Muungano wa vyama vya Chadema,CUF,NCCR na UMD kuelekea uchaguzi mkuu 2015 waweza kuwa neema kwao kama watakuwa wamejipanga au maafa makubwa kama hawatajipanga mapema kukabili changamoto ambazo watakutana nazo zingine zikiwa za asili na zingine zikiwa za KUTENGENEZWA na mahasimu wao wakubwa ambao ni chama wanachokusudia kukitoa madarakani.
Sasa hivi vipo vikao vya viongozi kupanga nini wafanye katika ushirika wao huo, sio vibaya ila mimi ningeshauri sasa ni wakati wakuunda timu kabambe ambayo sio ya viongozi pekee bali ikishirikisha wataalamu wengine wa siasa, Uchumi,Ushirikiano wa kimataifa na nyanja nyingine hata za kijasusi (nieleweke vizuri hapo) ili kuweza kupata ushauri wa jinsi ya kuendesha umoja huo vyema katika miono tofauti ya vyama vyao, kujua jinsi ya kupata support ya ndani na nje ya nchi na hta muundo gani utakuwa wa serikali kama watafanikiwa kushinda badala ya kusubiri majaliwa.
Timu hiyo sio lazima kuchaguana kutoka ndani ya vyama bali hata ajira zinaweza kutolewa kwa wale watakao chaguliwa kwa weledi wao ili walipwe kulingana na kazi zao watakazo fanya.
Kuitoa CCM madarakani kwa kusubiri vikao vya viongozi pekee na kutoa matamko sidhani kama itakuwa rahisi ni lazima wawepo watu wapanga mikakati 24/7 na hivyo vichwa viwe vichwa kweli ndio malengo yatatimia, vinginevyo November watu watarudi na malalamiko tuu na CCM kwao malalamiko ni wimbo mzuri wa kutafutia usingizi.
Nawasilisha.