UKAWA wakutana kwa dharula

UKAWA wakutana kwa dharula

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
15,202
Reaction score
25,378
Dar es Salaam. CHADEMA kwa kushirikiana na vyama vinavyounda UKAWA, leo wanakutana kujadili mwenendo waliouita usio halali wa kutangaza matokeo, wakiituhumu Tume ya Uchaguzi (NEC), CCM na Jeshi la Polisi kushirikiana kuhujumu matokeo.

Viongozi hao wa UKAWA, Freeman Mbowe, ambaye ni mwenyekiti wa CHADEMA, James Mbatia (mwenyekiti, NCCR Mageuzi) na Profesa Abdallah Safari, ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA walizungumza na waandishi wa habari jana Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Mbowe aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa kuna vijana kutoka Kenya, ambao wamewekwa hoteli mmoja Dar es Salaam ambao wanafanya kazi ya kuchakachua matokeo yanayotoka majimboni na baadaye kuyapeleka NEC.

Ndio maana matokeo yaliyopo kwenye fomu za mawakala wetu yanatofautiana na matokeo yanayotangazwa na NEC,? alisema mwenyekiti huyo wa CHADEMA.

Aliyataja baadhi ya majimbo hayo kuwa ni Nyamagana, Rungwe, Kahama Mjini,Shinyanga Mjini, Kyela na Muleba Kusini.?Kazi hii ya uchakachuaji matokeo inafanywa na CCM, inaratibiwa na NEC na wasimamizi wakubwa ni polisi?

Alisema Mbowe Akichangia suala hilo, Profesa Safari alitoa mfano wa Jimbo la Tandahimba ambako alisema NEC ilitangaza kuwa mgombea wa CCM, Dk John Magufuli alipata kura 49,098 na Lowassa kura 46,288 ambazo ni tofauti ya kura 280.?Lakini matokeo halisi kutoka kwa mawakala wetu yanaonyesha Lowasa alipata kura 44,537 na Dk Magufuli 44,253 ambazo ni tofauti ya kura 284,? alisema Profesa Safari.

Pia alisema NEC ilitangaza kuwa Lowassa alipata kura 6,000 Jimbo la Tunduma, wakati matokeo yao yanaonyesha alipata kura 32,442.

Mbowe pia alizungumzia vijana 191 waliokamatwa na polisi, ambao nane kati yao walifikishwa mahakamani jana kujibu mashtaka ya kufanya makosa ya kimtandao.

Kitendo kilichofanywa cha kuwanyima dhamana ni cha kinyama hakistahili,? alisema Mbowe?Kwanza kuna wageni wawili ambao hawahusiki kabisa na shughuli za ujumlishaji matokeo ya CHADEMA.?

Alisema kitendo cha polisi kuwakamata vijana hao waliokuwa wakijumlisha matokeo, kimevuruga mfumo wa ukusanyaji matokeo wa CHADEMA.

Lakini sasa tunatumia fomu za mawakala wetu ambazo zinaonyesha (mgombea urais wa CHADEMA, Edward)Lowassa anaongoza kwa tofauti kubwa ya kura,? alisema Mbowe.

Alisema vijana hao wamekamatwa kwa kosa ambalo linafanywa na mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM, January Makamba ambaye Mbowe alisema amekuwa anatangaza matokeo ya uchaguzi na idadi ya majimbo bila ya kuchukuliwa hatua zozote.

Huu si uchaguzi, ni uchafuzi,? alisema Mbowe. Hata hivyo, Makamba alisema jana kuwa hakuna tatizo la yeye kusema kuwa watashinda kwa asilimia fulani kwa sababu kila chama kimekuwa kikisema hivyo.

Hali hii inatufanya tuamini sababu za NEC kuchelewesha Daftari la Wapigakura na kutoruhusu wapinzani kukagua mfumo wa kujumlisha matokeo. "Mbowe alisema wanalazimika kujadili sasa suala hilo kwa kuwa katiba hairuhusu matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani.

Alisema Kamati Kuu ya CHADEMA inakutana leo jijini Dar es Salaam kujadili suala hilo na kutoa tamko na pia kikao cha viongozi wa Ukawa kitakutana leo kutoa mwelekeo wa uchaguzi.

Akizungumza kwenye mkutano huo na waandishi, Mbatia alisema:Hili ni janga la Taifa linalotengenezwa na binadamu huku wakijua athari zake.? Nchi ni mali ya watu wote na ukawa hawataki machafuko. NEC ikiendelea inaweza kukamilisha ile kauli kwamba uchaguzi wa mwaka huu utakuwa si huru.?

Unaweza kuchakua matokeo lakini huwezi kuchakachua hisia za Watanzania,? alisema Mbatia. Alisema kinachotokea ni kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kukataa mapendekezo ya vyama vya upinzani waliomtaka abadili mambo manne kwenye katiba kabla ya uchaguzi.

Aliyataja mamnbo hayo kuwa ni matokeo ya urais kuhojiwa Mahakamani,kuruhusiwa kwa mgombea binafsi, mgombea urais ashinde kwa zaidi ya asilimia 50 na tume ya uchaguzi kuwa huru.

Chanzo: Mwananchi
 
Nec wasicheze na hisia zetu tafadhali,watende haki la sivyo nchi itapasuka na itashindwa kutawalika,
Hatukukesha kwenye foleni ya kupiga kura kumpigia mpiga push up,lubuva nchi ipo mikononi mwako,maana naona kila ukipewa airtime ya kutangaza matokeo unajiteteatetea,
 
Nawashauri UKAWA wakubali matokeo. Mimi binafsi ni mwana Ukawa.
 
Teyari wamesha gundua kuwa GIA YA ANGANI haikufanya kazi.


Huwezi kumchafua mtu kwa MIAKA 10 halafu umsafishe kwa siku 60.
 
Nategemea baada ya kutoka kwenye kikao na wao watajitangaza washindi kama Maalim Seif Hamad.
 
NEC ya CCM itaingiza nchi hii katika vita...!!! I see it..!! Sbb matokeo ya URAIS yanachakachuliwa wazi wazi..!!
 
Nec wasicheze na hisia zetu tafadhali,watende haki la sivyo nchi itapasuka na itashindwa kutawalika,
Hatukukesha kwenye foleni ya kupiga kura kumpigia mpiga push up,lubuva nchi ipo mikononi mwako,maana naona kila ukipewa airtime ya kutangaza matokeo unajiteteatetea,

Hapo sawa, lakini wacheze na maamuzi yetu?
 
Uloi nga mâché68;14484305 said:
jilaumuni ninyi wenyewe kwa kumfukuza DR SLAA na kula matapishi yenu!
Hilo wamelisahau! Wamebaki kulia lia kwa kumlahumu kila mtu hisipokuwa wao.Niliwambia tangu mwanzo kwamba dhambi ya kumtimua DK.SLAA itakuja kuwatafuna-kikowapi sasa?
 
Teyari wamesha gundua kuwa GIA YA ANGANI haikufanya kazi.


Huwezi kumchafua mtu kwa MIAKA 10 halafu umsafishe kwa siku 60.

kwenye mpira unaweza kupata point za mezani, umecheza uwanjani unashindiwa mezani. ...
 
Haki itendeke na jaji lubuva atatuingiza kwenye machafuko Tanzania
 
Sarakasi za Wanasiasa, msingi mkuu kwao ni Uongo. Usimwamini mwanasiasa, hasa wale wa gia za angani, waliwahi kutuaminisha kuwa Slaa alishinda, mwisho wa siku ikawa si Kweli. Kubwa kuliko zote ni kudai wana ushahidi unaothibitisha madai yao ya 'the list of shame' . Mwisho wa siku Number 9 ktk hiyo list ndie Mgombea wao.
 
Mkuu wa ujumbe wa waangalizi wa Sadc (SEOM), Oldemiro Julio Baloi alisema licha ya kasoro ndogo ndogo zilizojitokeza siku ya kupiga kura, bado changamoto hizo hazikuweza kuathiri mchakato mzima wa upigaji kura. Alisema watu walijitokeza kupiga kura na kuvumilia muda wote mpaka zoezi hilo lilipokamilika.

"Tumefuatilia uchaguzi kuanzia ufunguaji wa vituo mpaka wanapofunga. Tumebaini kwamba katika vituo mbalimbali tulivyoviangalia hali ilikuwa shwari na watu wameweza kupiga kura zao kwa amani na utulivu," alisema.

