Mdau issue ya Migogoro ya ardhi haina itikadi,unless hutembelei vijijini.Mi this week nilikuwa Kata ya Mkata,wilaya ya Kilosa.Nimeongea na wanakijiji wananiambia hawana sehemu ya kulima kwa sababu kuna mwekezaji amepewa eneo kubwa ameanzisha ranchi.Lakini pia wameniambia kuwa kuna migogoro kila mara baina ya wafugaji wa kimasai na wakulima wanaojiegesha kwenye vipande vya ardhi .Ambapo wamasai huingiza mifugo mashambani mwao.Na kesi huisha kisanii kwani watendaji wameshikwa na wafugaji.Nakushauri nenda Wilaya ya Kilosa tembelea maeneo haya hapa
1.Kimamba
2.Mkata
3.Pararakwio
4.Rudewa
5.Tindiga
6.Malui
7.Mbwade.
Mimi nilikuwa huko Jumatatu mpaka Jumatano wiki hii inayoish leo.
Usiingize siasa kwa mambo yanayowaathiri wananchi ambao wengi hawana hata itikadi za kisiasa.
Chukua ushauri
Utatenganisha vipi Kati ya Serikali iliyopo na Chama tawala!Na pia utatenganisha vipi Kati ya wananchi na Ilani ya chama walichokichagua kutawala? Waungwana palipo na tatizo hupaona na kutafuta ufumbuzi!Sasa unaposema siasa haihusiki ninakushangaa!