Uke wenza...

pisi jacky

Member
Oct 21, 2020
31
150
Happy new year

Hope mko poa, tuanze mwaka na simulizi izi mbili za wake wenza.

Ya kwanza ni ya kijana mmoja natamuita dany, dany alioa kwa bahati nzuri au mbaya mkewe hakubahatka kuzaa ivo dany katika pita pita zake akakutana na kabinti kamoto kweli yule binti alibeba mimba na kuzAa kidume, Basi nakumbuka wakati wa kuja kumtolea mahali yule binti hapa mtaan wamama wote walioenda kupika waliondoka na ten kama shukran ya wamama wa jikoni.

Siku zikaenda binti akapendwa haswa akapewa adi biashara asimamie, lakin sijui ushamba sijui utoto au ndo wivu kale kabinti kakaanza kumtukana bi mkubwa, "wenye matumbo yetu tumetoka dukani ivi ndo tunahesabu mauzo ya siku nzima" Basi ikawa taflani.

Bimkubwa akaona isiwe shida unacholingia si ilo tumbo lako ngoja nkufunze adabu,. Kabinti siku iyo kamekaa na mtoto vzuri wamecheka mda wa kulala umefika wamelala, usiku wamelala mbona mtoto hata alii nimbadilishe hebu nimuangalie kumgusa mtoto wa baridi kama freezer kwenda hospital jaman mtoto alifariki kitambo.

Basi wakalia msiba ukaisha migogoro ikawa Mingi ikabidi na bwana yule waachane. Kabinti kapo kapo tu

Story namba mbili ntamuita mzee bosco, bwana mzee huyu nae alioa kwa bahat nzuri au mbaya mkewe hakubahatka kuzaa pia. Basi mzee bosco nae akaona isiwe tabu akavuta jiko lingine, lakin alichokifanya mke huyu wa pili alimpeleka nyumba anayoishi bi mkubwa akagawa vyumba wakawa wote wanaishi nyumba moja, alisema ivi nitakaposikia mnagombana mmoja ataondoka umu akiwa kwenye sanduku ntachinja mtu staki ujinga.

Basi kina bibie wakayaAnza Maisha mapya wanapika jiko moja wanaandaa meza moja wakazoeana wakawa mashost hatari kias kwamba watoto wa uyu mke mdogo hawajui nan mama nani sio mama maana wote wakawa mama zao ukiwakuta n kama mtu na dada ake, yaan wake hawa wakimuuzi mzee anatimua wote kulala jikoni na Maisha yakawa ya Amani sana kwa bahat mbaya mzee bosco aliugua ghafla akafariki lakin watoto wake wakubwa na wake zake wapo mpaka leo wanakaa pamoja hamna alieolewa Wala nin wote wapo wanalea watoto

Moral of the story
Maisha n zawadi kutoka kwa Mungu hayupo atakaeishi milele sio mkeo sio mmeo.

Ndoa na iheshimiwe na watu wote mwanaume unaetaka kuoa wake wawili usiruhusu hata siku moja mke mkubwa adharaulike always mwisho wake hua n mbaya sana na wenye madhara mengi

Mwanaume ni kichwa usipoongoza wewe wote tunapotea simamia nafasi yako

Tudada mnaoolewa wake wa pili usijione we ndo supu ya kuku na juisi ya embe, mwenzio n mgagani my friend wanaume ni kama gwaride wakienda umbali mrefu kuna wakati wa nyuma geuka. Dada utapata kichaa mheshim mwenzio uliemkuta hujui n wapi wametoka adi kufika apo

ANGALIZO; wanawake wote mnaowaungia wanaume midawa ili wawapende zile dawa hua hazifanyi kazi bure, kuna mmama alikuja kanisan analia watoto wake wanakufa ghafla katika kuombewa mchungaji akamwambia, ndan mwako umetunza nin akajibu hamna kitu kaulizwa una uhakika badae ndo akaanza mi tangu mme wangu anioe natumia dawa ili asimpende mwingine na aniskilize mim tu. mchungaji akamwambia bas io ndo inamaliza wanao kuombewa kutupa dawa na mumewe akamuacha from that moment

Hayupo anaweza kutulindia ndoa isipokua Yesu tu ukijifanya unajenga angalia usibomoe na hasira siku zote n hasara, wanawake wengi waliochika kwa kumwacha mwanaume kisa kaoa mke mwingine wengi wanajutia maamuz yao, akitaka kuoa mwache akikudharau mlilie Mungu kuna bakora yake special inamsubir. hatuishi milele usiumie kias kwamba uisi hapa ndo mwisho wako we're just passing

Mwanaume asievumilika ni anaepga kipigo Cha mwizi huyu ntakushauli ukimbie spidi mia.lakini wengine wote wanavumilika tupige moyo konde bila kuchoka utaachika kungap?

Happy new year once again
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom