UKAWA walipotoka Bungeni walishasaini posho?

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,305
3,327
Hakuna haki bila wajibu na hata katika vitabu vitakatifu vya Mungu imeandikwa asiyefanya kazi na asile.
Juzi tumeshuhudia UKAWA wakitoka nje ya bunge kwa kile kinachoitwa kupinga matangazo ya bunge kutokurushwa live.
Hii ni haki yao ya msingi lakini kwa upande mwingine kuna hili swala la posho za vikao vya bunge ambalo msingi wake ni uwajibikaji wa mbunge kwenye kikao cha bunge.
Je wabunge wa UKAWA wana haki yakupokea posho ya kikao huku hawakutimiza wajibu wao kwenye majukumu ya bunge?
 
Mkuu, hao jamaa wapo smart kweli. Yaani wanasaini kwanza posho ndo wanatoka nje. Kesho yake hakuna mgomo tena. Wanaingia kama kawaida na wanashiriki kile walichokataa jana yake
 
Kuna ulazima wakurekebisha kanuni za bunge,alaghai wa namna hii kwenye pesa za walipa kodi si wakuufumbia macho.
 
Je wabunge wa UKAWA wana haki yakupokea posho ya kikao huku hawakutimiza wajibu wao kwenye majukumu ya bunge?

BIBLIA kitabu cha 2thesalonike 3:10 inasema "Mtu asiyefanya kazi, asile." Wametenda dhambi ya kula bila kufanya kazi. Wakiumwa matumbo ya kuharisha wasimlaumu Mungu kwani wamekula chakula cha dhuluma.
 
Kitendo cha kuingia bungeni na kuonyesha hisia zao na kutoka nje kwa ajili ya woga wa wabunge wa Ccm kutokujua kujenga hoja tayari ni uwakilishi tosha na kumbukumbu zimehifadhiwa kwa kizazi kijacho.
Hivyo wanastahili posho zao na pongezi kuliko wale wanao lala mwanzo mwisho na kusema ndiyo hata kwa michango ya ajabu.
 
Kitendo cha kuingia bungeni na kuonyesha hisia zao na kutoka nje Hivyo wanastahili posho zao na pongezi .

Mojawapo ya kazi za mbunge ni kutoka nje bungeni na kuacha mijadala? Kwenye ilani zao waliliweka hilo? Walipoomba kura waliwaeleza wazi wapiga kura kuwa watakuwa wakitimka bungeni wakati vikao vinaendelea?
 
Ni muda wa kuanda kanuni zza bunge upya mfano wabunge wasain baada ya kikao na sio kabla hii itafanya watu wasifanye wizi mweupeee
 
Hakuna haki bila wajibu na hata katika vitabu vitakatifu vya Mungu imeandikwa asiyefanya kazi na asile.
Juzi tumeshuhudia UKAWA wakitoka nje ya bunge kwa kile kinachoitwa kupinga matangazo ya bunge kutokurushwa live.
Hii ni haki yao ya msingi lakini kwa upande mwingine kuna hili swala la posho za vikao vya bunge ambalo msingi wake ni uwajibikaji wa mbunge kwenye kikao cha bunge.
Je wabunge wa UKAWA wana haki yakupokea posho ya kikao huku hawakutimiza wajibu wao kwenye majukumu ya bunge?

Kutoka ndani ya bunge ni njia mojawapo ya kuelezea ubaya wa yale yanayoendelea ndani na sioni shida kwa wao kuchukua posho. Mbona tusianze na wale mabingwa wa kusinzia bungeni? Wengine zaidi ya kusema ndioooo hawana na hawawezi kuchangia chochote. Tuanze na hao kwanza.
 
Kitendo cha kuingia bungeni na kuonyesha hisia zao na kutoka nje kwa ajili ya woga wa wabunge wa Ccm kutokujua kujenga hoja tayari ni uwakilishi tosha na kumbukumbu zimehifadhiwa kwa kizazi kijacho.
Hivyo wanastahili posho zao na pongezi kuliko wale wanao lala mwanzo mwisho na kusema ndiyo hata kwa michango ya ajabu.
Ni katiba ipi imeandika kazi ya wabunge ni kuonesha hisia?
 
Back
Top Bottom