzi wa siku hizi ni mdogo sana,ndio maana huwezi siku hizi ukasikia wanapinga uovu wowote unaotokea kwenye jamii,hakuna kugomea uvunjifu wa haki za binadamu,hakuna midahalo.Wapo wapo tu...kama UD zamani Enzi za kizazi cha kina Sitta,kina JK, Mbatia na Zitto ilikuwa kisima cha maarifa na mapinduzi ya fikra...sasa hivi wamekuwa hohehahe...wanasubiri wapewe elfu kumi wavuruge midahalo ya katiba nk...
 
Kule waulize
1.Mke wa diamond ni Nani
2.imba wimbo wowote diamond au Ali kiba
3....
Maswali mengine ambayo vijana wetu watajibu kwa haraka:
3. Ronaldo anachezea timu gani.....
4. Ni nani bingwa wa ligi kuu ya Uingereza....
5. Baba yake Rooney anaitwa nani.....
6. Messi anatoka nchi gani....
6. Michael Jackson alikuwa anatoka nchi gani....
7. Wimbo wa Chura uliopigwa marufuku ulitungwa na msanii gsni......
 
hilo LA 11 hata siafu na ngedere WANALIJUA maana WKIMUONA 2! wanajua safari ya kupanda NDEGE Imewadia!!!
 
Maswali mengine ambayo vijana wetu watajibu kwa haraka:
3. Ronaldo anachezea timu gani.....
4. Ni nani bingwa wa ligi kuu ya Uingereza....
5. Baba yake Rooney anaitwa nani.....
6. Messi anatoka nchi gani....
6. Michael Jackson alikuwa anatoka nchi gani....
7. Wimbo wa Chura uliopigwa marufuku ulitungwa na msanii gsni......
Uko sahihi kwa asilimia 100.Hawa ndio wapiga kura wa nchi hii!
 
Back
Top Bottom