Ukerewe, Mwanza: Polisi ajinyonga kwa kipande cha chandarua

Ukerewe, Mwanza: Polisi ajinyonga kwa kipande cha chandarua

mtu watu

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2017
Posts
2,123
Reaction score
1,617
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Kituo cha Nansio wilayani Ukerewe, John Kalongola amejinyonga kwa kipande cha chandarua nyumbani kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema mwili wa askari huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe.

Amesema baada ya uchunguzi na utaratibu kukamilika mwili utasafirishwa kwa mazishi mkoani Iringa.

Kamanda Msangi amesema mwili huo ulibainika baada ya harufu kutoka ndani ya nyumba yake na mlango ulipovunjwa ulikutwa ukining’inia.

Mwili wa askari huo uligunduliwa jana Ijumaa Desemba 29,2017. Amesema kipande cha chandarua kilifungwa juu ya dari.

Chanzo; Mwananchi
 
nazani depo wanapaswa kuongeza nguvu kwenye mafunzo ya saikolojia ya askari ... nahisi kuna shida sehemu kwa matukio ya askari wengi
Inafaa kuwa hivyo pengne na ugumu ma maisha unaweza kuchangia!
 
Huko Majeshini kunapaswa kuwa Vitengo madhubuti vya Ushauri Nasaha, ingawaje asilimia kubwa tuna Msongo wa Mawazo ila wenzetu wamezidi, sasa ukizingatia zile Silaha wanazokabidhiwa ni bora Kinga kuliko Tiba!
 
Back
Top Bottom