Ukawa Wasaka Majangili Bungeni

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
OPERESHENI Tokomeza Ujangili iliyofanyika tarehe 4 Oktoba 2013 haijafika kikomo. Vyama Vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) leo bungeni vimedai idadi ya majangili waliokamatwa,

Ni kwa kuwa, mpaka sasa wameeleza kutoona matokeo ama utekelezwaji wa maazimio ya bunge yaliyofikiwa kutokana na operesheni hiyo.

Ni operesheni ilisababisha Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa mawaziri wake wanne kufuatia wabunge kuungana bila kujali itikadi za vyama vyao kupinga unyanyasaji uliofanywa wakati huo.
Mawaziri walioondolewa walikuwa David Mathayo (Mifugo), Dk. Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii) ambaye alijiuzulu.

Esther Matiko, Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni katika Wizara ya Maliasili na Utalii wakati akiwasilisha maoni ya upinzani kuhusu Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/17 leo amesema;

“Ni muda mwafaka sasa Kambi Rasmi kutaka kuelewa ni majangili wangapi baada ya operesheni hiyo kumalizika mali zao zimekamatwa na tayari kesi zao ziko mahakamani au tayari wamefungwa?”

Esther amesema, pamoja na operesheni hiyo kuwa na athari kubwa lakini watu wengi walioathirika hawajalipwa fidia zao mpaka sasa.

Mefafanua kuwa, kwa mujibu wa Taarifa ya Serikali, vitendo vya ujangili vinavyofanyika nchini vimegawanyika katika makundi mawili

Kundi la kwanza ni Ujangili wa Kujikimu; na kwamba aina hii inahusisha watu wenye kipato kidogo na hulenga zaidi katika kujipatia kitoweo na fedha kwa ajili ya kukidhi mahitaji mengine.

Aina ya pili ni Ujangili wa Biashara; Aina hii ya ujangili inahusisha zaidi watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha na hulenga kupata nyara zenye thamani kubwa.

“Wanyama wanaoathiriwa zaidi na aina hii ya ujangili ni pamoja na Tembo, Faru, Simba na Chui,” amesema.

Amesema “…tarehe 04 Oktoba 2013 ilizindua Operation Maalum ya kupambana na ujangili huo ili kuzuia vitendo hivyo ndani na nje ya hifadhi za Taifa, katika Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu.

“Pia kuwatambua mapema majangili na kujua nyendo zao ndani na nje ya maeneo ya hifadhi kwa kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wahusika wakuu wa nyara hizo za Taifa.”

Amesema, Rais Jakaya Kikwete aliunda tume maalum iliyoongozwa na Mhe Jaji Msumi ya kushughulikia suala hilo, lakini taarifa ya tume hiyo hadi sasa imeishia kwenye makabati ya Ikulu na Watanzania hawakupata nafsi ya kuelewa nini Jaji Msumi aliona na kushauri.

“Aidha hakuna hatua zozote za fidia zimechukuliwa kwa waathirika wa operation hiyo ambao wengi walipoteza mifugo yao, walichomewa nyumba zao, walibakwa, walidhalilishwa na wengine walipoteza ndugu na jamaa zao na wengine wamekuwa walemavu.
 
Mkuu,
Ni kudharau upinzani kuwa hawajui wanachosema au ni kutokuwaona wanajua chochote? Heading na maelezo yako mbona tofauti?? Hao UKAWA waliingia na ma-rangers kule ndani ya bunge kusaka majangili humo au?

Dharau nyingine ni kujidharaulisha mwenyewe tu. Ukikaa ukaisoma vyema hiyo hotuba ya upinzani kama ulivyoiandika, nadhani utaona ukweli wake, Ila, soma ukiwa na nia ya kuielewa sio kuipinga
 
Mkuu,
Ni kudharau upinzani kuwa hawajui wanachosema au ni kutokuwaona wanajua chochote? Heading na maelezo yako mbona tofauti?? Hao UKAWA waliingia na ma-rangers kule ndani ya bunge kusaka majangili humo au? Dharau nyingine ni kujidharaulisha mwenyewe tu. Ukikaa ukaisoma vyema hiyo hotuba ya upinzani kama ulivyoiandika, nadhani utaona ukweli wake, Ila, soma ukiwa na nia ya kuielewa sio kuipinga
Kama unashirikisha ubongo utanielewa
 
VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YETU.
Majambazi yampasua kichwa rais.

Simba ya sasa itaua mtu.

Yanga yasema haponi mtu.
RAY kufungwa miaka 3..........ikibainika alisema uongo
 
Mkuu,
Ni kudharau upinzani kuwa hawajui wanachosema au ni kutokuwaona wanajua chochote? Heading na maelezo yako mbona tofauti?? Hao UKAWA waliingia na ma-rangers kule ndani ya bunge kusaka majangili humo au? Dharau nyingine ni kujidharaulisha mwenyewe tu. Ukikaa ukaisoma vyema hiyo hotuba ya upinzani kama ulivyoiandika, nadhani utaona ukweli wake, Ila, soma ukiwa na nia ya kuielewa sio kuipinga
Huyu jamaa ushabiki unamsumbua
 
Kwahiyo unakiri ccm kuna mashine yakutengeneza mafisadi
Sina uhakika kama jina lako "mwanahabari huru" ni reflection ya career yako...kama ni kweli basi nakuonea huruma sana.

Kama mwanahabari, you are meant to be neutral and objective! You are only supposed to report news and create space for your audience to discuss...you are not supposed to be an active participant...your work is only to report what happened [you r not suppose to take sides]..
 
Tume zinaundwa kila kukicha,outcome zinafungiwa kabatini,wakiuliza mnashangaa na kuuliza mantiki ya hotuba au swali.

Ndugu zangu tuwe realistic kuna mambo are there for the benefit of this lovely nation sio kwa benefit of our affiliate political political parties .

Let's be realistic ujangili haufai wanyama wetu wanatokomea,Kesho tutakosa watalii na pato la taifa litashuka na hili linamgusa kila mtanzania no matter chama kipi unashabikia.
 
Tume zinaundwa kila kukicha,outcome zinafungiwa kabatini,wakiuliza mnashangaa na kuuliza mantiki ya hotuba au swali.
Ndugu zangu tuwe realistic kuna mambo are there for the benefit of this lovely nation sio kwa benefit of our affiliate political political parties .
Let's be realistic ujangili haufai wanyama wetu wanatokomea,Kesho tutakosa watalii na pato la taifa litashuka na hili linamgusa kila mtanzania no matter chama kipi unashabikia.
Eti wanasaka majangili wakati jangili kubwa lao wanakula nalo sebuleni!
 
Back
Top Bottom