UKAWA wote nipeni majibu

UKAWA wote nipeni majibu

juvenile davis

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2015
Posts
4,752
Reaction score
4,475
WanaJf,

Naamini uchaguzi umeisha na Magufuli ni rais, iwe kwa halali au kwa njia za panya ila ndio rais, kuna lalamikalalamika ya viongozi wetu wa CHADEMA na ukawa kiujumla, kwamba tuliibiwa kura za rais, jambo ambalo mimi siliafiki na nmekuwa nikikwaruzana na wanachama kadhaa wa CHADEMA na kuitwa msariti, mnafiki, gamba, mamluki, CCM.

Ninachopingana na wenzangu ni kwamba hatukuibiwa kura, bali tulikosea kuweka mgombea urais ambaye ana madoa na tumemuimba miaka 8, tumemwita fisadi, mwizi sugu harafu leo anagombea urais, hivi mlitegemea wananchi wangetuelewa vipi?

Sasa naomba mwana ukawa yeyote anieleze"hivi kuhusu Richmond, Lowassa amewahi kujieleza hadharani na tukamuelewa? Mimi binafsi najua akiulizwa utasikia "mwenye ushahidi aende mahakamani" sasa hapo kajibu nini?Au utasikia "hakuna nililofanya ambalo raisi alikuwa hajui", sasa hilo ndio jibu?

Naomba mtu wa UKAWA mwenzangu anipe jibu je Richmond, Lowassa amewahi kujieleza akaeleweka? Kama hapana basi hatukuibiwa kura.
 
Hakuna msemaji wa UKAWA humu, nenda ufipa au buguruni utapata majibu yako safi kabisaa
 
Kama alishinda kihalali kwa nini polisi walikamata vijana wa IT wa CHADEMA na wale wa Haki Za Binadamu? Lengo si kuondoa aina yoyote ya ushaidi? Suala la Richmond Lowassa alijivua siku ile alipojiuzulu uwaziri mkuu.
 
Fanya kazi kijana ukuu wa wlaya safari hii ni mgumu sana na hata huyo Magu hata kuletea sembe nymbni kwako
 
Hebu kwanza tuwe wakweli, umesema "ana madoa" na hii ya kusema kwamba ana "madoa" ni hoja inayotoka CCM lakini mwisho wa siku wanaishia kusema habari ya Ritchmond. badala ya kutumia wingi muwe mnatumia umoja kwa kusema "ana doa" kwani hoja yenu imejikita kwenye Ritchmond.

Wakati fulani huko siku za nyuma tulikuwa na usemi usemao "elimu haina mwisho". Maana ya usemi huu ni kwamba hakuna mwisho wa kujielimisha kuhusu jambo fulani. Zama za kale ilikuwa inaaminiwa kuwa dunia imebebwa juu ya Pembe za mnyama mmoja mkubwa sana anayefanana na Ng'ombe, na mnyama huyo anapojitikisa ndipo yanapojitokeza matetemeko ya ardhi, mpaka leo bado tunaamini hivyo? Sayansi imetusaidia kubadili mtizamo huo wa kizamani kuhusu Dunia na ulimwengu!

UKAWA na CHADEMA wameshajielimisha sana kuhusu sakata la Ritchmond na yatokanayo, ndiyo maana Tundu Lissu alisema kampuni ya Ritchmond Mhusika wake ni Kikwete lakini cha ajabu ni kwamba nyie hamsemi kuwa hilo ni doa kwa Kikwete na Serikali yake!

Lowassa anaposema kwamba mwenye ushahidi aende mahakamani anaongea kimantiki, kwani CCM wanalifanya suala la Ritchmond ni la Kijinai kwa ivo kama ni la kijinai basi ni lazima lipelekwe mahakamani. Kama hamuelewi ni kwa nini Lowassa anasema mwenye ushahidi aende mahakamani basi tena hakuna jinsi ya kuwaelewesha.

