Ukawa waanza ziara ya siku 10 Bara

Ukawa waanza ziara ya siku 10 Bara

rosemarie

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
6,887
Reaction score
3,439
Dar es Salaam. Wakati Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ukitarajiwa kuanza ziara ya siku 10 katika mikoa ya Tanzania Bara kesho, viongozi wa umoja huo wamemvaa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa kauli yake kuwa Katiba haina umuhimu.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema jana kwamba ameshangazwa na kauli ya Kinana kwa kuifananisha Tanzania na Uingereza ambayo haina Katiba.

“Kauli hii imenipa matatizo, naanza kutilia shaka kisomo cha hawa wenzetu...“Hawana Katiba ya kuandika lakini wana sheria zao ambazo wanaziheshimu, ndiyo maana huwezi kuwahoji kuhusu Malkia Elizabeth wakakuelewa.

Mikutano ya Ukawa

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro alisema awamu ya kwanza ya ziara hiyo itaanza kesho hadi Mei 26, mwaka huu.

Alisema ili kufanikisha ziara hiyo, Ukawa imejigawa katika timu tatu ambazo zitakuwa zinafanya mikutano na maandamano ya amani.

Kundi la kwanza litaongozwa na Katibu Mkuu wa NCCR- Mageuzi, Mosena Nyambabe, la pili litakuwa na Dk Slaa na la tatu litakuwa chini ya Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba.
 
Agenda tafadhali na watatumia Chopa au L/Cruiser.
Warning;Barabara ni mbovu sana so wawe na watu wakusukuma magari kbs.
 
Badala ya kupeleka ruzuku ktk matawi mikoani kuimalisha chama uchaguzi wa serikari za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani mnapoteza pesa tu uchaguzi ukifika mnaanza kutafuta sababu.
 
Tuko pamoja hapo ukawa naomba ziara ianzie huku rock city,hapo ccm wataisoma namba,tanganyika lazima ipatikane
 
Ukawa inatafanya jambo la maana iwapo watamsimamisha mgombea mmoja wa Urais anayetokea Zanzibar ili kuondosha uvumi kuwa hawapendi muungano.
 
Kwenye hiyo mikutano yao wasiache kuwafunda watanzania umhimu wa kupiga KURA.
 
U-K-A-W-A wao Bunge la BAJETI haliwahusu??? :A S 13:

Mathematics, Mbunge mmoja wa UKAWA anatosha nguvu ya wabunge 200 wa CCM hivyo wabunge wawili wa UKAWA wnatosha ndani ya Bunge la Bajeti linalo endelea hivi sasa.
 
Badala ya kupeleka ruzuku ktk matawi mikoani kuimalisha chama uchaguzi wa serikari za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani mnapoteza pesa tu uchaguzi ukifika mnaanza kutafuta sababu.

Leo umekua mtetezi wa upinzani au unatoa ushauri?
 
Leo umekua mtetezi wa upinzani au unatoa ushauri?

Natoa ushauri wa bure mkuu, bunge liko Dodoma, ajabu hata ofisi ya chadema mjini imefungwa, ukiuliza watu wanatafuta riziki mpaka uchaguzi ukaribie, hakuna mishahara wala posho mtu akae kufanya nini hapo?
 
Back
Top Bottom