Kuna mzee mmoja aliwahi kuniambia miaka ya nyuma, kwamba usimuamini mwanasiasa hata kidogo labda jina lake tu, na hata lenyewe lifanyie uchunguzi unaweza kukuta ni la kufoji. Freeman Mbowe tangu alipoigeza chafu kuwa safi, nimejikuta nikiyakumbuka maneno ya mtu aliyenizidi sana umri.
Upinzani unahitaji vision mpya, busara mpya, hekima mpya, la sivyo shimo watakalozama wapinzani mwaka 2020, hakuna atakayekuwa na kamba ya kuwavuta na kuwaokoa, inabidi wajipange kweli kweli la sivyo watazidi kupotezwa. Siasa za kwenye facebook, instagram na mitandao mingine haziwezi kuwapa credibility mbele ya mamilioni ya wananchi wa vijijini.
Na JPM ni mjanja sana ameanza tangu mwanzo kuongea lugha moja na wananchi wa hali ya chini. Na wao wanamuona kama ni mwenzao, kitendo cha yeye kula chakula pale airport Mwanza kinaweza kisieleweke kwa masharobaro wa UKAWA ambao wanaamini katika sifa za usafi sana za mijini. Lakini JPM amejisogeza karibu kabisa na mwananchi hivyo upinzani utafute mikakati hai ya kuweza kuonyesha kwamba CCM inahitaji mbadala wa haraka, vinginevyo itakula kwao na watabaki kutafuta huruma kwa kusema wameibiwa kura.