georgemwaipungu
JF-Expert Member
- Jul 7, 2015
- 2,779
- 589
BREAKING NEWS:UKAWA WAITISHA KIKAO CHA DHARULA KESHO:
Kufuatia hali kuwa tete ndani ya kambi ya UKAWA, viongozi wa vyama vinavyounda umoja huo wanatarajia kukutana kwa dharura kesho kujadili mwenendo wa umoja wao.
Taarifa za ndani ya UKAWA zinasema Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ambaye yupo nchini Marekani atalazimika kurudi haraka nchini na inaelezwa huenda akaingia usiku huu au mapema kesho kwaajili ya kikao hicho cha dharura ambacho kitaamua hatma ya umoja huo.
Mbali na Mbowe, timu yote ya kampeni za mgombea urais na mgombea mwenyewe pamoja na mgombea mwenza wanatarajia kusitisha kampeni na kurudi Dar es Salaam kwa siku ya kesho hadi watakapopata mwafaka wa masuala yanayobishaniwa ndani ya umoja huo.
Taarifa zinasema, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa viongozi wa CUF kulalamikia kutotimizwa kwa makubaliano yaliyofikiwa wakati wanaungana na kupjnga jinsi Chadema wanavyoendesha umoja huo hadi kufikia hatua ya mgombea mwenza wa Chadema Juma Duni kutangaza kujitoa kwenye chama hicho na inaelezwa kikao hicho kitatumika kumuomba asijitoe.
CUF wanalalamikia UKAWA kuendeshwa na mtu mmoja ambaye ni Mbowe badala ya kuendeshwa kama taasisi na amekuwa akichukua maamuzi bila kushirikisha wengine.
"UKAWA ni Mbowe na yeye ndo anaendesha mambo anavyotaka kwa maslahi yake na mkwewe mzee Mtei. Huu ni uhuni ambao tulikuwa tunausikia tu ila leo tunajionea baada ya kuingia ndani" alisema kiongozi mmoja wa CUF ambaye alisisitiza kama Mbowe lengo lake lilikuwa ni kuua CUF amefanikiwa ila dhambi hiyo itamtafuna na watahakikisha Chadema haibaki salama.
Chama kila kukicha ni migogoro, wakubwa wanagawana wenyewe afu shida tunapata sisi wanainchi wa kawaida. Hata tutakuwa makini kutokubali ujinga huu kamwe.
kwa mtindo huu tz hatuwezi kuendelea
Mbowe kama ameenda Marekani anatuacha tunapambana wenyewe hapo kuna shida huko juu, kibaya zaidi mgombea wetu ni shida kujieleza mwenyewe.
Time will tell.....ila Lowasa hafai kuwa kiongozi wetu
Mahaba mwanawane ni kitu kibaya sana, basi tuseme ukawa ni Kundi la malaika hakuna kukosea, lakini nawaambia mtakuja kuumbuka vibaya sana,wekeni kumbukumbu na mitusi yenu
hata kwetu Kibondo madiwani wameweka watatu kila chama kimeweka mgombea hivyo basi wanampa nafasi mgombea Wa CCM kupita kwa urahisi
Tamaa na uchu wa madaraka unaviponza vyama vya upinzani. Mzee kununua chadema imekuwa ni pigo tosha la kuwapoteza kabisa kisiasa.
Babu Duni leo alikuwa viwanja vya Barafu Mburahati na Jumapili atakuwa mkoa wa Manyara Katesh Hanang.
Una lingine la kuzusha!?
Washapigwa asubuhi kama wataendelea na migogoro yao. Tatizo ni tamaa ndo inayowasumbua hawa viongozi, wanachama nao ndo fuata upepo, mbaya zaidi ukiwauliza kwa nini mzee hakuna jibu la msingi zaidi ya kutamka mabadiliko.
Hivi ukawa niambieni hasa, kinachowaaminisha kuwa mshachukua nchi ni nini?
Naomba majibu ya kueleweka plz
Hotuba ya Lusinde bungeni alifananisha ukawa ni kama kuweka mayai mengi ndani ya kapu moja akitokea mtu mwenye shabaha akalipiga lile kapu ndo kwisha habari yake
Nakwambia lowasa anasaidia kuongeza viti vya urais wala sio kuwa rais, na snayebisha akiwa rais animate kichwa
Nakwambia lowasa anasaidia kuongeza viti vya urais wala sio kuwa rais, na snayebisha akiwa rais animate kichwa
Shida ya nini wakati lowasa anasaidia kuongeza viti vya ubunge tu,urais atausikia icu
UKAWA have planted the seeds of their own destruction..nilishasema mpaka Oct 25 hawa jamaa hawatokuwa wamoja..keep watching
Milembe bado yupo lowasa maana akili take imeoza na ndo maana hata pg take moja ya hotuba hawezi kuiweka kichwani,
Tehtehteh hivi unachoongea una uhakika nacho au unaongea tu kujifurahisha?! Ukweli ni kwamba ukawa hali ni tete na mbowe ndo kawafikisha hapo.. Sometimes mkubali kupikea ukweli mchungu. . Usijifanye hujaona jana walichokifanya viongozi wa nccr... Au wao sio ukawa?? Na Duni je, kaishia wapi?? Think BIG..