Kwanza naomba nikiri kwamba mimi ni nwanachama halali wa chadema,najua itifaki na mlengo wa chadema,na tangu niingie kwenye siasa au kuzijua siasa nmekuwa ni mwanachadema,sijawahi kuwa chama kingine chochote zaidi ya chadema,,lowasa alipokuja chadema na kuwa mgombea uraisi ilibaki kidogo nihame chama,ila niloposoma katiba yetu ya 2006,nikakutana na kifungu kinachoelekeza wanachama kuunga mkono wagombea wanaoteuliwa na chama,,hapo nikawa sina namna mana siwezi kuvunja katiba,
Tuje kwenye makosa yetu sasa
Kiukweli chadema naipenda sana na sifikirii kuhama labda kufanyike makosa makubwa sana ila hiki chama kina matatizo kadhaa ambayo inabidi tujisahihishe,
Kosa la kwanza ,viongozi wetu wana ndimi mbili,yaani leo anaongea hili na kesho lile,kiasi kwamba unashindwa kuwaelewa,mfano"lowasa ni fisadi,lowasa ni mwizi,mkimchagua lowasa mkapimwe akili,,lowasa hafai,lowasa ameiingiza gizani n.k" kesho "lowasa mi mkombozi,lowasa ni safi,lowasa ni shujaa" kwa nini mnatufanya wafuasi wenu chapati?
Kosa la pili ni kwamba chadema hawapendi kukosolewa,yaani ukikosoa chama utaitwa msariti,mamluki,au ccm,,mfano kingunge leo tunamwita kamanda,mtu ambae kazeekea ccm maisha yake yote eti leo anaikana tena kwa sababu ya lowasa afu ukisema uitwe msariti,lowasa,ambe amekuja chadema kwa sababu ya uraisi leo hii umuamini?
Chadema tufike sehemu tutambue kwamba kuna siasa kabla ya uchaguzi,siasa wakati wa uchaguzi na siasa baada ya uchaguzi,sasa ni siasa baada ya uchaguzi tunapaswa kutambua tunakosea wapi??? Na tujisahihishe sasa.
Utawasikia wengine wakiniita majina ya ajabu hapa
okay. Siasa ipo hivi, mtu anaweza kuongea jambo fulani kwa malengo mawili, kwanza kujijenga kisiasa hata kama ni kwa kupotosha umma, pili kuelimisha umma kuhusu ukweli fulani. hivyo waliomnadi lowasa kuwa fisadi walikuwa na ushahidi gani wa matendo, nyaraka na hata video kuuzihilishia umma kuwa kweli lowasa alikuwa fisadi? pili lowasa alisema yeyote mwenye ushahidi nje ya ccm au ndani ya ccm aupeleke mahakani, je ni nani alifanya hivyo? hata kama ana lowasa anapesa je ninani aliyesubutu hata kuonyesha documents za ushahidi kuwa kweli lowasa na richmond ni samaki na maji? hivyo yawezekana chadema kupitia slaa walikuza chama kwa mgongo wa lowasa dhidi ya richmond. that why hata mwakembe na sitta walijitutumua kwa kumzuia lowasa kwenda ikulu kwa maneno bila hata documents zozote ingawa nao walikuwa kwenye kamati husika.. hivyo ingekuwa busara kama wangeongea kwa nyaraka zikionyesha kweli mtu huyu ni muhusika na siyo polojo za maneno kwenye media.