Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
UKEREWE: Siku chache baada ya wakulima mkoani Simiyu kutakiwa kulima mazao yanayostahimili ukame, Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mkoa wa Mwanza, Estomiah Chang’ah amepiga marufuku biashara ya kuchoma mahindi mabichi.
Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka aliwataka wananchi kulima mazao yanayostahimili ukame ili kujikinga na tishio la njaa.
Hatua hiyo inatokana na hali ya ukame iliyopo katika maeneo mengi nchini, sanjari na agizo lililowahi kutolewa na Rais John Magufuli kwa wakuu wa wilaya na mikoa wahakikishe maeneo yao hayakumbwi na njaa.
Akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Stendi ya Zamani mjini Nansio, Chang’ah aliwataka kuacha biashara ya kuchoma mahindi kama moja ya mikakati ya kukabiliana na tatizo la upungufu wa chakula.
Chanzo: Mwananchi