UKAWA Wanadharau Mahakama

Mkuu Jabulani,
Ulikuja na mbwembwe kibao kumbe ulikuwa moto wa mabua?
 
Last edited by a moderator:
Hapana Mkuu Buchanan, sikuja kwa moto wa mabua. Mimi ni mhandisi, huwa nazingatia sana efficiency ya kila activity. Wakati mwingine huwa najitoa katika mjadala iwapo naona ninatumia nguvu nyingi (input) kuhoji kitu lakini kila jibu linalokuja (output) linakuwa halijatoa hasa mwangaza wa ninachohoji.

Ninachosema ni hiki, hukulitendea haki swali langu, nikaona utakuwa umefika mwisho wa uelewa wa hoja yangu, sasa badala ya kulazimisha nipewe majibu, nikaona niachane na mambo ya kurudia rudia maswali. Ulileta hukumu ya Kubenea vs Mwanasheria, nikakuhoji tafsiri ya hukumu, ukarudi kusema kwamba thread yako haijazingatia hukumu bali sababu za hukumu, sasa nikawa najiuliza, kama ni sababu, ina maana mahakama 'imetamka' sababu, na sio hukumu? Angalia hapo nimekuquote ulichosema kwamba mahakama 'ilitamka wazi'. Sasa kama ilitamka, itakuwa iltamka kwenye nini kama sio kwenye hukumu? Kwa nini nakuomba unitafsirie hukumu unakuja kusema hutaki hukumu ila 'sababu za hukumu'? Nikagundua either hautaki kutafsiri hukumu au hauwezi kutafsiri hukumu. Nikaona natumia input kubwa kupata output ndogo and hence low efficiency. Nikaamua kuachana na thread hiyo kwani inawezekana tukawa tunajaza space ya server yetu bila kupata tunachotaka.
 
Okay, mkuu kama unapata efficient ndogo kutoka kwangu nisikulazimishe kujadiliana na mimi! Kila lakheri na shughuli za uhandisi!
 
Uiambie mahakama iwaamuru UKAWA waache kudharau uamuzi wa mahakama.
Mkuu,
Kwa nini wewe usiiambie Mahakama iwaamuru wana-UKAWA waache kudharau maamuzi yake?
 
Na wewe utajisifu kwamba umechangia mada?

Kwani majaji wanateuliwa na nani, unatagemea nini lazima walipe fadhila, tatizo mfumo mbovu na tumelalamika sana mfumo ubadilishwe kupitia katiba, tulifurahi sana baada ya warioba kutuletea rasimu ambayo watu wengi waliikubali lakini ccm wameturudisha nyuma sijaona tofauti ya kimfumo kati ya katiba ya 77 na hii katba pendekezwa
 
Kinacho-matter kuhusu Majaji ni "Security of Tenure" na sio namna wanavyoteuliwa!
 

We mjamaa, k=unauliza kwa nini asiseme hivi???..yeye ndo kaona hivyo, wewe toa mtazamo wako ila usiweke maneno kwenye kinywa cha mtu.

Mungu akusaidie.
 
CCM wamedharau mara ngapi mahakama na wewe ukanyamaza? Acha hizo!!! Tambua haki zako unaibiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…