Balozi ameongeza kuwa pamoja na mafanikio hayo, bado kuna maeneo ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi kikamilifu ili kuboresha mazingira ya uchaguzi ujao. Aliyataja mambo hayo kuwa ni kumaliza changamoto zilizojitokeza wakati wa uandikishaji kwa kutumia mfumo wa BVR.

Kiongozi huyo amesema waangalizi wa Sadc walikutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi na kupokea malalamiko yao tangu wakati wa uandikishaji. Hata hivyo, aliipongeza Tume ya uchaguzi kwa kufanikiwa kuendesha uchaguzi kwa wakati.

"Serikali pia ijitahidi kuongeza ushiriki wa wanawake katika chaguzi kuanzia ngazi ya vyama mpaka wagombea. Pia, makundi ya watu wanaosahalika ni muhimu katika uchaguzi, ni vizuri sauti zao zikasikika," alisema Baloi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya nje wa Msumbiji.

Waangalizi hao wamependekeza vyama vya siasa kushiriki katika kutoa elimu kwa mpiga kura kipindi cha kampeni ili kusaidia wananchi ambao hawana uelewa juu ya masuala ya uchaguzi na jinsi ya kupiga kura.

SEOM imeridhishwa na uchaguzi mkuu wa Tanzania na kwamba unatosha kueleza matakwa ya Watanzania kupitia kura zao. Baloi alisisitiza kuwa kasoro ndogo ndogo zilizojitokeza kama vile kutokea kwa vurugu na kuchelewa kufunguliwa kwa baadhi ya vituo, hazijaweza kuathiri sehemu kubwa ya upigaji kura.

Mkuu wa Waangalizi wa Umoja wa Afrika (AU), Armando Guebuza alisema lengo la uangalizi wao ni kutathmini uchaguzi bila upendeleo kwa kuzingatia sharia na kanuni mbalimbali zinazoongoza uchaguzi hapa Tanzania.

Guebuza aliipongeza NEC kwa kuendesha uchaguzi kwa wakati bila kuathiri masharti yakisheria na kanuni mbalimbali za uchaguzi. Alisisitiza kuwa changamoto zilizojitokeza ni za kawaida zinaweza kutatulika katika uchaguzi ujao.

"Asilimia 95 ya vituo tulivyoviangalia vilikuwa wazi ndani ya wakati unaotakiwa kisheria na vilikuwa na vifaa vyote muhimu. Maandalizi ya NEC yalikuwa mazuri licha ya changamoto za manunuzi walizokumbana nazo," alisema.

Guebuza ambaye alikuwa Rais wa Msumbiji alisema vyombo vya habari vimeonekana kuwa na upande wakati wa kampeni. Alisema baadhi ya vyombo hivyo sasa vimeanza kutangaza matokeo, jambo linaloweza kusababisha migogoro isiyo ya lazima.

Naye Kiongozi wa Waangalizi wa Jumuiya ya Madola, Goodluck Jonathanalisisitiza kuwa bado wanaendelea kuangalia uchaguzi kwa sababu bado hatua ya utoaji matokeo inaendelea. Alisema ripoti yao ya awali inaonyesha kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wazi.

"Kwa sasa tunasema uchaguzi huu ulikuwa na ushindani mkubwa na ulifanyika katika mazingira ya haki na uwazi. Kama kutatokea kasoro zozote katika hatua ya mwisho ya kutangaza matokeo basi tutaambatanisha mapungufu hayo katika ripoti yetu ya mwisho," alisema.

Jonathan ambaye pia alikuwa Rais wa Nigeria alisema suala la kukaa umbali wa mita 200 kutoka kwenye kituo cha kupigia kura halikuwa tatizo siku ya uchaguzi. Alisema polisi walikuwepo katika maeneo mengi katika kuangalia usalama.

Kiongozi huyo alibainisha kuwa mazingira ya siku ya uchaguzi yaliandaliwa vizuri na kufanya uchaguzi huo kuwa huru na wa haki. Alisisitiza kwamba matokeo ya uchaguzi yatawakilisha maamuzi ya wananchi wa Tanzania.

-
 
Back
Top Bottom