Mitambo ya Ritchond ni haramu? si ndiyo ya DOWANS na si ndiyo inayoendelea kutumiwa na Symbion? Symbion imetoa misaada kiasi gani kwa jamii na Serikali yetu, fedha zinazotumiwa kutoa misaada hiyo si zinatokana na uzalishaji wa umeme unaofuliwa na Mashine Haramu zilizoletwa na Ritchmond? Au ndiyo mambo ya Baniani Mbaya kiatu chake dawa?
 
Mbona alikujibu labda IQ yako ndogo thats why darasani mnakuwa mi mwalimu mmoja na wanaweza wakaelewa 40 tu. Kwa kifupi ishu ya Richmond alieleza bayana kwamba yeye aliuliza lakini Mkulu akasema mchakato uendelee hajakana kutuhusika bali aliambiwa asimamie. Kama alikuwa na huisa kwenye ishu ya Richmond si tungemuona kwenye malipo ya huo mkataba maana baadhi yao wamelipwa kupitia ESCROW labda kama mgao wake umefichwa kwenye ile list ya Barclays.
Kuhusu CDM kutopita 2015 sababu sio Edo na angewekwa mtu mwingine awe slaa au lipumba tungepigwa zaidi ya hapa.
Kama skendo ya ufisadi ndio inafanya Mtu asichaguliwe Urais ilikuwaje 2010 JK akapita na makando kando yote ya ufisadi.
Je, aliyepita hana makando kando y ufisadi? Ile ripoti ya PPRA inasemaje kuhusu bilioni 121 zilizopotea hewani. Vipi kuhusu mabilioni ya shilingi wanayolipwa makandarasi kwa riba? Hiyo 10% anapewa nani? Kuna mkandarasi kalipwa barabara ya Tunduru bila hata kufanya kazi na kupewa mkandarasi mwingine huo si ufisadi?
 
Acha umbea wewe fisi wa kijani Lumumba sahiv hakuna vibahasha vya kaki Hazina pamekauka hapana kiyu

Mi ni chadema pure,na sijawahi kuwa ccm na sitakuja kuwa,tukubali kujisahihisha
 
Hebu kwanza tuwe wakweli, umesema "ana madoa" na hii ya kusema kwamba ana "madoa" ni hoja inayotoka CCM lakini mwisho wa siku wanaishia kusema habari ya Ritchmond. badala ya kutumia wingi muwe mnatumia umoja kwa kusema "ana doa" kwani hoja yenu imejikita kwenye Ritchmond.

Wakati fulani huko siku za nyuma tulikuwa na usemi usemao "elimu haina mwisho". Maana ya usemi huu ni kwamba hakuna mwisho wa kujielimisha kuhusu jambo fulani. Zama za kale ilikuwa inaaminiwa kuwa dunia imebebwa juu ya Pembe za mnyama mmoja mkubwa sana anayefanana na Ng'ombe, na mnyama huyo anapojitikisa ndipo yanapojitokeza matetemeko ya ardhi, mpaka leo bado tunaamini hivyo? Sayansi imetusaidia kubadili mtizamo huo wa kizamani kuhusu Dunia na ulimwengu!

UKAWA na CHADEMA wameshajielimisha sana kuhusu sakata la Ritchmond na yatokanayo, ndiyo maana Tundu Lissu alisema kampuni ya Ritchmond Mhusika wake ni Kikwete lakini cha ajabu ni kwamba nyie hamsemi kuwa hilo ni doa kwa Kikwete na Serikali yake!

Lowassa anaposema kwamba mwenye ushahidi aende mahakamani anaongea kimantiki, kwani CCM wanalifanya suala la Ritchmond ni la Kijinai kwa ivo kama ni la kijinai basi ni lazima lipelekwe mahakamani. Kama hamuelewi ni kwa nini Lowassa anasema mwenye ushahidi aende mahakamani basi tena hakuna jinsi ya kuwaelewesha.

Mitambo ya Ritchond ni haramu? si ndiyo ya DOWANS na si ndiyo inayoendelea kutumiwa na Symbion? Symbion imetoa misaada kiasi gani kwa jamii na Serikali yetu, fedha zinazotumiwa kutoa misaada hiyo si zinatokana na uzalishaji wa umeme unaofuliwa na Mashine Haramu zilizoletwa na Ritchmond? Au ndiyo mambo ya Baniani Mbaya kiatu chake dawa?

Kweli mbowe amewashika sana vijana wa bavicha,mimi kanikosa safari hii nmeshtuka,haiwezekani mtu walituambia ni mwizi,fisadi papa,leo eti awe msafi gafra
 
Kweli mbowe amewashika sana vijana wa bavicha,mimi kanikosa safari hii nmeshtuka,haiwezekani mtu walituambia ni mwizi,fisadi papa,leo eti awe msafi gafra
Hebu tuambie wewe unaonaje binadamu huwa hawabadilishi mitizamo wanapopata maarifa mapya? Unajua kwamba UKIMWI unapoingia Marekani waathirika walikuwa wanafungwa nyuma ya Pik Ups na kuzungushwa mitaani kama wahalifu wa Jamii. Unadhani jambo hilo sasa hivi linaweza kufanyika huko Marekani?
 
Kwanza naomba nikiri kwamba mimi ni nwanachama halali wa chadema,najua itifaki na mlengo wa chadema,na tangu niingie kwenye siasa au kuzijua siasa nmekuwa ni mwanachadema,sijawahi kuwa chama kingine chochote zaidi ya chadema,,lowasa alipokuja chadema na kuwa mgombea uraisi ilibaki kidogo nihame chama,ila niloposoma katiba yetu ya 2006,nikakutana na kifungu kinachoelekeza wanachama kuunga mkono wagombea wanaoteuliwa na chama,,hapo nikawa sina namna mana siwezi kuvunja katiba,
Tuje kwenye makosa yetu sasa
Kiukweli chadema naipenda sana na sifikirii kuhama labda kufanyike makosa makubwa sana ila hiki chama kina matatizo kadhaa ambayo inabidi tujisahihishe,
Kosa la kwanza ,viongozi wetu wana ndimi mbili,yaani leo anaongea hili na kesho lile,kiasi kwamba unashindwa kuwaelewa,mfano"lowasa ni fisadi,lowasa ni mwizi,mkimchagua lowasa mkapimwe akili,,lowasa hafai,lowasa ameiingiza gizani n.k" kesho "lowasa mi mkombozi,lowasa ni safi,lowasa ni shujaa" kwa nini mnatufanya wafuasi wenu chapati?
Kosa la pili ni kwamba chadema hawapendi kukosolewa,yaani ukikosoa chama utaitwa msariti,mamluki,au ccm,,mfano kingunge leo tunamwita kamanda,mtu ambae kazeekea ccm maisha yake yote eti leo anaikana tena kwa sababu ya lowasa afu ukisema uitwe msariti,lowasa,ambe amekuja chadema kwa sababu ya uraisi leo hii umuamini?
Chadema tufike sehemu tutambue kwamba kuna siasa kabla ya uchaguzi,siasa wakati wa uchaguzi na siasa baada ya uchaguzi,sasa ni siasa baada ya uchaguzi tunapaswa kutambua tunakosea wapi??? Na tujisahihishe sasa.
Utawasikia wengine wakiniita majina ya ajabu hapa
 
Kwa hiyo wewe kwa Mtazamo wako ENL unamuweka katika kundi gani ?
Mwizi ama sio Mwizi ?
 
very poor indeed you need to go back to your tutor men!!!
 
Uliposoma katiba ya CHADEMA ukagundua kuwa kuna kifungu kinachowataka wanachama kuwaunga mkono wagombea wanaopitishwa na chama? Kwa hiyo ukaogopa kuhama kwa kuwa utakuwa unavunja katiba ya chama? Toka lini kuhama chama imekuwa ni kuvunja katiba ya chama? Inawezekana hujui unachokizungumza.
 
Back
Top Bottom